newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,385
- 568
asante mkuu,hili la kuweka record sheet,ntalifanyia kazi,
Pole sana ila zingatia ushauri huu: Kwanza kabisa hakikisha magari yako wakati wote ni mazima na hayana hitilafu yeyote inayoweza kuyafanya yasimame. Pili hakikisha kila siku unasoma millage kabla gari halijaanza safari na mara limalizapo safari zake. Tatu hakikisha madereva unaowakabidhi g magari yako wana lesseni halali za udereva na hakikisha unawafahamu vizuri, makazi yao, wadhamini na viongozi wao wa serikali za mitaa wanayoishi na ikiwezekana wawe na wadhamini wakuaminika. Hakikisha kuwa kila wakimaliza kazi jioni/usiku, unapima (mwenyewe kiasi cha mafuta kilichobaki na kuongeza hadi kiasi ambacho unajua kitatosha kwa kazi ya kesho) awali nilikueleza kuwa hakikisha kuwa unarekodi millage ili kujua ni umbalii gani kwa siku gari yako inasafiri, hii itakusaidia kujua wastani wa mafuta yanayohitajika kwa siku. Kwa nchi kama kenya madereva hupewa sheet maalumu ambayo hurikodi mlolongo mzima wa safari na gharama zote ambazo dereva atakuwa ametumia
kwamfano:
Ubungo - posta -abiria 24 @ sh 300 =7200/= km 9
posta -Ubungo- abiria 30@ sh 300=9000/= km 9 n.k
aidha unatakiwa kuwa na mkaguzi (maneger) wa kuaminika ambaye kwa nyakati tofauti atakuwa anafuatilia nyendo za gari lako na kuhakikisha kuwa madereva wakati wote wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa. Gari inapoharibika hakikisha unafika wewe mwenyewe/msimamizi wako na kuhakikisha gari linapelekwa kutengenezwa kwenya gereji zinazoaminika. Hakikisha gari lako umelipa kodi zote kuepuka usumbufu wa kukamatwa na askari na kusababisha upotevu wa mapato. haya ni machache tu ila biashara ya daladala inahitaji usimamizi wa karibu na umakini mkubwa pia hakikisha dereva, fundi na kondakta wako unawapa vivutio na mikataba inayoeleweka ili waifanye kazi yao kwa bidii na uaminifu.