Biashara ya boda boda

Biashara ya boda boda

hivi natakiwa kuzingatia mambo gani kabla ya kumpa pikipiki yangu dereva illi anilitee hesabu kwa wiki.
 
Nyie ndio watu wakitoka kijijini kama kia masanja wanawakimbiza nyie mnaojiita wa mjini.
Hivi biashara gani mnayotaka nyie isiyo na changamoto.
Huyo mke tu balaa,watu wanakula nje itakuwa biashara?

Mjikaze msiwe zaidi ya wanawake,maana siku hizi wanawake wamejikaza kuliko hata midume.

We nani kakuambia kwamba Carry au Bodaboda,au Daladala hazilipi.
Tatizo ni kwamba mkinunua basi kijiji kizima kitajua,na wewe macho yako yote hukohuko.
Nyie mnakimbia wenzenu wananunua na siku inaingiza kama kawaida.Na kila siku ukienda TRA zinasajiliwa upya.Na mwenye nayo anaongeza.
Kama unaiga biashata kwa kuona fulani kafanya ndio utakwama,lakini kama unania ya kweli basi changamoto ni zakawaida sana.

Juzi nimeona kuna mama pale TRA anazo bodaboda 28 na alianza na mbili.Na ukimuambia habari ya changamoto anakuambia za kawaida sana.Na yupo sawa ile mbaya.

Kila siku zinavyozidi kwenda mbele uwezo wa vijana wa kiume kujituma na kujaribu kupambana unapungua kwa kasi sana na idadi ya mashoga inaongezeka.Na uwezo wa wanawake kwenye kipato na kujituma kwa kupambana na changamoto upo kwenye ari ya juu sana na wanauvumilivu wa hali ya juu sana.

We lala tu usubiri kazi laini isiyopasua kichwa,hakuna kazi hiyo labda ufe na ukifa huko unakutana na habari yako nyingine.

Kina dada na kinamama nawapongezeni sana kwa kujituma kimaisha na kujaribu kwa kupambana pia uvumilivu wenu kwenye maisha.
 
Naomben msaada jamani nina mpango wa kuijingiza katika biashara ya bodaboda...lakini naomba kujuzwa yafuatayo
1.Mambo ya kuzingatia na kuwa makini nayo kabla sijajihusisha na hii biashara na pia baada ya kujihusisha na biashara hii
2.Pros and Cons za biashara hii
3.Ninahitaji kuwa na mtaji wa kiasi gani?(Nataka kwanza nianze kwa kununua boda boda used)
4.Pia ningependa kufahamu niki-operate katika maeneo kwanzia kimara mpaka sinza kwa siku naweza ingiza kama sh.ngai kwa siku(Ntamuajiri mtu wa kuendesha)
Asanteni........Extra Comments nje na hizo guidelines 5 pia nitashukuru....Wenye mtani na mzaha please tusiharibiane siku
 
Nakushauri anzisha biashara ya game play station, biashara ya piki piki ni pasua kichwa, mimi ninayo, nilinunua kwa lengo hilo, ila kwa sasa nimeamua kuendesha kwa kwenda nayo kazini, madereva wa kibongo, pasua kichwa, anakupa hesabu siku tatu, ya nne, anakwambia kitu furani kumeharibika, unatoa pesa ya hesabu siku tatu zote. Mara siku nyingine hakuletei hesabu. Ni ushauri tu, na neno langu sio sheria. Wengine watakuja kukueleza ya kwako na uzoefu wao, pia tafuta humu ndani kuna uzi unaozungumzia hiyo biashara ya boda boda.
 
Pikipiki wanasema miezi sita hela inarudi ni uongo, hata mimi nilianzia pkpk 3, lakini nimeuza mbili na moja natembelea nayo iko choka, madrever ni pasua kichwa sana.
 
Mie yangu nimeipark ndani baada ya kuona michosho ya hawa madriver
 
boda boda inalipa kama utapata mtu mwaminifu wa kumkabidhi, na kuzingatia service ya injini.
 
dereva akiwa makini pesa inaonekana maana anakuwa na wateja wake na kwa dar hii foleni zina lipa sana.kikubwa uaminifu wa dereva.

ni memetoa kwa mkataba naona hesabu inakuja sawa kila wiki(elfu kumi kwa siku kwa mwaka), kuna ingine nimeitoa kwa hesabu nayo inaenda vizuri elfu 45 kwa wiki(service juu yake).
 
Naomben msaada jamani nina mpango wa kuijingiza katika biashara ya bodaboda...lakini naomba kujuzwa yafuatayo
1.Mambo ya kuzingatia na kuwa makini nayo kabla sijajihusisha na hii biashara na pia baada ya kujihusisha na biashara hii
2.Pros and Cons za biashara hii
3.Ninahitaji kuwa na mtaji wa kiasi gani?(Nataka kwanza nianze kwa kununua boda boda used)
4.Pia ningependa kufahamu niki-operate katika maeneo kwanzia kimara mpaka sinza kwa siku naweza ingiza kama sh.ngai kwa siku(Ntamuajiri mtu wa kuendesha)
Asanteni........Extra Comments nje na hizo guidelines 5 pia nitashukuru....Wenye mtani na mzaha please tusiharibiane siku


Well, mi nadhani uitoe kwa mkataba kiasi kwamba akivunja mkataba inamgharimu yeye dereva.Ni mkataba wa mwaka akimaliza mwaka mmoja bodaboda inakuwa ni yake.

Hesabu kwa siku elf kumi kwa wiki sabini au sitini itategemea na makubaliano yenu aidha kama siku ya saba itaenda service au laa.Hakuna longolongo wee unachotaka ni hela yako tu siku akizingua inamgharimu yeye inakuwa ni amevunja mkataba, unampa vigezo vyako na kumuuliza kama ataweza kazi au laa tena kwa kuandikishiana na umpate dereva muaminifu ikiwezekana unayemfaham uzuri kabisa.

Bodaboda iwe mpya kabisa sio used coz hii inasaidia dereva kuitunza kwa sababu anajua baada ya mwaka tu inakuwa ni yake kwa hiyo ataitunza na kuzingatia kazi yake na hesabu na chombo kwa ujumla.

Kama makubaliano yenu ni elfu kumi kwa siku, hivyo itakuwa ni elf sabini kwa wiki kwa makubaliano mtakayopeana kwa siku hizo za kazi.Hivyo kwa wiki nne za mwezi ni laki mbili na themanini (280,000) ambapo kwa mwaka utakuwa na 3360000.Kwa hiyo hela ukigawa mara mbili utakuwa umeweza kuongeza boda mbili na ile moja ukamuachia dereva wako ikiwa imekuzalishia boda mbili kwa mwaka, mbili zitazaa nne na hivyo kwa kifupi ni uangalizi na usimamizi mzuri tu wa chombo naamini MUNGU ataleta mafanikio.Na pia kila kitu ni kufanya na kupima kiko vipi ila maji hayapimwi kwa miguu miwili kwa hiyo kama mtaji wako ni wa boda nne anza kwanza na mbili mkuu huku pesa nyingine ikiwa kibindoni kiongozi.

Nakutakia kila la heri.
 
Salaaam!

Nimekaa chini nikaumiza kichwa wadau,nilijiunga vikoba. Sasa nawaza kukopa na kununua boda boda niwape vijana wazungushe.

Naomben ushauri na changamoto za ku run hii busness
 
Binafsi siamini sana biashara ya boda boda kama pesa yako ni ya ku unga unga. Hizo pesa ni nyingi sana kuwekeza kwenye biashara itakayokuwa inakulipa 49000/- kwa wiki. Chukua hiyo hiyo pesa ya boda boda nunua decorder ya DSTV na projector used anza kuonesha mpira. Utapata pesa zaidi with minimal risk na masaa machache ya kufanya kazi. Huo ni mfano tu kuna aina nyingi ya biashara.
 
Bodaboda ili upate faida endesha mwenyewe
 
Changamoto za bodaboda ni nyingi sana. Baadhi ya hizo ni
1. Kutoletewa hela yako kwa wiki kwa wakati muafaka.
2. Baadhi ya vijana hawako makini wanaweza kusababisha ajali na kuharibika vibaya hiyo pikipiki.
3. Wizi, kuibiwa hiyo pikipiki
4. Vijana mnaowakabidhi hawako makini kufanya service ya pikipiki kwa wakati unaofaa
5. Unaweza kupata msongo wa mawazo kwa ajili ya biashara ya bodaboda kuwa makini. n.k

N.B Sikushauri hata kidogo au la endesha wewe mwenyewe labda inaweza kukulipa.
 
Back
Top Bottom