Biashara ya boda boda

Mie pia nafanya hiyo biashara lakini hesabu zako naona kama hazijakaa vizuri.
Boxer ya kisasa BM 150 mpya in Full pamoja na Comprehensive insurance si chini ya 2.3m kwa sasa kwa wakala mkuu.
Sasa kufika bodaboda 10 si chini ya milioni 23.
Sasa kwa akili ya kawaida na kwa biashara hii ilivyo kwa sasa sidhani na sishauri mtu afike mtaji huo wote auweke kwenye biashara ya Bodaboda.
Ni mtaji mkubwa sana unaweza kuugawa na ukaingiza hesabu nzuri sana kwa biashara pacha.
Tabia ya kuwekeza biashara moja ni hatari sana tena sana,watu kipindi cha nyuma miaka ya 2008 kushuka chini watu na wafanyakazi wa serikali walikimbilia sana kuchukua mkopo wanunue Taxi,wengine hawakusoma alama za nyakati,sasa hivi hakuna hata mmoja anaetaka kusikia habari hiyo.
Wakahamia kwenye Hiace dungu,wakati sinaruhusiwa kuingia mjini,baada ya muda nako wakalia,kuna watu walikuwa nazo hadi 5,leo ni majanga hawaju wafanye nini nje ya mji ambapo pia ziilikuwepo nyingine zenye uzoefu na route za huko.
Leo hii Coaster nazo zimo safarini.
Kwahiyo Jaribu kuwekeza kwenye Biashara kwa kiasi hasa hizi.Usizidi Bodaboda 5.La sivyo utalia kaka.
 
Other factors being constant. That is the catch, kwani they are never constant. Kijana hatoleta sh 70,000 kwa wiki, then atapata ajali then atafungwa au kuibiwa. Doesnt work that way kwenye biashara
 
Other factors being constant. That is the catch, kwani they are never constant. Kijana hatoleta sh 70,000 kwa wiki, then atapata ajali then atafungwa au kuibiwa. Doesnt work that way kwenye biashara

Ni ushauri mzuri. Na sio mara zote 'other factors' zitakuwa kama zilivyo. Kuna siku utapaleka chombo kwenye matengenezo, ujue hio 10,000 haitapatikana. Siku dereva akiugua ujue ndo siku ishaenda, siku akiletewa shobo na polisi ama TRA ndio siku ishakata, etc.
 
Ushauri mzuri lakini nikuulize swali moja ina maana hizo toyo hafanyiwi marekebisho?
 
pia usiwasahau majembe na tambaza ambao faini zao zinaanzia laki kwenda mbele.. halafu pikpiki hata iwe hiyo boxer dereva akijitahidi kuleta hesabu ndani ya miezi sita mfululizo lazima pikipiki ukapime kwenye chuma chakavu! naongea kama dereva wa bodaboda
 
mmeongea sana kwakifupi nahii ni pasua kichwa hakuna mwenye ahueni labda ufanye mwenyewe
 
umetisha mkuu ulichikisema ni kweli kabisa na wengi ndo wanafanya hivyo.
 
kila biashara mnaidiscourage,basi mi naanzisha danguro,mtakuja tu kula mizigo
 
kila biashara mnaidiscourage,basi mi naanzisha danguro,mtakuja tu kula mizigo

Teh teh teh. Hata danguro akina Kova huwa wanakuja kuwavurumua na mitutu. Na yenyewe sio ya uhakika sana kihivyo! Labda ujaribu sembe, kwa kuwa ni biashara ya wakubwa!
 
usiombe ukawa na pikipiki mpya umkabidhi kijana imekula kwako mi kuna rafiki yangu mwalimu na pia kuna mama rafiki wa mama yangu walifanya hivyo wale vijana wakasema walitekwa na kuibiwa walipopelekwa mahakaman wote wameshinda kesi wako huru
 
Teh teh teh. Hata danguro akina Kova huwa wanakuja kuwavurumua na mitutu. Na yenyewe sio ya uhakika sana kihivyo! Labda ujaribu sembe, kwa kuwa ni biashara ya wakubwa!
hakuna biashara isiyokua na risk mkuu,na ukiwa muoga kamwe hutofanya biashara yoyote!kikubwa tafuta the best way uwezavyo kuovercome/reduce risk.kumbuka biashara yenye risk zaid ndio yenye faida kubwa...
 
usiombe ukawa na pikipiki mpya umkabidhi kijana imekula kwako mi kuna rafiki yangu mwalimu na pia kuna mama rafiki wa mama yangu walifanya hivyo wale vijana wakasema walitekwa na kuibiwa walipopelekwa mahakaman wote wameshinda kesi wako huru

wizi umezidi , hata mdogo wangu kijana wake amemuibia kwa staili hiyo hiyo........

ni tabu tupu
 
Mimi zilinitesa sana. Nilikuwa nazo mbili. ilibidi niiuze kwa bei ya hasara maana ilikuwa ni full majanga. Kila cku imeharibika hiki mara kile. Labda uwe na bahati nazo...
 
Kwa data hizi umaskini ungetoweka ghafla, ila ongezeko la bodaboda ukumbuke pia abiria watakuwa wachache.
 
Bodaboda? Sitaki kuzisikia kabisa, nilimtoa dereva kijijini kuja mjini ili imsaidie riziki matokeo yake undugu ukaisha ikabaki ni kupelekana polisi kila siku kwani hesabu alikuwa haleti kabisa ikabidi na pikipiki lenyewe niliuze kwa hasara, jamaa ikabidi arudi bush alikotoka tena kwa majuto sana

Sent from my iPhone 4S using JamiiForums app
 
Mkuu steveson manumbu Nina uzoefu wa kutosha juu ya hii biashara asikwambie mtu vijana in pasua kichwa baraa!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…