mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Risk ni nyingi sana mkuu.Japo napendelea bajaji, ila boda zinalipa pia.
[emoji117]Vipi ushawai fanya, au unasikia kwa watu[emoji848]
[emoji117]Kama ndio, ni changamoto zipi zilikukumba.
[emoji117]Kufeli kwako, unahisi na wengine itakuwa hivyo??
[emoji117]Vipi Kama waki/tukiboresha mbinu na mikakati ili kuendana na changamoto zilizopo[emoji848][emoji848]
[emoji117] Never say it's impossible coz the word it's self says I'm possible
Ukidhibiti risk moja nyingine lazima itakunasa.
Risk za biashara ya bodaboda ni kama zifuatazo
1.Madereva kuwa wasumbufu kukwepa kulipa au kukulipa marejesho yako kwa malimbikizo.
2.Ajali
3.Kuibiwa kirahisi
4.kukamatwa hovyo hovyo na askari kwa makosa yasiyotabirika(Kwa mfano bodaboda anaweza kumpa rafiki yake afanyie deiwaka,kisha rafiki yake akaenda kufanyia uhalifu)hapa ikikamatwa kuigomboa unaweza kuambiwa utoe faini ya milioni 2 ambayo ni sawa na kununua pikipiki nyingine tu.
5.Dereva kuendesha maeneo yasiyoruhusiwa akikamatwa atapigwa faini kubwa ambayo akishindwa kulipa itasababisha biashara isimame.
Sasa katika uhalisia ni ngumu sana kuzikwepa hizi risks zote,haijalishi uko smart kiasi gani maana hizi risks ziko nje ya uwezo wako