Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Aisee ukimwambia mtu yeyote anayefanya kazi maofisini akanunue guta atakushangaa sana! Lakini ukiangalia it really make sense.
Hizi biashara za magari ni nuksi sana aisee. hasa kama na wewe tajiri hujui spea za magari. yaani utafilisika.
nakumbuka yalinikumba haya haya ya mkuu hapo juu. nilinunua Hiace 14m baada ya miezi miwili niliuza 8m huku nikiwa nimeshaingia gharama zaidi ya 1.5m. its better ukajenga nyumba kama una mtaji
Hapo kwenye red nakubaliana na wewe ni kweli kuwa mfanyakazi ofisini lets say PPF tower ndo ofisi yake AKANUNUE GUTA, HATAKUBALI SIMPLY BECAUSE GUTA NA PPF TOWER ''WHERE AND WHERE'' I mean wapi na wapi?
Lakini tunasahahu yafuatayo:

1. Hata kama kama guta litagongwa leo to right off, hiyo laki tano uliyoitumia kununua guta haitakuuma sana kama 10M za hicho kikorola ulichokinunua showroom ya used vehicles
2. Spea za guta bei rahisi sana ukilinganisha na za korola
3. Kuirudisha hiyo 10M kwa 10,000/= ya kila siku ya teksi takes longer than laki tano kwa 15,000/=
4. Ukiona simu yako inapigiwa na ya dereva wa guta yako presure remains the same, lakini simu ya kutoka kwenye kikorola chako ina uwezo wa kukuharibia siku.
5. Guta haina traffic police, kikorola traffic nje nje
6. Guta haina kulipa kodi, bima, manispaa, etc hivyo hiyo 15,000/= inakuwa yako peke yako lakini ile 10,000/= ya teksi juwa kuwa unagawana na TRA, MANISPAA, BIMA. Kwa hiyo effectively hupati 10,000/= but may be 6,000/= ambayo italiwa na service ya gari na kulipia presure zote za simu ya dereva wako.

JAMANI SIFA NDO ZINAZOTUUWA.......... STUKENI...........SIFA HAZIKUBALIKI
 
Kaka pole, mimi miaka 3 iliyopita nilinunua saloon car 2 - ili nifanye taxi - kaka yalinikuta ya musa- hakuna hesabu yoyote gari zote zina matatizo kila baada ya siku mbili - matokeo yake mshahara wangu ukawa unaishia kutengeneza hivyo vimeo viwili. kwa hasira kimoja nikampa fundi wangu kwa hasira - kingine nikauza laki 7 pesa zote nikampelea mzee wangu. toka hapo sitaki kusikia taxi - bajaji au hiace. unaweza kufa siku si zako
 
Nyie acheni haya mambo; mkuu ngalihikinja nashukuru kwa kushare na vipi kuhusu management yake waendeshaji unawatoa wapi na inakuwaje kwenye ukusanyaji? mfano naishi Kinondoni.
 
USHAURI: MSHAHARA NA UKOMO WA DEREVA KUHUSU GARI
Kila biashara/shughuri yoyote ina ugumu na karaha zake

Biashara ya daladala inalipa na ni nzuri kwa wale wasio na muda mchana .As rule of thumb. HIACE (Tajiri=24days x 45,000/=, Service= 2days x 45,000/=, trafic &s umatra & majembe=2days x 45,000/=, Dereva= 2days x 45,000/=).Break even ni 22months.
Hayo ndiyo mahesabu ya makadirio kwa uzoefu.

Katika utafiti nilioufanya wamiliki wa daladala wanaoendelea vizuri wanafanya yafuatayo bila kukosa.

1. Hakikisha siku ya service gari inatengenezwa vizuri na unasimamia
2. Gari yako iwe nzima sana (pesa ya gari si yako hadi utakaporudisha mtaji).
1. Mafuta full tank ni ya tajiri, yanakaguriwa kituo cha mafuta au anapopaki daily.
2. Leseni na certificate vyote original anashika tajiri
3. Mshahara kwa mwezi kwa hiace ni 50,000/= coaster ni 90,000/= kwa mwezi.
4. Akilete hesabu pungufu, akipoteza suti, jeki, spanner au uzembe wowote unaandika deni anakatwa mwisho wa mwezi.
5. Ajira yake iwe na referee, barua ya mjumbe na ujue kwake na awe ameoa
6. Ukiendesha gari kwa miezi 30 fikiria kuuza, kwa kuwa hiyo ndo faida safi
7. Chagua garage 2 zenye mafundi unaowaamini ili ukipigiwa simu, nawe unawaelekeza dereve apeleke garage unatakayo mwambia,

DEREVA ASIPEWE MADARAKA YA KUTENGENEZA GARI YAKO

Hayo machache, pia maguta yana karaha/kero sana, ila ukifanya kama ndo maisha yako inakutoa kama vile daladala.
 
Kwa kweli biashara ya daladala ni ngumu kutokana na madereva tulio nao. dereva anaweza kukupigia simu kwamba kuna tatizo akijua huna nafasi, ukimwambia nisubiri utakuta anaendelea kula vichwa atakwambia ameshatatua tatizo. ni vema mara nyingine akikwambia kuna tatizo mwambie aliache mpaka utakapokuwa na muda, utashangaa hakuna pancha wala timing belt itakayo katika.
 
Mimi nilishaifanya biashara hiyo miaka minne iliyopita. Niliamua kusitisha ili nijipange upya.hata hivyo nataka kurudia tena hivi karibuni lakini nahisi nimepitwa na wakati.tafadhali nijulisheni hesabu ya tajiri kwa hiace, coaster, DCM na hay mabasi makubwa ambayo ndiyo real city bus.

Nawasilisha.
 
kaka pole, mimi miaka 3 iliyopita nilinunua saloon car 2 - ili nifanye taxi - kaka yalinikuta ya musa- hakuna hesabu yoyote gari zote zina matatizo kila baada ya siku mbili - matokeo yake mshahara wangu ukawa unaishia kutengeneza hivyo vimeo viwili. kwa hasira kimoja nikampa fundi wangu kwa hasira - kingine nikauza laki 7 pesa zote nikampelea mzee wangu. toka hapo sitaki kusikia taxi - bajaji au hiace. unaweza kufa siku si zako

Mhhhhhhhhhhh! Hii chumvi imezidi kwenye mboga.
 
Kila biashara/shughuri yoyote ina ugumu na karaha zake.
Biashara ya daladala inalipa na ni nzuri kwa wale wasio na muda mchana .As rule of thumb. HIACE (Tajiri=24days x 45,000/=, Service= 2days x 45,000/=, trafic&sumatra&majembe=2days x 45,000/=, Dereva= 2days x 45,000/=).Break even ni 22months.
Hayo ndiyo mahesabu ya makadirio kwa uzoefu.

Katika utafiti nilioufanya wamiliki wa daladala wanaoendelea vizuri wanafanya yafuatayo bila kukosa.
1.Hakikisha siku ya service gari inatengenezwa vizuri na unasimamia.Gari yako
iwe nzima sana.(pesa ya gari si yako hadi utakaporudisha mtaji).
1.Mafuta full tank ni ya tajiri, yanakaguriwa kituo cha mafuta au anapopaki
daily.
2.Leseni na certificate vyote original anashika tajiri
3.Mshahara kwa mwezi kwa hiace ni 50,000/= coaster ni 90,000/= kwa mwezi.
4.Akilete hesabu pungufu, akipoteza suti, jeki, spanner au uzembe wowote
unaandika deni anakatwa mwisho wa mwezi.
5.Ajira yake iwe na referee,barua ya mjumbe , na ujue kwake na awe ameoa.
6.Ukiendesha gari kwa miezi 30 fikiria kuuza , kwa kuwa hiyo ndo faida safi.
7.Chagua garage 2 zenye mafundi unaowaamini ili ukipigiwa simu, nawe unawaelekeza dereve apeleke garage unatakayo mwambia, DEREVA ASIPEWE MADARAKA YA KUTENGENEZA GARI YAKO

Hayo machache, pia maguta yana karaha/kero sana , ila ukifanya kama ndo maisha yako inakutoa kama vile daladala.

Mkuu hiyo kwenye red. Mbona ni kidogo sana? Huyu mtu ataweza kukufanyia kazi nzuri kweli kama unamlipa pesa hiyo kwa mwezi ambayo hata haitoshi kwa pango la nyumba?
 
JF MEMBERS,

Biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili (24 seats)

tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki (utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.

Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.

Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.

Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.
 
Mkuu pole sana,

Tafuta vijana uwatrain halafu uwape magari hayo, hao walioacha au kuacchika sehemu zingine watakupasua kichwa kama unavyosema.

Mimi pia nafikiria kuingia kwenye hiyo Industry, nini ushauri wako? Nina jamaa yangu anazo daladala tatu yeye anawachukua watu anawapeleka driving halafu anawapa magari yake
 
Kama hautosimamia mwenyewe i.e fulltime management nakushauri ufanya investment ktk secta nyingine. huyo jamaa anayewapa trainning anawatoa bush au anawachukua vijana hapa town?
Mkuu pole sana
Tafuta vijana uwatrain halafu uwape magari hayo, hao walioacha au kuacchika sehemu zingine watakupasua kichwa kama unavyosema.
Mimi pia nafikiria kuingia kwenye hiyo Industry, nini ushauri wako? Nina jamaa yangu anazo daladala tatu yeye anawachukua watu anawapeleka driving halafu anawapa magari yake
 
I did it and saw it pays though trafick police are the major hindrance to the business. NA BILA RUSHWA BIASHARA ITAKUWA NGUMU...HIVYO NAKUSHAURI UTOE RUSHWA KWA TRAFIKI BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA! I DONT JOKE KATIKA HILI
PM ME FOR MORE
 
kama hautosimamia mwenyewe,i.e fulltime management nakushauri ufanya investment ktk secta nyingine. huyo jamaa anayewapa trainning anawatoa bush au anawachukua vijana hapa town?
Vijana anawachukua bush sehemu aliyotokea yeye (Njombe), the way alivyowajenga wanaona wao ni sehemu ya biashara hiyo hata kama gari linashida wanatoa taarifa mapema sana na wakifikia target/month anawareward kidogo. Kabla ya hapo alichukua wahuni wa hapa mjini ilikuwa wakishapata pesa yao tu wanaanza kupiga simu gari limekufa mara wamekamatwa ilikuwa balaa.
 
ntaanza kulifanyia kazi hilo swala
Vijana anawachukua bush sehemu aliyotokea yeye (Njombe), the way alivyowajenga wanaona wao ni sehemu ya biashara hiyo hata kama gari linashida wanatoa taarifa mapema sana na wakifikia target/month anawareward kidogo. Kabla ya hapo alichukua wahuni wa hapa mjini ilikuwa wakishapata pesa yao tu wanaanza kupiga simu gari limekufa mara wamekamatwa ilikuwa balaa.

Mkuu Mahesabu nitaku PM now now
 
Pole Sana mkuu NM; hili ni tatizo linalotukabili wa-TZ wengi kwamba kila kitu tunahitaji ku-manage wenyewe, mwisho wa siku tunashindwa. Mimi ningekushauri kupitia hapa jukwaani ukawa-mobilze wale wote ambao mko kwenye same industry, halafu mka-form one company ambapo hisa ni idadi ya magari yako na kuajiri managers, technicians, accountants, drivers etc. Tukiendelea na movement hii nafikiri tunaweza kuwa na sustanable business. Kumbuka UMOJA NI NGUVU, NI UDHAIFU, inawezekana kuna ukweli katika hili.
 
Mkuu NM; hizo gari ziko kwenye condition gani? na zinafanya route ipi?
 
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.

Ebu nijuze hizo dala dala ziko kwenye hali gani, lini ulizisajili na zina tlb route gani.
 
Nashauri utafute madreva walio committed na wanathamini kazi yao walipe au aingia makubaliano mazuri katika ukusanyaji ili nao wafaidi, harafu tafuta root za wastaarabu kama vile Masaki, Mwenge nk. Hii inasaidia kwa kiasi fulani..
 
Mkuu nami nfkr kuingia ktk hii industry. Mi ushauri kwako ni kwamba kati ya w2 2(dereva au konda) ambao watakuwa kwenye hizo daladala yako mmoja awe ndugu yako kwani zimwi likujualo halikuli likakwisha. Zikikuwa zaidi umaweza kutafuta manager na wataalamu wengine
 
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.

Tuwasiliana hata mie ninazo hapa mjini nitakupa uzoefu wangu,usichanganye hii biashara na kazi zako zingine .Awali nilikua nafanya hivyo nilitaka kuchanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom