Biashara ya choo baada ya kustaafu utumishi wa umma

Biashara ya choo baada ya kustaafu utumishi wa umma

Coaster mayai 2 kwa siku upate 400k - 600k kirahisi tu !
Watu wasingepeleka magari yao kufanya shughuli za daladala.
Halafu kwa kikokotoo hichi kupata pesa ya coaster 2 na kubakiwa na pesa ya dharura si rahisi labda kama anastaafu kama afisa mkuu mwandamizi
 
Wadau salama, CCM hoyee.

Huwa nina tabia ya kupiga story na wazee watu wazima kidogo.

Sasa kuna huyu amebakiza kama miezi sita ya kustaafu kazi ya utumishi wa umma.

Anaitwa mzee Shayo, anasema yeye anataka hela yake akishastaafu ajenge at least matundu 30 ya vyoo hapa mjini sehemu tofauti tofauti.

Ila watoto wake wakubwa tu wamemshauri anunue Costa mayai 2 azipige special Hire at least kwa siku awe ana uhakika wa laki 4 mpaka 6.

Je, wana uchumi mawazo yenu ni yapi ? Tujengane maana naamini kwamba hata hapa JF wapo pia wastaafu au wanaokaribia kustaafu. Watapata mawazo pia.

Kwangu mimi, Ningemshauri biashara ya choo, maana nina mshikaji wangu yuko buguruni yeye ana matundu manne, kwa macho yangu jamaa anafunga elfu 50+ kwa siku.

Nawasilisha.

.
Rafiki Yako mwongo huwezi pata 50000 kwa siku otherwise huo mkoa una wagonjwa wa kipindu pindu.


Wapi unaweza kupata watu 41 wakupe kila mmoja 300 kwa kila choo kimoja kwa vinne
 
Biashara ya magari kwa mstaafu hapana sishauri,ajikite kwenye biashara ya huduma ya choo.Kikubwa asisahau kuandika bango kubwa kwenye choo "Mzee Shayo Shit Bank Plc" na kauli mbiu(slogan)kwa chini "MAVI yenu ajira yangu"
 
Ni kweli mkuu, biashara za kustaafia ni mtihani sana. Zinawaongezeaga depression wazee wa watu
Mtu hana experience ya biashara kasimuliwa huko biashara za makaratasi akaona aje afanyie experience kwwnye pesa ya pension ...watamuwahisha mzee wa watu akhera kwa pressure na mawazo .Biashara zinaupside down kibao na huwa hazisemwi na mchambuzi wa biashara yanaongelewaga mazuri tu ..kwa mtu ambae hakuwahi kufany biashara ujana wake wote aje ajaribie uzeeni anaweza akashindwa kuhimili japo wapo wanaotoboa
 
Back
Top Bottom