Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Pole sana. Wa kumlamu hakuna ila ni wewe mwenyewe ujilaumu. Hivi kweli biashara ndogo kama ya chips inahitaji ushauri wa watu wengi? Na hata ukipokea ushauri, kwani ni lazima uukubali? Mimi siku zote kwenye bishara huw nasema hivi: ukiona unataka kuanziasha biashara fulani, halafu unaulizia tena watu uanze namna gani basi hiyo biashara haikufai na ukiazna utanguka. Biashara unatakiwa ufanye utafiti mwenyewe na kama ni ushauri unaulizia watu wazoefu kwenye ile biashara tu tena wasijue nia yako ni nini?
 
Ulichosema kuhusu watu wa JF upo sahihi

Nikirudi kwenye wazo lako nadhani "umejifelisha mwenyewe"

si yeyote yule ila wewe binafsi maana ulikua mguu mmoja ndani mmoja nnje

Next time ukishika tena 1M usiwe na wazo 1 waza mawazo tofauti hata ma 5

Kisha usiku yaandike kwenye notebook anza ku tick moja baada ya jingine

Hadi upate 1 kisha usiangalie nyuma Nenda kafanye,Ni mara 100 ungepoteza hyo 1M

kwenye biashara ungepata experience na kitu flan ila wewe umetumbua yote ila sio mbaya

Kuna somo umelipata naamini ukishika 1M tena kuna ujinga/makosa hautoufanya.
 
Next time ukishika tena 1M usiwe na wazo 1 waza mawazo tofauti hata ma 5
Kisha usiku yaandike kwenye notebook anza ku tick moja baada ya jingine
Hadi upate 1
Unakuwa unatikije mkuu....hapa sijakuelewa...
 
JFukiitumia vizuri huwezi feli kirahisi. Humu watu hutoa maoni yao kulingana na mahitaji unayohitaji

Kiukweli chipsi classic huwez ipata katika sehemu ya uwekezaji wa milion 1! wewe labda ulifeli kuwasilisha wazo

1 Tuwekee huo uzi hapa tuusome na maoni ya wadau yalikuwaje
2 Wewe ungeomba msaada tu, unamilion moja mchanganuo wa biashara ya chipsi ungepewa maelekezo ya banda na vifaa vyake muhimu kulingana na pesa yako
 
Unakuwa unatikije mkuu....hapa sijakuelewa...
ndugu yetu tufanye angekua na mawazo kama ma 5

kaja JF kakutana na kila mtu anaponda wazo lake kwa point

yeye kwakua kashaamua kusikiliza wana JF usiku angetia X wazo la chips

siku inayofata anakuja na Thread ingine ya wazo no.2 angesikiliza tena maoni

Angeendelea na utaratibu huo mwisho katka yale mawazo ma 5 angechomoka na 1

Ambalo limepata kura Nyingi huku JF kulingana na alivyokua akihitaji yeye.


Ila kuwa na wazo 1 ni sawa na Mtu kaamua kufanya biiashara kakodi frem ya 1M kwa mwezi

badala aitumie frem kuweka biashara tofauti za kuingiza pesa,eti kagandana na biashara ya Nguo tu

kisa ndio biashara aliyokodia frem,Huyu mtu nguo zisiponunuliwa lazima alie kilio cha mbwa wakati

angeweza ongeza biashara nyingiine auze hapo hapo kwenye duka lake la nguo mambo yakaenda


Nguo zikigoma vitu vingine vinaenda... Kodi inapatikana.
 
somo kubwa sana nimejifunza
mapema Januari ninaweza pata kiasi cha pesa hakika sitarudia makosa
 
Huenda kweli nilikosea kulingana na maoni yako!

Huo uzi upo humu lakini nimeshindwa kuuquote, unaweza kunisaidia kuweka kupitia nyuzi nilizopost
 
 
asante mkuu
huu utaalamu naomba kuupata
 
Hv alietengeneza ndege ushauri aliutoa wapi? Alietengeneza artificial sitelite ushauri aliutoa wapi? Alieunda Jf, ushauri aliutoa wapi? Iamini akili yako,
 
Wewe unakuja Kuomba ushauri wa kuuza chips kwa Sisi ma Bilionairs wa Jf unategemea majibu gani? Billionaire kama mimi unakuja na kamilioni kako kuomba ushauri si nitaona unanipotezea muda wangu wakati mimi umeme wa nyumbani kwa wiki tu hako kamilioni kameisha.

Any way pole ndugu lakini hiyo hapo ndio mentality ya asilimia kubwa ya watu wa kwenye mitandao. Siku nyingine ukiamua kufanya biashara usipende kuomba ushauri. Take risk man

Kwenye biashara kuna changamoto sana utakuta kuna mtu aliwahi kuuza chips Kule kimara kwa wachaga ambao kwao kula home ni lazima kwahiyo kuuza chips kulechangamoto zake ni tofauti na kule sinza vi sister duu vinapenda chips na kupika home ni mwiko

Take risk buddy
 
Pole [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…