Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

...Asante sana Mkuu Mkeshaji. Je unaweza kuwa angalau na ka-Idea tu kuhusu Bei zake?
 
mkuu hayo mabus ya tata-marcopolo na skyline-eicher yamejadiliwa humu nadhani mwezi ulopita, tata walidai ni mil 70 na eicher inapungua kidogo bei. jaribu kupekua humu utaiona hiyo thread
 
Kuna taasisi moja ilinunua mabasi hayo mawili, yalikuwa yanaonekana kama mapya kwa nje viti vilikuwa na makaratasi yake kuonyesha kwamba ni mapya. Lakini baada ya mafundi kuzikagua zaidi waligundua kwamba engine zilikuwa used. Ni basi yasiyo na nguvu pia. Be careful enough if you want to purchase one
 
Tatizo kubwa watu wengi wananunua gari mbovu,utaona ata hapa JF mtu ana tsh 7ml anatafuta hiace super roof!!!pindi dereva atapoleta taarifa ya kwamba gari imeharibika anasema dereva mbaya/mwizi nk.
Kibiashara gari nzuri ni manual ambayo ni disel ambalo ni expensive kuliko petroli automatic,hiyo biz ni nzuri maana kila dakika watu utoka sehemu moja kwenda nyingine sasa kama una gari nzuri na msimamizi mzuri utaipenda..hesabu ya daladala kwa Kigamboni Dar ni 60,000/siku.Ukinunua gari nzuri ukalipia kila kitu ili dereva asipate mwanya wa kusema amekamatwa hana kibali cha sumatra au sababu nyingine yoyote faida ni kubwa kuliko hasara,hasara kama umenunua mbovumbovu maana kila siku ni spare na fundi.
 
Tatizo kubwa watu wengi wananunua gari mbovu,utaona ata hapa JF mtu ana tsh 7ml anatafuta hiace super roof!!!pindi dereva atapoleta taarifa ya kwamba gari imeharibika anasema dereva mbaya/mwizi nk.
Kibiashara gari nzuri ni manual ambayo ni disel ambalo ni expensive kuliko petroli automatic,hiyo biz ni nzuri maana kila dakika watu utoka sehemu moja kwenda nyingine sasa kama una gari nzuri na msimamizi mzuri utaipenda..hesabu ya daladala kwa Kigamboni Dar ni 60,000/siku.Ukinunua gari nzuri ukalipia kila kitu ili dereva asipate mwanya wa kusema amekamatwa hana kibali cha sumatra au sababu nyingine yoyote faida ni kubwa kuliko hasara,hasara kama umenunua mbovumbovu maana kila siku ni spare na fundi.

ushauri mzuri!
 
Wajanja na wanaofanikiwa na hii biashara wananunua gari ambalo halijafanya kazi huku yaani injini bado mpya haijafunguliwa (ndio kwanza limeagizwa).., wanalifanyia kazi likisharudisha pesa yake tu wanaliuza na kununua jingine. Hapo wanahakikisha gari haliwasumbui, (gari likishaanza matatizo linakuwa haliingizi tena bali linatumia tu..)
 
Hii biz haitabiriki mi nimenunua minibus nissan civilian toka jp nikampa Mzee mmoja niliyemuamini aniingizie mahesabu ya laki moja kwa siku. Kafanya kazi vizuri mwezi mmoja leo kanitumie taarifa eti gari imepata breakdown inahitaji sh milioni mbili kwa sasa niko confused.
 
Wajanja na wanaofanikiwa na hii biashara wananunua gari ambalo halijafanya kazi huku yaani injini bado mpya haijafunguliwa (ndio kwanza limeagizwa).., wanalifanyia kazi likisharudisha pesa yake tu wanaliuza na kununua jingine. Hapo wanahakikisha gari haliwasumbui, (gari likishaanza matatizo linakuwa haliingizi tena bali linatumia tu..)

Hii ni kweli kabisa,ndani ya mwaka faida inakuwa imerudi na unaliuza unanunua nyingine.
 
:welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome::welcome:
 
Wajanja na wanaofanikiwa na hii biashara wananunua gari ambalo halijafanya kazi huku yaani injini bado mpya haijafunguliwa (ndio kwanza limeagizwa).., wanalifanyia kazi likisharudisha pesa yake tu wanaliuza na kununua jingine. Hapo wanahakikisha gari haliwasumbui, (gari likishaanza matatizo linakuwa haliingizi tena bali linatumia tu..)
:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
biashara naomba muongozo kuhusu biashara ya daladala kwa mkoa wa iringa. Nina mtaji wa milioni kumi na moja, na daladala nayoihitaji ni hiace super roof.. Waungwana I need a potential.....
 
biashara naomba muongozo kuhusu biashara ya daladala kwa mkoa wa iringa. Nina mtaji wa milioni kumi na moja, na daladala nayoihitaji ni hiace super roof.. Waungwana I need a potential.....

Mkuu kuliko ununue Hice ya milioni kumi na moja bora ununue shamba tu,Hice nunua mpya (around 23 mln) itakulipa, ingawa sijui kuhusu Iringa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
duuuh, hata miili ya binadam haiko sawa jamani tunaumwa kila wakati lakini tunaishi, mkweche ukiwa road haina kwere pesa si inaingia bana.....
 
UELEWA WA KINA KUHUSU BIASHARA HII

Sorry wakuu kwa kuwaletea mada ambayo ni ya muda mrefu toka iandikwe but mimi nimeisoma leo na nimejifunza kitu nikaona ngoja niwaleetee wadau ambao hawakupata kuiona nao wajifunze jambo kidogo

Baada ya kununua basi dogo la kwanza (Hiace) na kulisajili kwa biashara ya kusafirisha abiria Mjini (daladala); nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto ziliponizidia niliaazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri. Nikamfuata mzee wangu mmoja hapa Mjini Iringa ambaye ameanza biashara ya kusafirisha mizigo na abiria tangu mwaka 1978.

Mzee wangu huyu baada ya kunisikiliza aliniambia sentensi moja tu na akasema huo ndio ushauri anaonipa na ambao utanisaidia. Alisema hivi, Kijana wangu! Ili umudu biashara ya magari hasa hizi daladala unatakiwa uwe mjeuri-jeuri kwa madereva, makondakta na wakati mwingine kwa matrafiki. Nikataka anipe ufafanuzi kuhusu hili ndipo akaongeza ufafanuzi huu, Hawa watu ninaokwambia usicheke nao ndio ambao wanaweza kukuliza ama kukufanya ufurahi. Ukizubaa katika hili usishangae kujikuta muda umepita, gari limechakaa na faedha za kununulia gari jingine huna.

Ushauri wa mzee wangu huyu niliufanyia kazi na ulizaa matunda (kwangu) Uzoefu wangu katika biashara hii ya daladala unachagizwa pia na nafasi ya uongozi niliyoapata kushika kuanzia mwaka 2009 hadi januari 2012. Nilikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa mabasi ya abiria mkoani Iringa kinachojumuisha magari yote ya abiria ukiacha mabasi ya mikoani. Nafasi hii ilinipa kufahamiana na kushirikiana na wafanyabiashara wengi wa magari ya abiria Iringa. Hivyo nafahamu chungu na tamu za biashara ya daladala na machozi yao nayajua.

Ukiacha changamoto ya faida (ambayo nitaichambua kwa kina kwenye makala hii) biashara ya daladala ina timbwili-timbwili si mchezo. Madereva wanasumbua sana, faini za barabarani zisizoisha na uharibifu wa magari ni kama chachandu chungu kwenye biashara hii.

Kati ya biashara nilizowahi kuzifanya biashara ya daladala inaongoza kwa kupasua kichwa Miezi machache iliyopita wamiliki wa daladala-Dar es Salaam waliwasilisha kusudio la kupandisha nauli za daladala kwa asilimia mia tatu (300%) mbele ya baraza la watumiaji wa huduma za usafiri.

Baraza hilo pamoja na SUMATRA waliwagomea wamiliki wa daladala kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu hizo ni pamoja na Mosi; wamiliki wa daladala walishindwa kuwasilisha taarifa za kifedha za biashara zao.(Approved financial statements) Pili sababu walizozitoa kuhusu kupanda gharama walidai (exagrated) zilikuzwa mno na kukosa ushahidi wa bei katika soko. Baada ya kufuatilia mnyukano ule niliwahurumia sana wamiliki wa daladala kwa sababu wenye rungu la kuwasaidia hawajui viatu vya umiliki wa daladala vinavyobana na kuumiza.

Nimetafiti biashara hii katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Dodoma huku Iringa nikiwa nimeifanya kwa vitendo. Sehemu karibu zote changamoto zinafafanana ingawa kuna tofauti ndogo ndogo kutegemea na tamaduni za kimaeneo. Sehemu hizi zote viwango vya fedha inayolazwa ni shilingi kati ya elfu thelethini (30,000) na elfu arobaini (40,000) kwa siku kwa mabasi madogo (Hiace Super Roof). Kwa mabasi ya kati (Coaster) kiwango kwa siku ni kati ya elfu hamsini (50,000) hadi elfu themanini (80,000) kwa siku. Sasa twende kimizania ya uhasibu hapa.

Bei ya kununua basi dogo (Toyota Hiace Super Roof) pamoja na kusajili leseni, njia, na taratibu zote ili ianze biashara ni kati ya shilingi milioni ishirini hadi milioni ishirini na tano (20M-25M). Bei ya kununua basi la kati (Coaster) ni kati ya milioni thelathini na tano hadi milioni arobaini na tano (35-45). Magari hayo yote ni yale yaliyotumika kule Japan (Used Cars) Tukokotoe mahesabu ya basi dogo.

Kwa upande wa mapato kama gari inalaza shilingi elfu 30 kwa siku ina maana kwa mwezi unakusanya shilingi 840,000 (laki nane na arobaini elfu). Hesabu hizi ni kwa siku ishirini na nane. Siku mbili kikawaida hutengwa kwa ajili ya kufanya service ya gari ambayo ina fanyika kwa mwezi mara mbili kila baada ya siku 14.

Tushuke kwenye matumizi. Galoni moja la kilainishi kizuri(oil) ni shilingi elfu 45, gharama ya kubadilisha sahani za breki ni shilingi 25, vifaa ambatanishi vya service ni karibu shilingi 20. Ukichanganya na ufundi na ikiwa unafanya service ya uhakika katika gari lako kila service moja unatumia shilingi laki moja kwa kadirio la chini.

Katika kipengele cha service kwa mwezi unatumia kama laki mbili. Mshahara wa dereva kwa mujibu wa sheria za SUMATRA zinazoambatana na masharti ya kupewa leseni yanakutaka mmiliki wa gari ulipe kuanzia kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi shilingi elfu themanini. Kodi za serikali ikiwemo leseni ya barabara, leseni ya njia, zima moto, mapato na ushuru wa manispaa/jiji ni wastani wa shilingi elfu sitini kadirio la chini.


Nyingi ya kodi hizi zinalipwa kwa mwaka lakini hapa nimezigawanya katika mafungu ya miezi 12. Mwisho tujumlishe mshahara wa wewe Mjasiriamali unayemiliki gari. Najua wajasiriamali wengi hawana utaratibu wa kutenga mishahara yao kwa biashara zao, lakini hata kama hutengi mshahara tukadirie kuwa unajilipa shilingi elfu themanini tu kwa mwezi.

Sasa ukichukua mishahara ukajumlisha na kodi ukajumlisha na gaharama za matengenezo (service) unapata matumizi ya shilingi laki nne na ishirini elfu (420,000). Kiharaka haraka unaweza ukadhani faida inayobaki ni shilingi laki nne na ishirini (420,000).

Hapa ndipo wafanyabiashara wengi wa magari ambapo hufilisikia kwa kusahau jambo la muhimu kuliko yote. Jambo hili la muhimu ni gharama ya uchakavu wa gari (depreciation cost). Gharama hii kitaalamu hutakiwa kujumuishwa kwenye kipengele cha matumizi.

Tunaposema gharama ya uchakavu ni pale unapoelewa kuwa ikiwa gari inatembea basi tairi zinazidi kuisha, vyuma vinasagika na bodi linachakaa. Kinachoamua kiwango cha gharama ya uchakavu ni makadirio ya muda ambao gari lako litakaa kabla ya kuchakaa kabisa. Kuna njia kadhaa za kitaalamu lakini hapa nataka nitumie njia rahisi ya kijasiriamali ili tuelewe vema.

Mathalani kama gari yako inapita kwenye barabara nzuri unaweza kukadiria kuwa uhai wa gari lako utakuwa ni miaka mitano. Unachofanya unachukua thamani ya kununulia hadi kusajili gari ianze biashara kisha unagawanya kwa miaka mitano. Twende pole pole hapa.

Tumesema wastani wa chini wa basi dogo ni shilingi milioni 20 hadi ianze biashara. Ukichukua milioni 20 ukagawanya kwa miaka mitano unapata shilingi milionI 4 ambayo ndio gharama ya uchakavu kwa mwaka. Sasa chukua milioni hii 4 kisha gawanya kwa miezi kumi na mbili unapata wastani wa shilingi 333,000 (laki tatu na thelathini na tatu elfu). Hii fedha tunaiingiza kwenye sehemu ya matumizi.

Kwa maana hiyo jumla kuu ya matumizi yetu kwa mwezi inakuwa ni shilingi 753,000/=(laki saba na hamsini na tatu elfu). Ili uelewe faida HALISI unayozalisha kwa mwezi chukua mapato ya mwezi (840,000) kisha utoe na matumizi ya mwezi (753,000). Ukikokotoa hapo utaona faida HALISI ya biashara ya daladala ikiwa una basi dogo kwa mwezi ni shilingi elfu themanini na saba (87,000/=) tu! Najua mahesabu haya yatawastua wengi na wengi wanaweza wasiyaelewe na kwa kutoyaelewa wanaweza wasiyakubali. Bahati nzuri ni kuwa nimeshafanya biashara hii huku nikiwa na digrii ya biashara kutoka chuo kikuu hivyo naelewa ninachokisema hapa. Labda nitafsiri maana ya mahesabu hayo hapo juu kwa lugha nyepesi na ya picha.

Iko hivi; ukinunua gari la milioni 20 leo, baada ya miaka 5 linaweza kuwa limeshachakaa kabisa. Wakati huo gari litakapochakaa unatakiwa uwe na fedha mkononi za kununua gari jingine kutoka katika biashara hiyo hiyo na ubakiwe na fedha nyingine ambayo ndiyo tutaiita FAIDA. Ile hela utakayorudishia gari lililochakaa ni mtaji ulioanza nao. Kwa mahesabu hayo hapo juu ambapo tumeona faida HALISI ya daladala ikiwa unamiliki Hiace Super Roof ni shilingi elfu themanini na saba kwa mwezi.

Kwa faida hiyo (@87,000/=) itakuchukua Mjasiriamali miaka 19 ili afanikiwe kununua gari jingine la pili! Mliowahi kufanya biashara ya daladala mtakubaliana nami kuwa; ukiona mtu ameongeza daladala ya pili ndani ya mwaka mmoja ama miwili basi uwe na uhakika kuwa fedha ya kununulia gari ya pili hajaitoa kwenye gari ya kwanza kwa asilimia mia moja.

Ni ama amechukua mkopo au fedha ameongezea kutoka vyanzo vingine. Naomba nieleweke vema hapa. Sisemi kuwa biashara ya daladala hailipi, la hasha! Lakini faida HALISI iliyopo kwenye daladala ipo tofauti sana na vile SUMATRA na abiria wanavyoitazama ama kuifikiria.

Mtazamo na mawazo ya wadau hawa ndio yamekuwa yakisababisha kuwakatalia wenye daladala ama kuwakubalia kwa mbinde kila wanapotaka kuidhinishiwa kupanda kwa nauli. Mathalani, kilainishi (oil) ambacho mwaka 2006 kilikuwa kikiuzwa shilingi 19,000/= leo kinauzwa 45,000/=. Tairi ambalo wakati huo liliuzwa kwa shilingi 85,000/= leo linauzwa 165,000/=. Gari lililokuwa linauzwa milioni 12M mwaka 2006 leo linauzwa milioni 22M (Toyota Hiace Super Roof).

Kwa mabadiliko hayo nauli za daladala zilitakiwa zipande kwa asilimia 236% kutoka mwaka 2006 hadi leo. Lakini hali ni kinyume, kwani maeneo mengi nauli ya daladala imeongezeka kwa kati ya shilingi 50 hadi 100 ongezeko la kati ya asilimia 25% hadi 50% tu.

Ndio maana SUMATRA na baraza la watumiaji walipowagaragaza wamiliki wa daladala kwa kufutilia mbali madai yao ya kupandisha nauli, nilijichekea na kusikitika tu. Hata hivyo sina neno na wala sina lawama kwa SUMATRA wala baraza la watumiaji; kwa sababu wenye daladala wenyewe walishindwa kujitetea utetezi wenye nguvu za hoja.

S
ource: suleimanmagoma.blogspot.com
 
Asante kwa maelezo yako marefu ambayo kwa kiasi fulani umeonesha ukweli halisi ulivyo kwenye biashara hii ya usafiri
Pamoja na pongezi zangu kwako naomba nikushauri kwamba itakuwa vizuri kama utakutana na wadau wenzio katika biashara hii ili muweze kuandaa taarifa hii kiufasaha kabisa mkielezea michanganuo yote ya gharama za uendeshaji biashara hii ili taarifa hii ipelekwe kwa wahusika waweze kutoa maamuzi ambayo yataleta tija kwenu.

Kimsingi sekta binafsi ikikua tunaamini itatoa suluhu ya tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu na hii si kwa upande huo tu wa biashara uliyoizungumzia hata pia kwenye sekta zote zinazotoa fulsa za kiuchumi kwa nchi yetu.

Tatizo letu kama Watanzania ni watu kama wewe ambao licha ya kuwa na elimu nzuri namna hii ya biashara bado tunashindwa kusaidiana sisi kwa sisi ili tuweze kuwaamsha hata wale ambao labda kwa upeo wao mdogo kielimu bado wameendelea kuishi kwa mazoea.Na katika hili ndio maana tumejikuta ni watu wa kuingia na kutoka.

Nitakupa mfano
Hebu fikiria makampuni makubwa ya usafiri unayoyajua ambayo tokea ukiwa mtoto mdogo uliyaona yakiwa yamewekeza kwenye biashara hii ya usafiri. Je leo hii yako wapi? Kama kweli watu/makampuni haya yangekuwa ni yenye kufanya biashara kwa weledi wa nidhamu ya biashara yenyewe ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali juu ya nini kifanyike ili kukuza sekta hii binafsi ikue unadhani mpaka kufika leo Tanzania yetu ingekuwa wapi kiuchumi?

Naomba kila mmoja kwa nafasi aliyonayo asimame na apaze sauti kwa kuchangia ufahamu wake kwa wengine ili siku moja nchi yetu tuwe na uchumi wa mfano duniani
 
hakika umenena vema, nimekulia kwenye mazingira ya ndugu aliyekuwa na hadi sasa anafanya biashara za daladala, changamoto ni nyingi ila zinalipa, na ukizoea hiyo biashara huwezi kuacha, nami najikongoja nitafute yangu, ndugu zangu wengi wanafanya hii biashara kwa mwanza daladala zinakabithi 50, 55 na 60 kwa siku.
 
Back
Top Bottom