Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

anonimuz

Senior Member
Joined
Nov 5, 2007
Posts
102
Reaction score
71

Mambo vipi wakuu,

Nimeamua kujikita kwenye biashara ya daladala na bado nipo kwenye hatua ya utafiti. Nimepitia threads nyiiingi sana humu na watu wengi wanaoipiga vita hii biashara wanakuwa na hoja za "Biashara pasua kichwa", "Madereva watakunyonga" n.k bila kuelezea kiundani changamoto wali/nazopata katika biashara hii. Madhumuni ya thread hii ni kutaka kupata ushauri

1) Kutoka kwa watu ambao walifanya hii biashara ikawashinda. Watueleze matatizo waliyokumbana nayo.

2) Kutoka kwa watu ambao bado wanafanya hii biashara na inaenda vizuri. Watueleze namna wanavyoiendesha na kukabiliana na matatizo ya hapa na pale. Tukipata watu wakatupa mfafanuo wa gharama na mapato itakuwa vizuri zaidi.

3) Kutoka kwa watu wenye uzoefu thabiti wa magari kuhusu aina ya magari (Toyota Hiace, Toyota Coaster, Isuzu, Nissan etc) yanayofaa kwa biashara hii. Mapungufu na faida ya kila aina.

4) Juu ya hili: Nimeamua kuanza kwa kununua Nissan Civilian mbili ila baadhi ya ndugu, jamaa, na marafiki wanatoa ushauri wa kwamba uimara wa gari hizi ni wa wasiwasi, "spare" mgogoro etc. Mwenye ufahamu juu ya hili tafadhali. Hasa wale ambao wanamiliki magari haya.

5) Juu ya hili: Nimekua nikifanya malinganisho ya gharama na mapato ya uendeshaji kwa Dar na mikoani ila bado sijafikia hatua ya kuamua ipi inalipa zaidi. Wale wenye biashara hii Dar NA mikoani, tunaomba muongozo wenu hapa

Mwisho ningependa wamiliki na wadau wengine watueleze wanauonaje muelekeo wa biashara hii kwa Dar, sasa ambapo DART ipo njiani.

Nafahamu kuwa ni rahisi mno mtu kuchangia "thread" kiushabiki zaidi kwa kuandika "one liner posts" kama "biashara pasua kichwa" na kadhalika ila ningependa tuweke ushabiki pembeni na tujitahidi kuchangia uzi huu kutokana na uzoefu tulionao kwenye biashara hii na kufafanua hoja zetu.


WADAU WENGINE WANAHITAJI KUJUA NINI KUHUSU BIASHARA HII?


MICHANGO TOKA KWA WADAU
 
Karibu Alnadaby kwenye shughuli hii ya kusafirisha abiria katika miji mikubwa.Kitu cha kwanza kabisa katika bajeti yako weka 30% ya mapato yako kwa ajili ya mafisadi wa barabarani, hakuna jinsi kubali kugawana mapato na hao jama kwani ndiyo wadau.

Pili fuatilia sana mienendo ya madereva na makonda,maana wengi ni wavuta bangi na hawana akili ya kawaida.

Na kma unashindwa kufanya hivyo nakushauri haraka uza gari tafuta bishara nyingine mkuu.
 
Makalangilo, p

Linapokuja suala la Anti-Corruption, tunaona ni jinsi gani ambavyo mazingira yanatengenezwa kwa anayetaka kufanya biashara ili ajiongezee kipato kuwa ngumu!

Kumbuka mtu huyu analipa malipo yote halali yatakiwayo ili kuendeleza NJI HII lakini wakamuaji wasio rasmi wana 30% yao kutoka ktk biashara hiyo! Hapo hapo wanataka uwaajiri watumishi hawa kwa mishahara minono!
 
Adha na kero hatimaye zimefikia mahali ambapo madereva wa daladala waliamua wao wenyewe kugoma na kuzipanga gari kuanzia hapo Sahara hadi barabara yote ya Pamba Rd ikawa haipitiki kwa msongamano magari zaidi ya mia na ushee, hadi Mkuu wa Mkoa akafika na kuuliza kulikoni!

Kero za rushwa na ufisadi wa trafiki zilimwagwa na wakulu wote wa usalama barabarani wakiwa wanajifaragua maana tatizo la kutokuwa na mahali pa kupakilia abiria lilizaa mradi wa kuwakomoa madereva.

Matokeo Mkuu wa Mkoa alishtuka kwa kutokuwa na habari na tatizo hilo na akaahidi kulitafutia ufumbuzi.

Mradi huu wa kifisadi ulioundwa na Mapolisi wa Trafiki wa Mwanza wa kuwapiga bao madereva kwa kupakia abiria bila kituo (Hakuna vituo)umewanufaisha wana usalama barabarani wengi hapa Mwanza wakiwa wamejijengea majumba kwa hela za kufisadi za kuwapiga bao madereva.

Stendi hiyo ya Sahara sasa imeruhusiwa kwa muda kupakia abiria na hali inaelekea kuwa shwari leo hii.

Nilipoanza biashara hii nilidhani ni biashara kama zingine kumbe ni maradhi makubwa! Sasa natafuta mnunuzi wa Hiace nitafute biashara nyingine.
 
Dont give up the fight ELLY!

Give them for u to survive!

Wape na uje uyaweke hadharani kuwa ushahidi tosha!
 
Ipo shughuli nyingine yoyote ungeweza kufanya tofauti na kubeba abiria ukitumia hiyo Hice? Pengine umewahi kuwa na mawazo ya namna hii, labda ukaona hailipi.

Unaweza kushirikisha wadau hapa? Unaweza kuambulia different ideas usilazimike kuuza Hice.
 

UZOEFU: CHANGAMOTO YA MADEREVA KUTOKUWA WAAMINIFU

Nilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.

Leo dereva anakwambia center-ruber imeisha, kwa hiyo badala ya Tsh 40,000 unapata 15.Kesho asbh ndo kwanza unaingia ofisini anakwambia timing belt imekatika...inatumika pesa ya jana na haitoshi inabidi utoe yako mfukoni.

Siku ya tatu na ya nne akikuhurumia ukakusanya 80 basi siku inayofuata unaambiwa nimepigwa bao na majembe. Ilikuwa nilipe 250,000 so nimewapoza 35,000. so hesabu yako mkuu hii hapa elfu tano! Gosh!!!

Picha hizo zimeendelea mpaka nikatia shaka, akipiga dereva wkt mwingine nachomoka kuthibitisha tatizo. Ajabu! Mara kadhaa ni uongo kunakuwa hakuna cha majembe wala mashoka! Bse of that nimewatimua kila nikigundua usanii huo, ndani ya mwezi 1 madereva wanne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.

Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!
 
Cha muhimu pata dereva qualified usichukue tu hawa wa mtaani ambao ni longolongo tu na wamezidi usanii. Au tafuta tender ya kubeba wanafunzi hela mabayo wazazi wa wanafunzi au shule sijui itakuwa inakulipa wewe and not trhough dereva.

Halafu siku nyingine kama hauko busy sana chukua daladala yako mwenyewe endesha ukiwa na konda kama weekend hivi halafu ucgheki mapato yake yatakuwa kiasi gani. Au weka limit ya kiasi kama ni laki kwa siku iwe laki na kama wamekamwatwa na majembe au traffic au nani wewe ndo udeal nao straight saa zingine si vizuri sana kuwaachia madereva to deal na kila kitu esp wa daladala.
 
Kumiliki daladala inabidi uwe kichaa kidogo.

Ni lazima uwe na akili kama za watu wanaofanya kazi kwenye daladala ndio mtaenda sawa, vinginevyo utakuwa unafanya kazi wa kuwafaidisha dereva na konda wake.
 
JS,

Nimejaribu kuwa nayo over the week end malipo yanakuwa mazuri hasa, wao wanakwambia ni kawaida kuwa na abilia wengi week end na siku za sikukuu (Ambazo ndizo siku mi nipo nyumbani)

Kwa upande wa pili ni vigumu mimi kumalizana na majembe na matrafiki maana nakuwa kazini. Na wao wanatake advantege hiyo!
 
Sumbalawinyo,

Unachosema ni kweli Sumbalawinyo lakini we upo kazini tangu asubuhi mpaka saa kumi na mbili huo muda wa kukomaa nao si ndo inakuwa issue? Ilifika kipindi nikaamua niipaki kabisa lkn bado nikaona si wazo la busara.
 
Pole sana mkuu,

Madereva wa daladala ndiyo tabia yao. pole sana! Tafuta tu dereva mwaminifu!

Ushauri:

Wewe mkabidhi gari. Mwambie hii nakukabidhi wewe. Mpunguzie hesabu mpaka labda 35. Kisha mwambie aihudumie kila kitu, Na wewe hutaki kusikia longolongo lolote. Mwambie akupe hesabu ya wiki nzima!

Hayo mambo ya bao, sijui nini ni juu yake, wewe hayakuhusu!

Hapo lazima uwe na roho ya paka la sivyo utakuwa unafanya biashara ya kuuza ubuyu na visheti kila siku!
 
Pole sana ndugu yangu.

Biashara nyingi ndivyo zilivyo, wafanyakazi wengi wanalazimika kuwa majambazi kwa sababu ya masha magumu na mishahara midogo. wewe mtu unamlipa laki 1.5 au 2 dar au arusha unategemea aishi maisha gani, analazimika kuwa fisadi.

Mambo ni hayohayo hata ukiwa na hoteli au roli. Kikubwa kama umeamua kufanya biashara ni kuchakarika na kuwa kaksi, wakati mwigine unaweka mtu wako kuwa konda au deree.

Ikiwezekana unasuka mwenyewe wakati mwingine. all in all nisingekushauri kufanya biashara ya usafirishaji kuwa biashara ya kwanza (i prefer uzalishaji mali).

Ukipata tenda ya kukodisha itakupunguzia presha.
 
Dereva mwaminifu atampata wapi?
 
biashara ya daladala ni sawa na kufuga kuku! kama hufugi au huendeshi mwenyewe personally, hesabu umeumia. sasa subiri nyepesinyepesi kuwa dereva wako naye kanunua daladala....................... mjini hapa
Hii nayo ni kiboko aisee! Sasa tutatokaje mjini hapa sie wenye mitaji midogo?
 
Biashara ya daladala kwa mfanyakazi wa ofisini ni ngumu. Anayefaidi ni dereva. Chukua ushauri wa Mkuu mmoja hapo juu wa kutafuta tenda za shule au mahoteli.
 
Biashara ya daladala kwa mfanyakazi wa ofisini ni ngumu. Anayefaidi ni dereva. Chukua ushauri wa Mkuu mmoja hapo juu wa kutafuta tenda za shule au mahoteli.
Natoa shukurani zangu kwa wote waliochangia mawazo. Nakubaliana na ukweli kuwa biashara ya daladala kwetu tunaofanya kazi ni ngumu mno.

Nimeanza kufanyia kazi wazo la kutafuta tenda za shule, so km kuna mwenye link si mbaya akaniunganisha.

Changamoto tuliyonayo ni kufahamishana juu ya ni biashara gani mfanyakazi anaweza kufanya na ni zipi amabazo zitamuweka katika wakati mgu kama mfanyakazi (I.e. zinahitaji very close supervision)

Naendelea kupokea mawazo yenu wakuu.
 
Pole sana ndugu yangu. Watafute wapenda tena mujahidina kabisa ndo anakufaa kwani wewe unawatafuta vibaka tu. Pia nenda kijijini kwenu tafuta kijana aliyetulia mwambie unampaka zi kisha awe konda kama kuna ujinga atakwambia tena unampamasharti utaona matunda.

Ishu ingine wewe usimkabidhi dereva gari mkabidhi konda ndio atafute dereva kwahiyo linakuwa lao sim moja ukiona hivi unapiga chini konda sio dereva waizi ni makonda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…