wakuu
Ni miezi sita sasa imepita tangu nilipojitokeza hapa jamvini nikiwa na kiasi cha shilingi milion 1 pesa nikiwaomba mnipatie muongozi wa kufungua banda la chipsi zenye ubora wa kiwango cha juu na kukamata soko dhidi ya wapinzani wanouza chipsi locally
Aiseeeee, nilijuta na mpaka sasa najutia uamuzi wangu wa kulileta lile bandiko langu humu
Kiukwrli sikuweza kuendelea na lile wazo kwasababu wananchi wengi humu walinipinga na kunikatisha tamaa sana kwamba wazo halitekelezeki, hii ilinikatisha tamaa
Ile pesa niliamua kutulia nayo, hii ndio ilikua mistake kubwa
pesa haitulii kabisa, nilijaribu kuituliza lakini wapi mwishowe yote ikapukutika kwa sababu tu ya ushauri butu wa wajf walionikatisha tamaa
mbaya zaidi kilichosababisha nilete mrejesho humu, leo nimekatiza ile mitaa niliyokuwa naiplan kufungua ile biashara nimekuta mtu mwingine amefungua biashara ileile ya chipsi tena kama kahamisha mawazo yangu na kuyatekeleza
nimejaribu kumuuliza ni kiasi gani kainvest kasema kaweka milion 1 tu, hii imeniuma sana
Nimeamua kula chips kuku tena tamu kweli na kuishia kufyonya tu huku nikikumbuka michango ya wadau wa humu
Humu kuna watu hawapendi wengine tufanikiwe!
Humu kuna watu wanajifanya ni wataalamu wa kila kitu
Humu kuna watu kila uzi lazima wakoment
Tafadhalini sana, Jf tutoe mawazo bora na kujenga na si kukatishana tamaa kiboya tu na kuziacha pesa zipigwe na wengine