Biashara ya boda boda

Biashara ya boda boda

Mie pia nafanya hiyo biashara lakini hesabu zako naona kama hazijakaa vizuri.
Boxer ya kisasa BM 150 mpya in Full pamoja na Comprehensive insurance si chini ya 2.3m kwa sasa kwa wakala mkuu.
Sasa kufika bodaboda 10 si chini ya milioni 23.
Sasa kwa akili ya kawaida na kwa biashara hii ilivyo kwa sasa sidhani na sishauri mtu afike mtaji huo wote auweke kwenye biashara ya Bodaboda.
Ni mtaji mkubwa sana unaweza kuugawa na ukaingiza hesabu nzuri sana kwa biashara pacha.
Tabia ya kuwekeza biashara moja ni hatari sana tena sana,watu kipindi cha nyuma miaka ya 2008 kushuka chini watu na wafanyakazi wa serikali walikimbilia sana kuchukua mkopo wanunue Taxi,wengine hawakusoma alama za nyakati,sasa hivi hakuna hata mmoja anaetaka kusikia habari hiyo.
Wakahamia kwenye Hiace dungu,wakati sinaruhusiwa kuingia mjini,baada ya muda nako wakalia,kuna watu walikuwa nazo hadi 5,leo ni majanga hawaju wafanye nini nje ya mji ambapo pia ziilikuwepo nyingine zenye uzoefu na route za huko.
Leo hii Coaster nazo zimo safarini.
Kwahiyo Jaribu kuwekeza kwenye Biashara kwa kiasi hasa hizi.Usizidi Bodaboda 5.La sivyo utalia kaka.
 
Wana JF,

Sikuwahi kudhani hapo nyuma kama bodaboda inaweza kutajirisha mtu kwa kumtengenezea mpaka Tshs 3 millioni kwa mwezi (other factors remain constant) kwa kuanza na bodaboda moja tu!

Imagine umenunua bodaboda MPYA aina ya Boxer (pamoja na gharama zingine kama insurance nk) kwa Tshs 1.7 million.

Kwa hapa Dar, kila siku bodaboda inaingiza Tshs. 10,000 (kama umeajiri dereva akupigie kazi). Hivyo kwa wiki unapata Tshs. 70,000 ambayo kwa mwezi ni Tshs 280,000 Net.

Kwa mapato hayo ya mwezi, itakuchukua takribani miezi 6 kurudisha mtaji wako wote. Hivyo kuna option 2, kuuza bodaboda na kuongeza fedha kidogo ili upate zingine mbili, au kuendelea kubaki nayo kwa miezi mingine 6 ili ununue nyingine na ziwe 3.

Hii maana yake ni kwamba, ndani ya mwaka (if other factors are constant) unaweza kuanza na bodaboda moja na kuufunga mwaka na bodaboda 3!

Unaweza kufanya hesabu ili kupata mapato ya mwezi kwa bodaboda 3. Hivyo kama mambo yataendelea vizuri, kuna uwezekano ndani ya miaka 3 kuwa na boda zaidi ya 10 na kufanya pato la mwezi kuwaTshs 2. 8 millioni.

Other factors being constant. That is the catch, kwani they are never constant. Kijana hatoleta sh 70,000 kwa wiki, then atapata ajali then atafungwa au kuibiwa. Doesnt work that way kwenye biashara
 
Other factors being constant. That is the catch, kwani they are never constant. Kijana hatoleta sh 70,000 kwa wiki, then atapata ajali then atafungwa au kuibiwa. Doesnt work that way kwenye biashara

Ni ushauri mzuri. Na sio mara zote 'other factors' zitakuwa kama zilivyo. Kuna siku utapaleka chombo kwenye matengenezo, ujue hio 10,000 haitapatikana. Siku dereva akiugua ujue ndo siku ishaenda, siku akiletewa shobo na polisi ama TRA ndio siku ishakata, etc.
 
Wana JF,

Sikuwahi kudhani hapo nyuma kama bodaboda inaweza kutajirisha mtu kwa kumtengenezea mpaka Tshs 3 millioni kwa mwezi (other factors remain constant) kwa kuanza na bodaboda moja tu!

Imagine umenunua bodaboda MPYA aina ya Boxer (pamoja na gharama zingine kama insurance nk) kwa Tshs 1.7 million.

Kwa hapa Dar, kila siku bodaboda inaingiza Tshs. 10,000 (kama umeajiri dereva akupigie kazi). Hivyo kwa wiki unapata Tshs. 70,000 ambayo kwa mwezi ni Tshs 280,000 Net.

Kwa mapato hayo ya mwezi, itakuchukua takribani miezi 6 kurudisha mtaji wako wote. Hivyo kuna option 2, kuuza bodaboda na kuongeza fedha kidogo ili upate zingine mbili, au kuendelea kubaki nayo kwa miezi mingine 6 ili ununue nyingine na ziwe 3.

Hii maana yake ni kwamba, ndani ya mwaka (if other factors are constant) unaweza kuanza na bodaboda moja na kuufunga mwaka na bodaboda 3!

Unaweza kufanya hesabu ili kupata mapato ya mwezi kwa bodaboda 3. Hivyo kama mambo yataendelea vizuri, kuna uwezekano ndani ya miaka 3 kuwa na boda zaidi ya 10 na kufanya pato la mwezi kuwaTshs 2. 8 millioni.

Ushauri mzuri lakini nikuulize swali moja ina maana hizo toyo hafanyiwi marekebisho?
 
Ni ushauri mzuri. Na sio mara zote 'other factors' zitakuwa kama zilivyo. Kuna siku utapaleka chombo kwenye matengenezo, ujue hio 10,000 haitapatikana. Siku dereva akiugua ujue ndo siku ishaenda, siku akiletewa shobo na polisi ama TRA ndio siku ishakata, etc.

pia usiwasahau majembe na tambaza ambao faini zao zinaanzia laki kwenda mbele.. halafu pikpiki hata iwe hiyo boxer dereva akijitahidi kuleta hesabu ndani ya miezi sita mfululizo lazima pikipiki ukapime kwenye chuma chakavu! naongea kama dereva wa bodaboda
 
mmeongea sana kwakifupi nahii ni pasua kichwa hakuna mwenye ahueni labda ufanye mwenyewe
 
Tulishapita huko mkuu na tulipga sana hizo mathematics kabla hatujawakabidhi hawa vijana bodaboda!
Sipendi kukukatisha tamaa ila ukitaka kuwezana nao ingia nae mkataba na umkabidhi hiyo bodaboda kama yake kwa dhamana maalum ndani ya miezi 10 tu daily akuletee Tsh10k. Akifuzu huo mtihani muachie iwe yake. Na ili ufanikishe mambo yako anza na pikipiki3 mpaka5 ili ikitokea mmoja kazingua usiumie sana roho.
All in all ugopa kuletewa kipande utabuluzwa na huyo chalii vibaya sana uichukie bodaboda na biashara yenyewe.

umetisha mkuu ulichikisema ni kweli kabisa na wengi ndo wanafanya hivyo.
 
kila biashara mnaidiscourage,basi mi naanzisha danguro,mtakuja tu kula mizigo
 
kila biashara mnaidiscourage,basi mi naanzisha danguro,mtakuja tu kula mizigo

Teh teh teh. Hata danguro akina Kova huwa wanakuja kuwavurumua na mitutu. Na yenyewe sio ya uhakika sana kihivyo! Labda ujaribu sembe, kwa kuwa ni biashara ya wakubwa!
 
usiombe ukawa na pikipiki mpya umkabidhi kijana imekula kwako mi kuna rafiki yangu mwalimu na pia kuna mama rafiki wa mama yangu walifanya hivyo wale vijana wakasema walitekwa na kuibiwa walipopelekwa mahakaman wote wameshinda kesi wako huru
 
Teh teh teh. Hata danguro akina Kova huwa wanakuja kuwavurumua na mitutu. Na yenyewe sio ya uhakika sana kihivyo! Labda ujaribu sembe, kwa kuwa ni biashara ya wakubwa!
hakuna biashara isiyokua na risk mkuu,na ukiwa muoga kamwe hutofanya biashara yoyote!kikubwa tafuta the best way uwezavyo kuovercome/reduce risk.kumbuka biashara yenye risk zaid ndio yenye faida kubwa...
 
usiombe ukawa na pikipiki mpya umkabidhi kijana imekula kwako mi kuna rafiki yangu mwalimu na pia kuna mama rafiki wa mama yangu walifanya hivyo wale vijana wakasema walitekwa na kuibiwa walipopelekwa mahakaman wote wameshinda kesi wako huru

wizi umezidi , hata mdogo wangu kijana wake amemuibia kwa staili hiyo hiyo........

ni tabu tupu
 
Mimi zilinitesa sana. Nilikuwa nazo mbili. ilibidi niiuze kwa bei ya hasara maana ilikuwa ni full majanga. Kila cku imeharibika hiki mara kile. Labda uwe na bahati nazo...
 
Kwa data hizi umaskini ungetoweka ghafla, ila ongezeko la bodaboda ukumbuke pia abiria watakuwa wachache.
 
Bodaboda? Sitaki kuzisikia kabisa, nilimtoa dereva kijijini kuja mjini ili imsaidie riziki matokeo yake undugu ukaisha ikabaki ni kupelekana polisi kila siku kwani hesabu alikuwa haleti kabisa ikabidi na pikipiki lenyewe niliuze kwa hasara, jamaa ikabidi arudi bush alikotoka tena kwa majuto sana

Sent from my iPhone 4S using JamiiForums app
 
Mkuu steveson manumbu Nina uzoefu wa kutosha juu ya hii biashara asikwambie mtu vijana in pasua kichwa baraa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom