Biashara ya choo baada ya kustaafu utumishi wa umma

Biashara ya choo baada ya kustaafu utumishi wa umma

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Wadau salama, CCM hoyee.

Huwa nina tabia ya kupiga story na wazee watu wazima kidogo.

Sasa kuna huyu amebakiza kama miezi sita ya kustaafu kazi ya utumishi wa umma.

Anaitwa mzee Shayo, anasema yeye anataka hela yake akishastaafu ajenge at least matundu 30 ya vyoo hapa mjini sehemu tofauti tofauti.

Ila watoto wake wakubwa tu wamemshauri anunue Costa mayai 2 azipige special Hire at least kwa siku awe ana uhakika wa laki 4 mpaka 6.

Je, wana uchumi mawazo yenu ni yapi ? Tujengane maana naamini kwamba hata hapa JF wapo pia wastaafu au wanaokaribia kustaafu. Watapata mawazo pia.

Kwangu mimi, Ningemshauri biashara ya choo, maana nina mshikaji wangu yuko buguruni yeye ana matundu manne, kwa macho yangu jamaa anafunga elfu 50+ kwa siku.

Nawasilisha.

.
 
Back
Top Bottom