Biashara ya Bodaboda

Risk ni nyingi sana mkuu.
Ukidhibiti risk moja nyingine lazima itakunasa.
Risk za biashara ya bodaboda ni kama zifuatazo
1.Madereva kuwa wasumbufu kukwepa kulipa au kukulipa marejesho yako kwa malimbikizo.
2.Ajali
3.Kuibiwa kirahisi
4.kukamatwa hovyo hovyo na askari kwa makosa yasiyotabirika(Kwa mfano bodaboda anaweza kumpa rafiki yake afanyie deiwaka,kisha rafiki yake akaenda kufanyia uhalifu)hapa ikikamatwa kuigomboa unaweza kuambiwa utoe faini ya milioni 2 ambayo ni sawa na kununua pikipiki nyingine tu.
5.Dereva kuendesha maeneo yasiyoruhusiwa akikamatwa atapigwa faini kubwa ambayo akishindwa kulipa itasababisha biashara isimame.
Sasa katika uhalisia ni ngumu sana kuzikwepa hizi risks zote,haijalishi uko smart kiasi gani maana hizi risks ziko nje ya uwezo wako
 
Mbona wako wengi tu Dar es salaam,ukiwa na uwezo wa kununua pikipiki 10 unaunganishwa kisha unaandaa leseni na tin number kisha unafungua kibranch chako.
 
Betting,na hata kama umerudisha na faida juu usigande kwenye hiyo biashara badilisha hiyo biashara haraka iwezekanavyo,ukijifanya una top up kukuza mradi wa bodaboda ipo siku itakubadilikia hutoamini macho yake.
Tume ameamua kuwekeza kwenye bajaji Sasa hivi
 
Nyie ndo wale motivation speaker kaz yenu kubwabwaja tu Lima matikiti heka sjui nn ingieni field kwa vitendo unakuta ata boda boda hujui ata kuziba pancha
Hao wanataka kutumia formula za kuclick kwenye real life kitu ambacho sio applicable.
Wana msemo wao wanakwambia"Kuwa tajiri sio kupata hela nyingi bali kuwa tajiri ni kuhifadhi kile kidogo/kiduchu unachokipata" Sasa ukiwauliza wewe tangu uanze kuhifadhi kidogo ukipatacho hadi sasa una utajiri wa kiasi gani?hana majibu
 
Hata mimi nimeshangaa yaani mtaji wa kuanzisha Hardware la vifaa vya ujenzi ukauchezee kununua bodaboda
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wanachezea mitaji adse
 
Sawa bro, Kila mtu ana formula yake. Mimi katika business nilizofanikiwa kuzifanya na nikaona inafaa kwangu kwasasa ni Pikipiki. Mawazo mengine yatakuja mbeleni
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wanachezea mitaji adse
Ni mawazo ukiwa na Hela utaona wengine wanachezea mtaji na usipokuwa na mtaji utaona wengine hawafanyi unachokiwaza ww.

Sijaona umuhimu Wa kufungua duka la hardware, ningewekeza huko ila ni chaguo la Kila mtu kuwekeza sehemu anayoona ni sahihi kwake.
 
na hiyo ndo hali halisi ya hizo biashara
 
Changamoto kubwa ktk hii biashara ni tamaa,, mfano maboss wengi wanageuka majambazi na kuwauwa au kuwanyang'anya vijana wao wa kazi pikipki pale mkataba unapokalibia kuisha kwa kuwateka, pia vijana wenyewe nao baadhi sio waungwana pindi wakikalibia kumaliza mkataba huwa wanafanya visa sana mf kuibiwa pikipiki kwa kufeki nk
 
Umesema ukweli
 
Sasa kweli yaani pikipiki 15 ni sawa na milioni 34.5 unaona faida ya 49,500 kwa siku ni sawa kweli?!!Hapanaaa hiyo kwa hesabu za kibiashara ni hakuna kitu hapo!!
Kuna kitu hapa watu wanashindwa kuelewa Sina mtaji Wa 34.5 Millions, nimesema nilianza na mtaji Wa 9 Millions Kwa kuanza na Pikipiki 4 tu mpka kufika sasa zipo zaidi ya Pikipiki 15.

Concept hapa ni kwamba Kwa marejesho haya haya ya Pikipiki nilizonunua mwanzoni ndio nilitumia kununua Pikipiki nyingine zilizofuata huku nikiongeza 30% ya sehemu ya Mshahara wangu Kila mwezi.

Mtaji wangu ni 9 Millions + 30% ya Mshahara wangu Kila mwezi mpka kufika hatua hii Kwa muda wa miezi 13 mpka Leo hii.

Kukosoa sio jawabu nipeni ushauri Wa Biashara ambayo inatakiwa kuingiza Faida ya zaidi ya 50,000/= Kwa Siku Kwa mtaji Wa 9 - 10 Million's.

Kukosoa Kwa sababu ulisikia mtu mwingine akishindwa hiyo biashara sio jambo jema, Nina zaidi ya mwaka mmoja sasa na sijaona shida yyote katika hii Business.

Kushindwa kwako sio kwamba na mwingine asifanye hiyo Biashara, TUKOSOE Kwa kutoa USHUHUDA Wa Biashara unayofanya wewe na KIPATO/FAIDA unayopata Kwa Siku itapendeza.

🟢Mfano Mimi Kwa Siku sikosi REJESHO La 150,000/=. Katika hii Hela 50,000/= ni kama Faida yangu Kwa Siku na 100,000/= ni Hesabu ya hela inayorudi kutokana na uwekezaji wangu ndani ya siku Moja Kwa mwezi mmoja (30 days) nitarudisha 3M ya mtaji wangu.

🟡TUPEANE IDEA ZA BIASHARA ZA KUFANYA, TOA USHUHUDA KAZI/BIASHARA UNAYOFANYA NA FAIDA UNAYOPATA ILI TUPATE MOYO WA KUFANYA BIASHARA NYINGINE PIA, ILI NlWEKEZE KATIKA BUSINESS NYINGINE.
 
Lengo langu lilikuwa sio kukukatisha tamaa,kwaninkila mtu anapokuwa na pesa ni juu lake kuamua anaiwekeza wapi,ila kuna sehemu unawekeza lakini mtu mwingine akaona hapana kwa kiwango hicho ungewekeza sehemu fulani kwa mtaji huo,ungeweza kupata faida hata mala nne yake.mfano mtu anachukua 50,000,000 anaiweka kwenye fixed deposit ili kwa mwaka apate faida ya 10% humo kuna withholding tax unaona kabisa sio uwekezaji mzuri kama angepata ushauri mzuri,.Ok hata kama ulianza na 9M,kama sasa zimefika 15 jua kabisa hicho kipato unachokipata hakilingani na THAMANI YA MTAJI uliyoweka,huo ndio ukweli wa ki biashara.Mfano
Kuna mtu ana mataji wa 110,000 ana nunua nyama kilo 20 , akiuza kwa siku anapata faida ya 50,000!!!Siwezi kusema specific fanya biashara hii,kwani unapoamua kufanya biashara fulani,lazima uifanyie uchunguzi.Wengi wanaokimbilia biashara ya bodaboda huwa ni kutotaka usumbufu wa hapa na pale tu,kulinganisha na biashara nyingine,ndio maana yeye kupata 7000 kwa siku ana rizika tu.Japo na kwenyewe kuna changamoto zake hasa ukimpata kijana asiyejitambua.
 
hio hela ni bora ukapata bajaji used na kuanza biashara
 
Habari Mkuu,

Hiyo 50,000 baada ya kuuza kg 20 sio faida ni mapato kwa siku. Bado hujatoa gharama za uendeshaji hujazihesabu kama gharama za usafiri hadi nyama inafika buchani, gharama za frame, gharama za TRA na gharama nyinginezo. Hapo faida yake inaweza kuwa 30% ya 50,000 ambayo ni sawa na 15,000/=. Kwenye biashara kuna mambo mengi sana ambayo watu huwa hawaangalii.
 
Heee!!unajua nini maana ya mapato?kama hiyo 50,000 ni mapato na hiyo 160,000 itakuwa nini??hiyo 50000 ni faida ghafi(Gross profit) na sio mapato!!hapo gharama ya usafiri tayari!!Ndio maana siku andika NET PROFIT!!!!BASI fanya 20,000 ndio ya matumizi hayo!!NET PROFIT IWE 30000 TU.
 
Uko sahihi ni gross profit na sio mapato kama nilivyosema mwanzo:-

Nje ya gharama ya usafiri ila bado kuna operation costs ambazo hujazihesabu:-

1. Gharama za TRA
2. Gharama za pango
3. Mengineyo, kama vile chakula ukiwa ofisini, gharama za kulipa msaidizi (kama unaye), na gharama za machine (kama unatumia machine).

Ndio maana nikakadiria kutoka kwenye 50,000, let's say Net net profit ni 30% (Though inaweza kuzid)
 
Ok!hakuna mashine,pango 50,000 kwa mwezi,TRA kwa mwaka 150,000,msaidizi kwa siku 5000.na bodi ya nyama tu.huyu kwa siku analaza si chini ya 30,000.Kwa mtaji huo wa 110,000.Mimi bado nasemq biashara ya pikipiki/bajaji kwa returns zake hazina afya ki biashara.Mfano bajaji mtaji wa milioni 9 uniletee faida ya 7000 kwa siku kweli??na baada ya miaka 2 inakuwa sio mali yangu tena!!!
 
Sasa kweli yaani pikipiki 15 ni sawa na milioni 34.5 unaona faida ya 49,500 kwa siku ni sawa kweli?!!Hapanaaa hiyo kwa hesabu za kibiashara ni hakuna kitu hapo!!
Nyie ndio wale wasomi mlotoka chuo kaz hamtak mnabet tu mkitarajia muwe mamilionea sasa wewe faida ya 49500 unaona ndogo kwa siku tena kumbuka huyu ni kama kaweka ela yake kwenye mzunguko inaongezeka na hapo anasema Ana kazi anayofanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…