Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Sasa sinasikia mabasi ya kasi yanakuja bongo watu wa biashara ya daladala nasikia wanaanza kuziuza kiaina zikiwa zinalipa sasa angalia usiigie mkenge

Mkuu nimekupata, nitatafuta habari zaidi.
 
Usijidanganye kufanya biashara ya Daladala ,wewe kama siyo dereva wa hilo dala dala,basi uwe inspecta wake,ukae kituo cha basi linalopita ili uwe unawaona na kuhesabu tripu zake.
kama unapesa bora ununue canter/fuso ndogo ili ufanye biashara ya shamba na ukodishe hilo gari lako.

mimi namiliki daladala najua wizi wake ,hvi sasa nataka kuziuza niwe mfugaji fulltime

wizi ni popote mkuu. Kikubwa ni kuangalia kama unaletewa mahesabu kamili.
Mfanyakazi yeyote unapombana na yeye ndio anazidi kutafuta mbinu za kuibia kwa kukukomesha.
 
Note taken, lakini vipi ukipanga hesabu ya kukuletea na usisikilize hadithi yoyote?
 
wizi ni popote mkuu. Kikubwa ni kuangalia kama unaletewa mahesabu kamili.
Mfanyakazi yeyote unapombana na yeye ndio anazidi kutafuta mbinu za kuibia kwa kukukomesha.

Thanks Husninyo. Naona kila mtu akiwa na biashara lazima aibiwe, iliyopo ni kufuta loopholes za wizi. Maana hakuna mwajiriwa asiyeiba, hata mlinzi mlangoni na ndo maana watu wanaishi kwa mishahara midogo.
 
. Maana hakuna mwajiriwa ndo maana watu wanaishi kwa mishahara midogo.

hilo halina ubishi. Watu siku hizi wanatafuta kazi kwa kuangalia chances za kuiba na sio mishahara.lol
 
Mkuu nimekusoma!ila ungekua vyema utueleze kama una mpango wa kununua gari gani,coaster,Dcm,eicher,nissan,au isuzu?ukishanipa hiyo plan mm ntakushaur vizuri sana about that business.
 
Naombeni msaada kwa hili. Nimefanikiwa kupata mtaji sehemu, nikaamua nifanye investment kwenye daladala na sehemu kununua shamba Visiga. Katika pilikapilika za kuitafuta gari inayomudu mazingira ya daladala nikakutana na jamaa mmoja ambaye amenidiscourage kabisa kuhusu hiyo biashara kwamba kama nataka kufa kwa presha basi niingie huko! Jamani kama kuna anaufahamu na hii biashara naomba msaada japo imeshaniingia akilini kabisa kuwa lazima niifanye.

Mkuu mimi binafsi nimejaribu ii biashara ni kweli inakupa presha maana dereva na konda wake ndo waakao faidika ni iashara yako ni sisi wewe mwenye mali labda ushindi ndani ya gari kila siku na hata hivyo ni gumu mkuu.try another business proposal
 
mkuu me na daladal lkn zimenitesa sana mpaka nieamua kuuza nijenge nyumba za kupanga so sikushauri kabisa kuingia huko lbda ume hel yako haina kazi nyimgine
 
gongo la mboto chanika gari zote zinafanya kazi ila inabidi ubate nissan caravan qd, nissan caravan td27 haziwezi moto mwingi ni za safari za kila siku. Suka atalalamika sana kama ukimpa td maana watampita njiani vituo vyote hasa najua chanika kuna gari vijana wanasema mnyama yaani toyota 5l inakimbia coaster haifati.
Kwa gharama maana hiace about 22M and nisaan qd about 16M but hesabu sawa ya tajiri.
Ila lifetime ya hiace is about 7-10 years, wakati nissan ni 2-5 years kwa uzoefu wangu hasa kwa high way.
Ninayo ilikua inaenda Arusha karatu, hiace 5l na Nisan Qd
 
Nafikiri biashara yoyote ile hata kama unasimamia mwenyewe kuibiwa kupo. Suala la msingi ni kupunguza rate ya kuibiwa.. Kuna wadau ambao wameshafanya hii biashara ikawashinda but nafikiri wangetupa sababu mbili tatu au changamoto zilizowafanya wakashindwa na sio kumkatisha mtu tamaaa tuu bila kumpa mwangaza kwa nini unasema hivyo. Naamini kabisa biashara ya usafiri inalipa, hawa madereva, kondakta wanaiba but la muhimu ni kuhakikisha kuwa wanakamilisha hesabu, wanatumia gari vizuri na kuwafuatilia kwa ukaribu wasililete story za uongo kama vile kukamatwa na trafiki na kadhalika. Ukiwabana sana wao watakula wapi? hii ni kazi yao na wao wanahitaji kula, na kutunza familia zao. Ni maoni tu.
 
Search humu utakutana na thread kibao zinazoongelea changamoto za biashara hii
 
naombeni ushauri kwa wajuao kwa undani hii biashara ya daladala...nina 8M na nataka kutafuta Hiace used kwa biashara Arusha...hii inakuwaje hebu nipeni maushari yenu wakubwa
 
Kuna jamaa yangu anazo kama 6 ivi ila ananiambia chonde chonde ussiingie uku heri utafute biashara ingine nkimuuliza why ananiambia zina usumbufu wa kufa mtu waweza chinja mtu.

Na akanipa mfano wa dreva wake mmoja ambae kwa sasa anamiliki GX100 apo ndo nkachoka.

Wadau mtujuze yaliyomo kwa hii biashara as personally naiona inalipa
 
transport kwa ujumla wake inalipa
ila usimamizi wa karibu unatakiwa pia kodi ni nyingi sana
 
Kuna jamaa yangu anazo kama 6 ivi ila ananiambia chonde chonde ussiingie uku heri utafute biashara ingine nkimuuliza why ananiambia zina usumbufu wa kufa mtu waweza chinja mtu.
Na akanipa mfano wa dreva wake mmoja ambae kwa sasa anamiliki GX100 apo ndo nkachoka.
Wadau mtujuze yaliyomo kwa hii biashara as personally naiona inalipa
hizo sita alizinunua kwa wakati mmoja au? Kama alikuwa ananunua moja moja usumbufu alikuwa hauoni hadi awe anaongeza idadi!

Hujui kama usumbufu ni mojawapo ya changamoto na ni lazima ukumbane na changamoto katika kila biashara.

Halafu dereva kumiliki gx100 imekuchoshaje? Kama unahisi hela ametoa hapo ndio ujue kuwa kweli biashara inalipa.
 
inalipa sana kama utakaa mlangoni mwenyewe

kwanini ukae mlangoni mwenyewe? We mpangie dereva kiasi anachotakiwa kuleta kama ni per day au week huku unaendelea na mambo yako.
 
kwanini ukae mlangoni mwenyewe? We mpangie dereva kiasi anachotakiwa kuleta kama ni per day au week huku unaendelea na mambo yako.

Hapo ndipo chanzo cha tatizo. Hivi unajua chombo kinachoka kadiri kinavyotembea? Licha ya kumpangia kiasi cha kukuletea iwe kwa siku au wiki, vile vile uhakiki wa kilometa ni lazima. Hapo ndipo watu wengi wanashindwa.
 
At least uwe na hiace 8 kwenda mbele. Kuwa na moja ni hedeki. Madereva wasumbufu, matrafiki, usipokuwa mwangalifu utalizwa kwenye spea.
 
Back
Top Bottom