Si dhani kama utanielewa, Biashara ndogo ni sawa na mtoto mdogo, wakati ambapo biashara inahitaji care ya hali ya juu kabisa ni wakati ikiwa ndogo, inahitaji initiator awepo full time, na ndo maana ukisoma story za wote walio fanikiwa walianza wao kama wao, mwanzo ni mugumu sana, Biashara inapo kuwa kubwa hapo ndo sasa unaweza kuwa na watu wengi wa kukusaidia, Sisemi mwanzo usiwe na watu kinacho takiwa ni wewe uwepo full time, Unless kama biashara hiyo huna malengo nayo.
Biashara nyingi sana hufa kwa sababu ya kuendeshwa kwa simu, uko ofisi unauliza leo wamekuja wateja wangapi? e kuku wamepewa dawa? hapo ndo unamkumbusha awapatie dawa, Ni vigumu sana kufanikiwa kwa staili hii, that is why ni kaseama kama kweli umeamua kuingia kwenye biashara na unatageti mbali ni lazima uchague moja, najua ni ngumu sana ila ukweli ndo huo