Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Thank you my dearest! Ushauri wako ni wa maana sana! Na nitafanya hvyo!
 
Sure mkuu! Hili ni wazo zuri sana, asante mkuu!
Na kama.ni mfanyakazi achukue likizo hata ya wiki.

Asimamie mauzo na kusoma biashara. Inakwendahe. Nini kinatoka sana nini aboreshe nk

Then mpe anweza mpa limit au amweleze bila kiasi kadhaa hatomwelewa
 
Wazo lako zuri kuwa nisiconcentrate kuthbiti wizi kwani ni ngumu sana kuthbiti, zaidi niwe profit oriented!
Usiogope kuibiwa kikubwa angalia usipate hasara, kama anachapa kazi vizuri na faida inakutosha achanana fikra hizo watakukimbiwa sana
 
Kama kawaida ya jukwaa letu kushauriana na kuelimishana, hatimaye nimefanikiwa kuanzisha biashara ya chips ila tatizo nakuwa busy mpaka saa 12 jioni, je nifanyeje ili niweze kuweka strong internal control ili kuthibiti kuibiwa? Asanteni!

Kuwa mdadisi jaribu kuuliza kwa wauza chips wengine kuwa NDOO moja ya chips inatoa sahani ngapi iwe chips yai au kavu, vilevile kuna kuhesabu trei za Mayai utajua chips yai zimeenda ngapi! Upande wa Kuku nafkiri inajulikana wazi ukinunua Kuku mmoja na kukata vipande vipande kuuza kutegemea na sehem ulipo.


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Nunua vifaa vyote viazi,tomato,kuku, mayai,mafuta, mkaa nk, halafu mpange kila siku awe anakupa sh ngapi inategemea na eneo alipo kama ni elfu 10/15/20 we utakuwa unapewa hela yako ,na vitu vikiwa vinaisha anatakiwa awe ananunua yeye wewe unalipa kodi ya pango tu. lakini ukisema umsimamie we haupo atakuwa ananunua viazi vyake anauza we ukija unakuta viazi vyako anakwambia biashara mbaya.
 

wengi walioshauri hawakufikiria hili....siku hizi huibiwi hela,wafanyakazi wanaleta vyao wanauza eneo lako ukija unaambiwa biashara ngumu na bidhaa zako unazikuta!!! huu huwakuta sana wenye baa.
 
Kuna braza mmoja nilimweka kwenye hicho kitengo, sasa kwenye mishe zangu nikuwa narudi jioni. Ninapofika naona yupo busy balaa ila ananiambia leo mdogo wangu hali mbaya yaani wateja ndio wameanza kuja sasa hivi wewe unapofika.
Kila siku ikawa hivyo hivyo. Lakini cha ajabu utakuta muda wa usiku amekaa na warembo wanapiga banana wakati anasema hali mbaya.
Sasa kuna siku nilimwotea, nikaondoka asubuhi, halafu ghafla nikarudi. Duh! Nikaona jamaa amenunua maviazi mara 2 na nusu ya kawaida wakati hela niliyomwachia ni chache. Hiyo siku nilikomaa naye nikamlamba na faida ya viazi alivyonunua kwa hela yake na akshindwa kunibana.
Kuanzia hiyo siku tukapigiama hesabu alete kumi na tano per day na ndio ikawa suluhisho la kuibiwa.
 
Biashara mpya mkuu kaa pale as mfanyakazi uangalie upepo unaendeje inaingiza sh ngapi per day

Usifanye kosa ya kumkabithi mtu biashara mpya ambayo hujui unaingiza sh ngapi
Mtakuja kugombana bure
 
Pamoja na kucheka sana baada ya kusoma majibu mbalimbali humu.... ngoja nikwambie kitu.

Hii biashara naijua sana. Kama huwezi kuisimamia mwenyewe moja kwa moja huwezi kuzuia kuibiwa labda Umpate msimamizi mwaminifu sana. Hata ukihesabu viazi, wanachoshafanya wauza chips haibi chips zako; yeye atanunua viazi vingine pembeni hivyo atakuwa anauza vya kwake; vyako utavikuta vile vile havijaibiwa na atadai biashara sio nzuri.... yaani siku akimaliza vyake ndio na wewe siku hiyo utapata kidogo. umeelewa @ Makaula? Nafikiri biashara nyingi kama huzisimamii mwenyewe... kuibiwa ruksa
 
Kiukweli wewe mpangie tu kama UNAHITAJI kiasi gani kwa siku lkn binadamu ukimsimamia mmh hautaweza kwani ipo SIKU utasema umemwamini kumbe ndio umefungua milango TA wizii
 
Kama kawaida ya jukwaa letu kushauriana na kuelimishana, hatimaye nimefanikiwa kuanzisha biashara ya chips ila tatizo nakuwa busy mpaka saa 12 jioni, je nifanyeje ili niweze kuweka strong internal control ili kuthibiti kuibiwa? Asanteni!
skia kilo moja ya viaz sawa na saa 4 za chips so km gunia kilo mia piga mahesabu mi nshauza ila sa hv nimeacha zina faida sana
 
Sahani moja ya chipsi ni viazi viwili vya mbeya

Ha Mkuu na biashara ya chips unaijua? Hongera sana. Ila ni ngumu sana kukadhibiti maana kanaweza kupunguza namna ya kukata vipande! Ingawa ni ushauri mzuri!!
 

Hivi Stata mzuka nalo jina
 
Kama mtaji wa kuansisha hii biashara wewe mwenyewe umeiba basi tegemea kuibiwa pia.Akikosa kukuibia mfanyakazi basi nyumbani hata mkeo atakuibia
 
Reactions: THT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…