Kama unaweza basi epuka kununua gari lililotumika hapa Tanzania, linakuwa limeshapigika sana.
Kingine, kati ya hayo magari uliyotaja, yote ni ya Kijapan na yana sifa za ubora, na spea zake zinapatikana. Ila kuna mengine yana reputation za "roho ya paka" kuliko nyingine (2L vs Hiace "mayai.") Lakini sasa roho za paka hizo unakuta ni matoleo ya zamani sana (2L engine, kwa mfano), unakuta ni bora Hiace "Mayai" ya mwaka 2005 kuliko "Roho ya Paka" ya mwaka 1988, itakusumbua.
Lakini Mkubwa, bila kuku discourage, is this the only business you could get in?
Biashara ya daladala imekaa kienyeji enyeji mno. Huna tight control na biashara yako, utunzaji na matumizi ya assets zako uko mikononi mwa ma strangers, when I say strangers I mean hata huyo dereva wako half of the times sio yeye anaeendesha! Na ndio industry standards, ukisema hutaki "day waka" aguse gari zako unakwenda against the grain of the business kwa saab gari inaamsha saa kumi na moja inazima saa mbili, tatu usiku, dereva mmoja kila siku hawezi! Una deal na mafundi wa miembeni unprofessional, untrustworthy, mpaka unajikuta umeshinda kwenye ma gereji unasimamia ufundi. Una deal na ma security wa kwenye ma gas station zinakolala gari kuwahonga honga all the time wasiibe site mirrors au wasifanye kufuru kubwa zaidi "change quarter" (kubadilisha hata engine zima na usijue)!
Lakini kikubwa kibaya kuliko vyote katika biashara ya magari kwangu mimi, siku kibasi kikipata ajali polisi wanakung'ang'ania wewe mmiliki eti ukawaonyeshe dereva alipo! Wait a minute now, dereva kaingia mitini, na mimi pia nilikutanishwa nae barabarani (hakuna dala dala yenye ofisi Tanzania!) tumekutana Mtanzania mwenzangu ana vibali, ana reference ya ajira za nyuma, nimempa ajira, mapicha na makaratasi yake haya hapa, si ndugu yangu, simjui Mama yake, sijui dini yake, kama ambavyo professional employees wa maofisini wanavyoajiriwa wakiwa ma strangers waliojibu matangazo magazetini, kwa vitambulisho vyao na certificate zao na references of the last jobs wanakabidhiwa mali za ofisi, sasa konda au suka ameharibu ameingia mitini nang'ang'aniwa mimi nikamlete, nimpate wapi kama nyinyi polisi mliobobea kutafuta fugitives hamumuwezi? You know? Such a shambolic, perilous, unprofessional business.