Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

mkuu .... mimi niliwahi kuwa na nissan caravan mwaka jana nili import direct from japan ... niliitumia kwa matumizi yangu mwenyewe...hii gari ni nzuri sana ...fuel consumption and mechanically it is very robust ....

cha kushangaza alikuja mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha akaiona hii nissan caravan nimeipaki sehemu moja pale sinza akasimamisha gari yake akaulizia mwenye gari na baadae akanipata .... aliitaka hii gari na kesho yake alinipa pesa niliyotaka cash na kuipeleka arusha ...hizi nissan caravan zipo nyingi sana Arusha ... na ndizo zipo popular aka vi fodi au kama daladala za dar ... niliuliza ni kwa nini nissan na siyo Toyota haice nikaambiwa nissan ni ngumu na vumilivu sana na pia kwa arusha spea zinapatikana kwa urahisi Nairobi na ni genuine spare parts
 
mm nakushauri toyota zinahimili sana ila kama ni mkoa wa arusha nissan utafaidi kwa vile hali ya hewa na baridi zinatabia ya kuchemsha sana
 
Kaulize wenye daladala ndo wenye uzoefu.

Yupo kwenye ukumbi sahihi, so kama umekosa jibu la swali alilouliza hapa ni vyema kukaa kimya na si urojo unaoandika hapa!!! Wengi tunaelimika kupitia humu na si kumbi za walevi kama unavyofikiria!!

Mwenyewe nina caravan hapa Iringa na nimepata mawazo mazuri sana hapa ikiwamo kuipeleka Arusha aisee Iringa route zake fupi fupi sana na abiria bado ni tatizo!!
 
Peleka Arusha man kwasababu arusha abiria ni wengi sana so inalipa sana na pia caravan ni nyingi so spair zake ni very ize kuzipata mimi mwenyewe naizunguusha pale ila sasa tatizo mabao kwa trafki yaani kama una ndugu pale trafki bora umtumie huyo ili waijue v kwanza gari ya nani wasikupige mabao!maana wale jamaa wanaboha sana
Yupo kwenye ukumbi sahihi, so kama umekosa jibu la swali alilouliza hapa ni vyema kukaa kimya na si urojo unaoandika hapa!!! Wengi tunaelimika kupitia humu na si kumbi za walevi kama unavyofikiria!!

Mwenyewe nina caravan hapa Iringa na nimepata mawazo mazuri sana hapa ikiwamo kuipeleka Arusha aisee Iringa route zake fupi fupi sana na abiria bado ni tatizo!!
 
Wajameni ,nimerudi back to square one.::A S 13:
jamaa ameona oportunity,anataka nimmpe all the documents,afanye management,amepunguza hesabu yangu by thirty percent,then anakata management fee around Ten percent.#%^
nimeamua kutafuta mtu nimuajiri,pia nafikiria nimtoe nani bush aje town nimpeleke driving school ,awe supervisor,{ushauri wa JF member}
ila MKUU JAY2da4 naona umefanikiwa kuwa nazo Kumi na Tano,with a management of only Four people hiyo imenitia moyo sana,Sasa nimeamua KukAza Boot kama nilivyoshauriwa na mageuzi1992 .
Bado napokea maoni na ushauri ktk hili jambo
 
ni kumpata mtu mwaminifu tu man mie yangu inakwenda vizuri pale arusha nimempa trafki mdogo wangu ili aisimamie hesabu kwa siku inaingia mie nachukua kwa mwezi!
 
Markach: Ushauri wa bure usifanya biashara ya daladala!!. Mimi nilibahatika kufanya hii biashara miaka ya 1996-1997 na kuna matatizo mawili makubwa (a) Huwezi kupanga bei na bei inapanda polepole kuliko mfumuko wa bei. serikali inapanga bei hivyo ni biashara mbaya sana (2) Huwezi kupanga bei ya mafuta hivyo kama bei ya mafuta ikipanda huwezi kupandisha bei kwasababu bei inapangwa na serikali. Hali hii ilisababisha Isuzu NPR na Costa zishidwe kufanya biashara na hali ya daladala ni ya duni kuliko 1996!!.

Unaweza ukafanya biashara ya tender, fungua kampuni halafu katafute shele zinazohitaji magari halafu ingia mkataba na shule wa kuwapeleka watoto majumbani baada ya shule. Vilevile kama unamagari mazuri peleka card zako balozini ili uweze kuchukuwa wagani mbalimbali wanaokuja na group zinazotoka nje. Hii itakusaidia uhakika wa biashara, kukua kwa biashara na target yako ya watu ni nzuri badala ya kukimbizana na makondakta na matrafiki. Mimi nashauri usiige badilisha kidogo utaona matunda! Huu ni ushauri wangu ndugu
 
Huyu mzalendo kaulizia mahali pake kabisa...kwa Arusha Nissan DX8 na TD27 petrol ndo ziko nyingi. Nilimuuliza jamaa yangu anazo kama saba hivi anasema ni cheap ku maintain na service yake haihitaji vitu vingi sana....
 
Markach: Ushauri wa bure usifanya biashara ya daladala!!. Mimi nilibahatika kufanya hii biashara miaka ya 1996-1997 na kuna matatizo mawili makubwa (a) Huwezi kupanga bei na bei inapanda polepole kuliko mfumuko wa bei. serikali inapanga bei hivyo ni biashara mbaya sana (2) Huwezi kupanga bei ya mafuta hivyo kama bei ya mafuta ikipanda huwezi kupandisha bei kwasababu bei inapangwa na serikali. Hali hii ilisababisha Isuzu NPR na Costa zishidwe kufanya biashara na hali ya daladala ni ya duni kuliko 1996!!.
Unaweza ukafanya biashara ya tender, fungua kampuni halafu katafute shele zinazohitaji magari halafu ingia mkataba na shule wa kuwapeleka watoto majumbani baada ya shule. Vilevile kama unamagari mazuri peleka card zako balozini ili uweze kuchukuwa wagani mbalimbali wanaokuja na group zinazotoka nje. Hii itakusaidia uhakika wa biashara, kukua kwa biashara na target yako ya watu ni nzuri badala ya kukimbizana na makondakta na matrafiki. Mimi nashauri usiige badilisha kidogo utaona matunda! Huu ni ushauri wangu ndugu
Kamundu mkuu, Ahsante sana
Umenifungua macho pia mimi japo muuliza swali ni mwingine, hii ndio raha ya jamii forum bwana.
Lakini mkuu mashule yanalipa vizuri kweli unaweza kucover cost za uendeshaji?
 
Naombeni kuuliza

Kwa siku daladala dar au arusha zinaingiza kiasi gani
 
i did it and saw it pays...though trafick police are the major hindrance to the business....NA BILA RUSHWA BIASHARA ITAKUWA NGUMU...HIVYO NAKUSHAURI UTOE RUSHWA KWA TRAFIKI BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA....! I DONT JOKE KATIKA HILI
PM ME FOR MORE

Mkuu,
Naomba kujua hiyo rushwa haiwezi epukika? Ni nini hasa hutokuwa nacho ili utoe rushwa? Ina maana ukifuata masharti yoote yaani yoote bado inabidi utoe rushwa??? Kama gari imelipiwa kila kitu, ina fire extinguisher nzuri, reflectors, dereva anafunga mkanda, anasimama vituoni tuu, hajazi watu what will make him pay rushwa?? Naomba kuelimishwa ingawa sifanyi hiyo bness. Mimi naendesha private car napita popote tz hii sitoi hata senti moja kwani nina kila kitu kwenye gari langu labda kwenye speed ya 30 aur 50 ndo wanikamate lakini nitatoa elfu ishirini na wanipe notification na risiti ya malipo. Otherwise sitoi chochote....
 
Mashule na balozi zinalipa kwanza kwasababu ni mkataba hata kabla ya kazi. Kitu kimoja tu unabidi uwe tofauti kidogo mfano. Kanunue vitabu vya invoice na mkubaliane mtalipana kwa trip au siku ngapi halafu unaweka record na kutuma invoice. Hii wanaipenda sana kwasababu wanakuwa na record na wanaweza ku budget kirahisi. Vilevile hakikisha gari yako ina Air Condition. Dereva wako vilevile avae vizuri kama ukiwatafutia kama uniform nzuri hivi kwasababu wanaudumia watoto dereva asiende kimtaani. Vitu vidogo kama hivi vitakupa biashara sana.
 
Dereva akiwa msafi, akiweza kuongea english kidogo kwa ukarimu. Gari ikiwa safi na AC inafanya kazi vizuri. Gari ikiwa inafanyiwa service kwa wakati so haisumbui ikiwa kazini na inapotokea tatizo basi unawafaamisha in advance, kuenda na wakati (kuwa on time) vitu vikienda ki proffesional kama unafanya kazi na hawa mabalozi, watakupenda sana na nirahisi hata kudai ela nzuri.
 
Asante sana kwa ushauri wenu mwingi wenye busara nitaufanyia kazi
 
raha ya ngoma uingie ucheze,huwezi jua Adha ya matrafiki kwa daldala mpaka uwe mdau ktk hii bizness.
trafic wa dar huwa wana targets za kila siku mtu apate revenue ya 50,000 and above.
so kila dreva wa daladala anakuwa analipa kitu inaitwa dambwe daily.around elfu4-10. sasa do the math. kwa daldala za ubungo posta zipo 200X6000=`1,200,000 gawa kwa trafic 12, wanaosimamia hiyo ruti for that day.kila mtu anapata laji moja. hapo tena kila mtu anatakiwa apelelke kwa bosi ,anagalau 15% of mapato.

nadhani sasa picha umeipata.
Mkuu,
Naomba kujua hiyo rushwa haiwezi epukika? Ni nini hasa hutokuwa nacho ili utoe rushwa? Ina maana ukifuata masharti yoote yaani yoote bado inabidi utoe rushwa??? Kama gari imelipiwa kila kitu, ina fire extinguisher nzuri, reflectors, dereva anafunga mkanda, anasimama vituoni tuu, hajazi watu what will make him pay rushwa?? Naomba kuelimishwa ingawa sifanyi hiyo bness. Mimi naendesha private car napita popote tz hii sitoi hata senti moja kwani nina kila kitu kwenye gari langu labda kwenye speed ya 30 aur 50 ndo wanikamate lakini nitatoa elfu ishirini na wanipe notification na risiti ya malipo. Otherwise sitoi chochote....
 
Jamani kuhusu trafki ilikua kabla ya Mpinga!
Hao madereva wanawadanganya,siku hizi Trafiki wanaogopa
sana hongo ya daladala!
Kama kuna kosa wanatoa notification na malipo na kituoni.
Sasa hapo kama gari lako halijakamilika siku nzima wataimaliza
kituoni.
Lakini kwa zile njia zisizo rasmi siwezi kusema kwa kua
hata daladala zinazopita huko hali yake haisemeki.
Mimi sio Trafiki ila ni uzoefu wangu mdogo na ufuatiliaji
wa karibu wa biashara hii.
 
masharti yako moja kutunza gari,hesabu kila siku icpotimia deni
isipotimia ni deni, na asipolipa deni? Ukimshtaki dereva kwa madeni ya buku nne buku kumi utalipia zaidi kufungua kesi kuliko madai.

Na sharti la "kutunza gari" unalipima vipi? Akirudisha gari ma spring yamekatika kwa kuparamia mifereji akakwambia spring ilikuwa imechoka, utabisha? Hilo sharti limejaza mkataba tu.

akigonga kwa uzembe wake analipa,
dereva wa daladala akisababisha damage ya milioni 2, atakulipa nini mjomba? Hukuweka bima?

akikamatwa na makosa ya uzembe kama kutokuvaa uniform akiandikiwa ni yake, kusimama juu kwa juu akiandikiwa ni yake alafu
akipigwa notification za uhakika na asipotoa anaswekwa lupango, utamfata mwenyewe kumdhamini na kulipia gari lako litoke. Upende, ukatae, huwezi kusema "makosa ni yake," itakula kwako.

wape mtaji wa full tanki na kila siku akirudisha iwe full
Na dereva mwenye uelewa hawezi kukubali kizunguzungu cha "mtaji wa full tank." Mtaji wa full tank ndio shilingi ngapi? Mafuta yanapanda bei asubuhi mchana na jioni, there is no such thing as "mtaji wa full tank."

Angalia tena huo mkataba, una vingi vya kufikirika tu.
 
Mawazo yote yaliyotolewa ni mazuri, lakini hili la kuwa na kampuni (kikundi cha ushirika) wa daladala ni zuri zaidi, kwani zote zinakuwa chini ya management moja. Naamini kama mkianza wawili watatu si muda mnaweza kumobilize wengine.
Na kama ni kuendesha biashara mmoja mmoja, jaribu kuwafanya moja au baadhi ya yafuatayo:
1. Wafanye mdereva na makonda kuwa ni sehemu ya biashara. Watu wanasema Mchawi mpe mwana kulea.
2. Njia ya kumzawadia mwajiriwa anapofanya vizuri ni nzuri. Bora kuwana faida ndogo iliyo "constant" kuliko faida kubwa ya siku moja.
3. Sipendelei mambo ya rushwa lakini inaonesha hili haliepukiki kwa bongo. Ikibidi tafuta "traffic" unayemwamini ailinde biashara, ni bora kuwa na mlaji mmoja kuliko walaji wengi.
 
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.
HAKIKISHA USALAMA NA UZIMA WA GARI KILA SIKU

Pole sana ila zingatia ushauri huu: Kwanza kabisa hakikisha magari yako wakati wote ni mazima na hayana hitilafu yeyote inayoweza kuyafanya yasimame. Pili hakikisha kila siku unasoma millage kabla gari halijaanza safari na mara limalizapo safari zake. Tatu hakikisha madereva unaowakabidhi g magari yako wana lesseni halali za udereva na hakikisha unawafahamu vizuri, makazi yao, wadhamini na viongozi wao wa serikali za mitaa wanayoishi na ikiwezekana wawe na wadhamini wakuaminika.

Hakikisha kuwa kila wakimaliza kazi jioni/usiku, unapima (mwenyewe kiasi cha mafuta kilichobaki na kuongeza hadi kiasi ambacho unajua kitatosha kwa kazi ya kesho) awali nilikueleza kuwa hakikisha kuwa unarekodi millage ili kujua ni umbalii gani kwa siku gari yako inasafiri, hii itakusaidia kujua wastani wa mafuta yanayohitajika kwa siku. Kwa nchi kama kenya madereva hupewa sheet maalumu ambayo hurikodi mlolongo mzima wa safari na gharama zote ambazo dereva atakuwa ametumia
kwamfano:

Ubungo - posta -abiria 24 @ sh 300 =7200/= km 9
posta -Ubungo- abiria 30@ sh 300=9000/= km 9 n.k

Aidha unatakiwa kuwa na mkaguzi (manager) wa kuaminika ambaye kwa nyakati tofauti atakuwa anafuatilia nyendo za gari lako na kuhakikisha kuwa madereva wakati wote wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Gari inapoharibika hakikisha unafika wewe mwenyewe/msimamizi wako na kuhakikisha gari linapelekwa kutengenezwa kwenya gereji zinazoaminika.

Hakikisha gari lako umelipa kodi zote kuepuka usumbufu wa kukamatwa na askari na kusababisha upotevu wa mapato. haya ni machache tu ila biashara ya daladala inahitaji usimamizi wa karibu na umakini mkubwa pia hakikisha dereva, fundi na kondakta wako unawapa vivutio na mikataba inayoeleweka ili waifanye kazi yao kwa bidii na uaminifu.
 
raha ya ngoma uingie ucheze,huwezi jua Adha ya matrafiki kwa daldala mpaka uwe mdau ktk hii bizness.
trafic wa dar huwa wana targets za kila siku mtu apate revenue ya 50,000 and above.
so kila dreva wa daladala anakuwa analipa kitu inaitwa dambwe daily.around elfu4-10. sasa do the math. kwa daldala za ubungo posta zipo 200X6000=`1,200,000 gawa kwa trafic 12, wanaosimamia hiyo ruti for that day.kila mtu anapata laji moja. hapo tena kila mtu anatakiwa apelelke kwa bosi ,anagalau 15% of mapato.

nadhani sasa picha umeipata.

Hiyo Dambwe ipo kwenye sheria gani. Tatizo lenu nyie ni waoga tu na hamtaki kujifunza sheria na taratibu. Hamtaki kabisa kusoma.
Mimi huwa nasafiri na mabasi sijawahi ona Dar express wanatoa hela lakini safiri na gari kama taqwa sijui nini wanajilengesha wenyewe.
 
Back
Top Bottom