Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Mkuu kila kitu kina challenges zake maana hata ukitaka kuanzisha kibanda cha mama ntilie lazima watu watakuja hapa watasem kila kitu kibaya.

In fact hii biashara ina chngamoto kama alizosema mkuu hapo juu, lakini cha msingi ni kukaa na kutafuta dereva mzuri na ikumbukwe kuwa hata dereva yupo kazini so wewe unatakiwa kupata chako, na gar ipo katika hali nzuri.

Mfano mimi namiliki Hice tatu hapa Arusha mwanzo nilihangaika kupata dereva mzuri nilipoanza na gari moja 2010 na ilinichukua miezi mitatu nikampata dereva ambaye mpaka leo ninae na ni mwaminifu kwa gari angu 100% hata akinambia nimepata special ya mbeya namwambia mimi niletee pesa kazaa tu chapa mwendo, anaenda na kurudi na mkwanja wangu na gari full tank. huyu pia alitafuta hawa wengine niliponunua gari na wako poa sana.

Kazi kwangu huwa nikitoka kazini ni kupitia shell na inapofika mida ya saa mbili kamili hadi saa mbili na dk 15 huwa wote wameishafika wanajaza mafuta nikiwepo na wananipa pesa yangu, wanapaki gari.
 
NIvema ukapata ushauri kwa wanaofanya hii biashara ili ujue inaendeshwa vip, kama we ni mgeni hata Dreva utakaempata atakuzingua kwenye hesabu. pia hutakiwi kujua mapato ya siku ni kiasi gani maana utashidwa kufanya biashara, kama mtindo ni kukubaliana na hesabu na Dreva itabidi uzingatie hapo maana ile kazi ni ngumu sana, madreva wanapata changamoto kubwa sana na hawa Ma-Traffic
 
Mimi nilibahatika kuwa Manager wa biashara ya daladala Arusha na Dar miaka ya 1996-1997 nilipomaliza kidato cha sita. Niligundua baada ya serikali kuanza kupanga nauli za daladala na bei ya mafuta kuongezeka biashara ilikuwa ya hasara kabisa. Bei zilivyokuwa zinapangwa zilikuwa ni kisiasa bila kuzingatia bei ya mafuta wala spare za magari. Biashara ya mabasi ikaanza kupungua na biashara ya Toyota Hiace iliongezeka sana kwani hizi sio gari za kusafirishia abiria.

Sasa hawa wanaotaka kujiingiza kwenye biashara ya Daladala Dar watafilisika kwani bei itakuwa inapangwa na wanasiasa badala ya hali ya uchumi na ushindani. Mayor wa Dar anaweza kuwa ndiye mpanga bei za Daladala. Kama unapesa fanya bishara za magari ya kwenda mikoani au magari ya mizigo lakini Daladala ni hasara kubwa
 
Sikubaliani na wewe biashara yoyote ili kufanikiwa inabidi uzingatie kanuni za biashara lakini biashara ya daladala inafanya na mtu yoyte aliyesoma ,asiyesoma,darasa la saba mwenye elimu ya chuo kikuu kikubwa biashara hii inaendeshwa kienyeji kiasi kwamba wanaofaidi ni watu wengine wasiochangia hata senti kama traffic,madereva na makonda lakini kun abaadhi ambao wanafanya biashara hiyo hiyo na wanamiliki mabasi zaidi ya 10 na kuendelea
 
KAMUNDU UMKWELI SANA. MIE DALADALA LANGU NAHISI NTALIPELEKA KWA WATU WANUNUA SKREPa. MAANA WAFANYAKAZI WANGU NI MASHTAN. TRAFIKI WANAKULA UMO. TRA WANAKULA UMO. WAPIGA DEBE WANAKULA UMO. WAUZA SPEA FEKI WALA UMO. BIASHARA HII LAANA USIINGIE UTAFILISIKA
 
kama ngumu fanya kazi zingine... Kwanza madaladala binafsi yanasumbua sana. Na kuonea abiria mnafikiri serikali ingekuwa haipangi bei si mngewatoza wananchi ts elfu kumi hapa. Wewe kama mfanya biashara inabidi ujue demand and supply and the role of the government
 
Biashara zote ni akili yako kwani ukitegemea mboga hapo Bia hapo huwezi ona kitu ndio maana ukaitwa biHASARA
Hebu jaribu ulanguzi km madini haina leseni,Trafiki wala TRA faida capchap lkn hasara ya siku moja utajinyonga
 
Sijui utafiti wako umeufanyia wapi! Mi ni mmoja wa wadau wa usafiri Arusha na still huo mradi unalipa sana na ni njia mojawapo ya kusaidia wananchi coz dereva, kinda, tra, traffic, HALMASHAURI,wapiga debe, makampuni ya parking, Sumatra, mafundi makanika, wauza mafuta na spea wote hufaidika hapo... Turudi kwenye mada mfano Arusha USA river kwa siku hesabu ni elfu thelathini na tano kwa siku na full tank huku gharama zote zikiwa zimeshalipiwa service ni Mara moja kwa two weeks coz Ars USA ni km 21 wanapiga tripu kumi tu.. Ngaramtoni pia kuna lipa ila sio ka kwa mrombo nimeanza hii biashara 2008 na hiace super roof moja kwa Sasa Nina hiace super roof 4 na equity bank wamenikopesha Nissan qd "vipanki" viwili na ntalipa Hilo deni before deadline na Kununua vingine vya petrol kwa ajili ya route ya magugu Arusha Sasa wewe mtoa mada unasemaje. Biashara hailipi? Hiace kwa Arusha na Babati unalipa sema tu wewe hujajipanga
 
Nimeona wadau mbalimbali wakifanikiwa. Mimi nilijaribu hii biashara kwa muda wa miezi mitatu. Kisha nikaamua kuuza gari niliyokuwa nayo. Tatizo kubwa bila kukuficha ni wahudumu (dreva na konda). Ndani ya miezi hiyo mitatu nililazimika kubadili madereva mara tano!!! Tabia ya kubadili njia na kwenda vijijini gari inarudishwa mbovu. Na mimi pia sikuwa na muda mzuri wa kufuatilia. Lakini nasisitiza, ukiifanya kwa uangalifu biashara hii utafanikiwa. Gari muhimu kabisa ni mantanance, na usimamizi mzuri.

Ukiniuliza kama naweza ifanya tena hii biashara, YES. Lakini mimi sio mfano mzuri kwa vile sikukaa sana kwenye game.

8023944424_3418a32197_o.png
 
kwa hapa dar, SUMATRA wamesha award contracts kwa kampuni kubwa za usafiri kuendesha huduma za daladala kwa routes zote

habari ndiyo hiyo, utatakiwa ku-subcontract na wenye contract ili gari yako iingie kwenye route kwa masharti yao

mkuu tangulia sumatra wakupe yoote
 
wowAPTvh+SQA3J2AAAAAElFTkSuQmCC

Nyenyere, asante sana. Kwanza kwa kutufungulia mjadala na kutupa uzoefu wako. Na pili kwa kutoa maelezo yaliyonyooka badala ya maneno ya ushabiki.

Nina maswali machache tu ambayo ningependa unifafanulie. 1) Gari yako ilikuwa aina gani? 2) Mapato yake yalikuwaje? 3) Gari ilikuwa inafanya kazi mji upi/ njia gani? 4) Hawa wadau unaoona wakifanikiwa kwenye hii biashara, kuna mbinu zozote ambazo unaona wakizitumia kukabili changamoto ambazo ulizipata wewe? 5) Nimefurahi kusoma kwamba upo tayari kuifanya tena hii biashara. Kama ungeamua kuifanya tena, ni kipi ambacho ungefanya tofauti?
 
kwa hapa dar, SUMATRA wamesha award contracts kwa kampuni kubwa za usafiri kuendesha huduma za daladala kwa routes zote

habari ndiyo hiyo, utatakiwa ku-subcontract na wenye contract ili gari yako iingie kwenye route kwa masharti yao

mkuu tangulia sumatra wakupe yoote

Bluetooth, asante sana kwa taarifa hizi.
 
KUFANIKIWA KUNATEGEMEA SANA UBORA WA GARI NA USIMAMIZI

1. Gari ilikuwa Isuzu Journey Long

2. Niliweka hesabu ya chini kwa kulenga kumshawishi dereva atunze gari (70,000/= per day)

3. DSM Gongo la mboto - Temeke (Route fupi sana na bora kwa gari)

4. KUfanikiwa kunategemea sana ubora wa gari na usimamizi. Gari ikiwa imara utakwenda service mpaka service. Maana yake pesa utaiona. Na Kwa utaratibu niliokuwa nautumia, service ilikuwa ikifanyaka kila jumanne ya wiki ya pili. Tatizo ni pale dereva anapoanza tamaa na kupata route za kwenye barabara za vumbi.

Gari litaanza kula hela kwa matengenezo na utaichukia kazi. Pia kama ukianza na gari bovu utaapa kutogusa tena biashara ya daladala. Hao jamaa wengine sijaelewa wanatumia utaratibu upi kuhakikisha dereva habadili route, ila wengi nimegundua wanazingatia sana dereva mwaminifu. Ila kwa anayeendesha mwenyewe (mmiliki), huyo hamna shaka ana asilimia kubwa sana ya kufanikiwa (hata hesabu itakuwa kubwa).

5. Kitu ambacho nitafanya tofauti- gari lazima liwe kamili. Pia dereva lazima awe MZEE WA MAKAMO MWENYE FAMILIA. Yes, niko serious. Vijana wameniua. Watu wazima wanatend kuheshimu kazi zao na kujali familia zao. Vijana wengi wana ujanja ujanja ili ku-maximize profit. Wanajua ukimfukuza wewe atapata ajira sehemu nyingine. Pia kuwa na gereji yako ambapo utakuwa unatengeneza gari lako ni muhimu mno.

Awepo fundi maalum ambaye atakuwa kama personal na close associate, huyu atakutoa sana kwani hata likitokea tatizo kwenye gari wewe utapiga simu tu, naye atakwenda eneo la tukio kuicheki gari. Hii itaondoa ujanja ujanja wa madereva kusingizia magonjwa au kukuficha magonjwa yanayotokana na uzembe wao. Mfanye awe kama rafiki yako wa karibu utashukuru. Dereva akikutaarifu kwamba kuna ugonjwa, unamzuia kutengeneza unamwambia kuna fundi anakuja, wataogopa kiasi fulani. Hii niliifanya mwishoni kabisa, na huyu fundi ndiye akanishauri niiuze gari ninunue nyingine. Pia alinisaidia sana kwa mambo ambayo otherwise madereva wangeniliza.

Nadhani nimefunguka vya kutosha, karibuni kuchangia wakuu.
 
Mkuu,
1. Gari ilikuwa Isuzu Journey Long
2. Niliweka hesabu ya chini kwa kulenga kumshawishi dereva atunze gari (70,000/= per day)
3. DSM Gongo la mboto - Temeke (Route fupi sana na bora kwa gari).
4. KUfanikiwa kunategemea sana ubora wa gari na usimamizi. Gari ikiwa imara utakwenda service mpaka service. Maana yake pesa utaiona. Na Kwa utaratibu niliokuwa nautumia, service ilikuwa ikifanyaka kila jumanne ya wiki ya pili. Tatizo ni pale dereva anapoanza tamaa na kupata route za kwenye barabara za vumbi. Gari litaanza kula hela kwa matengenezo na utaichukia kazi. Pia kama ukianza na gari bovu utaapa kutogusa tena biashara ya daladala. Hao jamaa wengine sijaelewa wanatumia utaratibu upi kuhakikisha dereva habadili route, ila wengi nimegundua wanazingatia sana dereva mwaminifu. Ila kwa anayeendesha mwenyewe (mmiliki), huyo hamna shaka ana asilimia kubwa sana ya kufanikiwa (hata hesabu itakuwa kubwa).

5. Kitu ambacho nitafanya tofauti- gari lazima liwe kamili. Pia dereva lazima awe MZEE WA MAKAMO MWENYE FAMILIA. Yes, niko serious. Vijana wameniua. Watu wazima wanatend kuheshimu kazi zao na kujali familia zao. Vijana wengi wana ujanja ujanja ili ku-maximize profit. Wanajua ukimfukuza wewe atapata ajira sehemu nyingine. Pia kuwa na gereji yako ambapo utakuwa unatengeneza gari lako ni muhimu mno. Awepo fundi maalum ambaye atakuwa kama personal na close associate, huyu atakutoa sana kwani hata likitokea tatizo kwenye gari wewe utapiga simu tu, naye atakwenda eneo la tukio kuicheki gari. Hii itaondoa ujanja ujanja wa madereva kusingizia magonjwa au kukuficha magonjwa yanayotokana na uzembe wao. Mfanye awe kama rafiki yako wa karibu utashukuru. Dereva akikutaarifu kwamba kuna ugonjwa, unamzuia kutengeneza unamwambia kuna fundi anakuja, wataogopa kiasi fulani. Hii niliifanya mwishoni kabisa, na huyu fundi ndiye akanishauri niiuze gari ninunue nyingine. Pia alinisaidia sana kwa mambo ambayo otherwise madereva wangeniliza.

Nadhani nimefunguka vya kutosha, karibuni kuchangia wakuu.

Nyenyere, haya maelezo yako yatanisaidia sana katika kuendesha biashara hii na ninaamini kuwa wengine wengi watanufaika sana pia. Kwa muhtasari tu, mambo mawili muhimu ambayo nimeyaona ni 1) Uzima wa gari 2) Uaminifu wa dereva. La kwanza lipo ndani ya uwezo wetu. La pili ni mtu kutafuta namna ya kuweza kumpa "incentives" dereva ili awe muaminifu. Changamoto ipo hapo kwenye "incentives". Wachumi karibuni. Nyenyere asante sana.
 
kwa hapa dar, SUMATRA wamesha award contracts kwa kampuni kubwa za usafiri kuendesha huduma za daladala kwa routes zote<br>
<br>
habari ndiyo hiyo, utatakiwa ku-subcontract na wenye contract ili gari yako iingie kwenye route kwa masharti yao<br>
<br>
mkuu tangulia sumatra wakupe yoote
<br><br><font size="3"><strong>

Hapa ndo nimewaona SUMATRA wakifanya kazi, na mimi binafisi nawapongeza sana kwa hili, Jiji kama Dar haiwezekani liwe na Utitili wa wamiliki wa Dalada na pamoja na kuwa wengi hakuna Ufanisi, Majiji mengine makubwa hata kuliko Dar unakuta yana kampuni zisizo zidi 10 tu za kutoa huduma na wanatoa huduma yenye ubora wa hali ya juu kabisa, Dar wamiliki na Makonda wao wanacho jua ni pesa, babasi mabovu, wafanyakazi hawana lugha ya uteja.

Hapa ndo inabidi Watanzania tujifunze, mimi nashangaa sana pamoja na Miradi wa Mabasi yaendayo kasi pamoja na Tren bado watu wanakomaa na daladala moja, watu wanashindwa kuproject baadae itakuwaje, Watanzania walikuwa na Muda Mrefu sana wakujipanga kuja&nbsp;kucompete na haya Mabasi yaendayo kasi, lakini hakuna hata mmiliki mmoja mwenye hilo wazo watu wana angalia pesa kuliko kuangali feature ya hiyo biashara itakuwaje kwa miaka 10 hadi 30 ijayo

Na nina uhakika SUMATRA wanataka kuwapa tenda Makampuni ya Nje, na hii itakuwa safi sana ili watanzania tujifunze jinsi biashara zinavyo fanywa na si usanii

Mkuu samahani kama sijachangia kama unavyotaka wewe ndio mambo ya binaadamu,kwakifupi biashara ya usafirishaji(pikipiki,badaji,hiace,costa,marcopolo) zinalipa sana,changamoto ni dereva na konda wake ukiweza kuwadhibiti au kupata waaminifu basi umewin,pili ukianza bizness hyo inabidi uwe na mda wa kuzisimamia ili wasikuingiza king,na mie nipo kwenye mchakato wa kununua costa moja kuiweka barabarani sema mie mwenyewe ndio nitaisimamia.........

Nararaaaaaaaaaaaaaa! Nararaaaaaaaaaaa!!!!
 
Chasha, asante sana kwa mchango wako. Kwanza, ninatumai ya kwamba unajaribu kujibu kipengele cha "Mwisho ningependa wamiliki na wadau wengine watueleze wanauonaje muelekeo wa biashara hii kwa Dar, sasa ambapo DART ipo njiani" kilichopo kwenye uzi huu. Pili, ninaomba tuchangie uzi huu kwa uzoefu tulionao au kwa nukta ambazo tunaweza kuzilinda kwa hoja thabiti bila kutoka nje ya mada; tusiwe wahanga wa "subjectivity". Mfano wa "subjectivity" ni hayo maneno niliyoyaangaza kwa rangi nyekundu.

Ninafafanua:

Hapo kwenye kijani, ninatumai unafahamu ya kwamba si kila mtu anaweza kuwa na mabasi zaidi ya moja kwani si kila mtu anaweza kuchanga mtaji, si kila mtu anaweza kupata mkopo benki au kwa jamaa, na si kila mtu anaweza kuikuza biashara ya basi moja kufikia mabasi zaidi ya moja. Na kila mtu anahitaji fedha, hivyo watu wanalazimika kufanya kile kinachowezekana. Ninaamini ya kwamba ni watu wachache sana ambao watakataa kuikuza biashara kuongeza idadi ya mabasi yao pale wanapopewa nafasi ya kufanya hivyo na pale ambapo biashara inawaendea vizuri. Hivyo sidhani kama ni sahihi kulaumu watu kwa kuwa na basi moja tu iwe kwenye uzi huu au sehemu nyengine yeyote. Hasahasa kwenye uzi huu, kwani tunataka uwe "referencing source" ya wafanyabiashara wa sasa na wajao wa daladala na sio sehemu ya majungu.

Hapo kwenye nyekundu, tafadhali angalia kama kuna uwezekano wa kuthibitisha kauli hizo. Kama upo tuthibitishie. Kama haupo ninaomba wachangiaji wajao wachukue hili kama funzo la kutochangia kwa ushabiki. Watoe "facts". Asante sana Chasha.
 
Mkuu samahani kama sijachangia kama unavyotaka wewe ndio mambo ya binaadamu,kwakifupi biashara ya usafirishaji(pikipiki,badaji,hiace,costa,marcopolo) zinalipa sana,changamoto ni dereva na konda wake ukiweza kuwadhibiti au kupata waaminifu basi umewin,pili ukianza bizness hyo inabidi uwe na mda wa kuzisimamia ili wasikuingiza king,na mie nipo kwenye mchakato wa kununua costa moja kuiweka barabarani sema mie mwenyewe ndio nitaisimamia.........

Nararaaaaaaaaaaaaaa! Nararaaaaaaaaaaa!!!!

King Kong III, asante sana kwa mchango wako. Naona kwamba suala la dereva (na konda) bado linaendelea kuwa changamoto nambari moja. Nimefurahi kusoma ya kwamba kuna wadau wengine ambao wanataka kujikita kwenye biashara hii, ishara ya kwamba inalipa. Swali moja tu King Kong III: Unaposema ya kwamba una mpango wa kuisimamia mwenyewe una maana ya kwamba utakuwa dereva/konda mwenyewe au una usimamizi mwengine ambao ni "fail-safe" ?
 
Nyenyere, haya maelezo yako yatanisaidia sana katika kuendesha biashara hii na ninaamini kuwa wengine wengi watanufaika sana pia. Kwa muhtasari tu, mambo mawili muhimu ambayo nimeyaona ni 1) Uzima wa gari 2) Uaminifu wa dereva. La kwanza lipo ndani ya uwezo wetu. La pili ni mtu kutafuta namna ya kuweza kumpa "incentives" dereva ili awe muaminifu. Changamoto ipo hapo kwenye "incentives". Wachumi karibuni. Nyenyere asante sana.

Pia kumbuka kukata bima kubwa si unajua tena ndio unaingia kwenye game na ajali haina kinga mdau hivyo once lolote likitokea unakuwa compensated na si kuanguka kwa pressure, sio mtaalamu sana kwenye hii business ila mwanzo unatakiwa uifuatilie kwa karibu sana ikiwezekana hata siku moja moja unajifanya na wewe kuendesha kama leseni yako inakuruhusu ila kwa style ya nia njema sio ya kumfanya mpaka dereva akushitukie kwamba unamfuatilia (hawa staff wa daladala pamoja na kwamba wengi wanaonekana ni wahuni wakati mwingine inatakiwa style flani ya kuwa-handle)
 
Back
Top Bottom