Nakushauri anzisha biashara ya game play station, biashara ya piki piki ni pasua kichwa, mimi ninayo, nilinunua kwa lengo hilo, ila kwa sasa nimeamua kuendesha kwa kwenda nayo kazini, madereva wa kibongo, pasua kichwa, anakupa hesabu siku tatu, ya nne, anakwambia kitu furani kumeharibika, unatoa pesa ya hesabu siku tatu zote. Mara siku nyingine hakuletei hesabu. Ni ushauri tu, na neno langu sio sheria. Wengine watakuja kukueleza ya kwako na uzoefu wao, pia tafuta humu ndani kuna uzi unaozungumzia hiyo biashara ya boda boda.