Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake


Mawazo sahh kwa mda sahh yafaa nikazichange kwa Mara ya mwsho afu nianze mipango upya
 
Sikubaliani na Mtoto tajiri, hii njia anayoisema ni ngumu sana, tena utajuta. Kabla siajaanza kununua used kutoka Japan nilikuwa nafanya hivyo. Tofauti ni kubwa mno kwenye uendeshaji. Asikuambie mtu,gari hasa daladala ni zaidi ya injini. Wewe jipange nunua gari ambayo mafundi wetu hapa nyumbani hawajaigusa sana au used Japan. Zaidi ya hapo utanufaisha, dereva, konda, fundi na wauza spea na wewe hautapata kitu.
 
jaman mm nataka ushauri kuhusu magar aina ya eicher na tata, jinsi ya kuyahandle ndugu Zanzibar vp hapo una mchango wwte
 

Labda ungeweka mchanganuo kwamba ni usumbufu gani uliopata wakati ulipokuwa anafanya hivyo then tuone kama kuna ukweli wowote
 
jaman mm nataka ushauri kuhusu magar aina ya eicher na tata, jinsi ya kuyahandle ndugu Zanzibar vp hapo una mchango wwte
Legend,kuna uzi ulichambua magari hayo kwa kina sana,we search utaukuta umechambuliwa kitaalam.
Ila kura nyingi kwenye uzi huo zilienda kwa TATA
 
Wadau,

Nataka nifanye biashara ya Usafiri hapa mjini, mwenye uzoefu anipe maujanja itani cost how much ili niweze kupata two used Costa kwa ajili ya kuanza biashara. Pia naomba unipe Overview Costa moja inarudisha bei gani kwa siku na nini matatizo yake hii biashara.
 

Kwanza kabisa naanza kwa kukaribisha sana ktk biashara hii na pia kukuondolea ile roho ya uoga ya kusema biashara ya usafiri ni pasua kichwa!any way bila kupoteza muda naanza na hiki kijiswali Je unayajua magari japo kwa kifupi au ndio kwanza unataka uingie kwenye magari?
 

Mkuu vipi ulifanikiwa kupata coaster? Hebu naomba unipe Changamoto na faida zake maana mm nataka niingie kwny hii biashara ya daladala
 

aha we xio ramazan mxofe "ms"
 
tatizo kubwa ni usimamizi, we piga hesabu gari yako kama inalaza 50000 kwa siku itakurudishia faida baada ya muda gani, kama ni miaka miwili mkabidhi dereva mwambie kila siku niletee 50000 service juu yangu habari ya traffic au majembe hainihusu baada ya miaka miwili gari itakuwa ya kwako hapo lazima gari itatunzwa na pia hesabu zako zitakuja kama zilivyo wamiliki wengi wanapigwa bao na madereva sababu hawana malengo ya biashara
 
AISEE MKUU UMENISHANGAZA SANA. YAANI UMENUNUA GARI MBILI HALAFU NDIO UNATAFITI UIMARA WAKE. KATIKA MAKAMANDA NA WEWE UMO.
 


Katika biashara ni hatari sana kuwekeza kwenye mradi mmoja (Concentration Risk) kwani ukipata hasara basi umepoteza kila kitu. Ni muhimu sana kupanga kuyaweka mayai yako kwenye makapu tofauti ili kapu moja likioza kwa sababu yai moja limeoza ndani ya kapu hilo basi makapu mengine yasalimike na hivyo kukuwezesha kuendelea na biashara yako (Diversification).


Ili kufanya diversification yenye tija basi hakikisha miradi unayotaka kuifanya in risk profiles ambazo hazishabihiani kabisa kwa maana kwamba kama vyanzo vya hasara vikitokea kwenye biashara moja basi vyanzo hivyo ni vyanzo vya faida kwenye biashara nyingine. Kwa mfano kama unataka kufanya biashara ya kuuza mablanketi basi fikiria kufanya na biashara ya kuuza barafu pia kwa sababu kama hakuna baridi basi mablanketi hayatauzika lakini barafu zitauzika kutokana na watu kutumia sana vitu vya baridi wakati wa joto hivyo hasara utakayoipata kwenye uuzaji duni wa mablanketi itafidiwa na faida utakayoipata kwenye uuzaji mwingi wa barafu.

Kama unafikiria diversification basi ushauri wangu ni kufikiria mradi wa Rifaro kwani vyanzo vyake vya hasara (Risk Profile) vinatofautiana sana na biashara za kawaida tulizozizoea na hivyo itakusaidia ku diversify risk ya kuwekeza kwenye miradi ambayo ina risks zinazoshabihiana.

Toa TZS 128,500 tu kwenye hizo hela zako uwekeze kwenye mradi wa Rifaro zilizobaki wekeza kwenye mradi utakaoamua kuufanya.

Kwa maelezo ya kina kwa nini uwekeze kwenye mradi wa Rifaro soma thread hii hapa

Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?
 
Biashara ya usafirishaji ni ngumu sana.,usipoielewa na ukaingia kichwa kichwa..,
Vitu vilivyowafanya watu weng kukwama katika hii biashara ni
1. Dereva makini
2.usimamizi wako katika gari lako
3. Services
4. Kula yako na maisha yako kutegemea kipande cha siku....
Niliiogopa sana hii biashara but namshukuru mungu nilikwenda Zanzibar nikapata Nissan Carvan used safi.,nikaiweka barabara leo ni mwaka wa 3.,cjagusa engine wala gear box,wala diff,na imeshanipa gari nyingine Nissan carvan ya pili na najiandaa kutoa ya 3 mwezi may mwaka huu 2016.
 
Hongera sana mkuu, unaweza ku share nasi jinsi ulivyoweza kuisimamia biashara yako vizuri hadi mpaka sasa inakuwezesha kupata gari ya tatu. Pia naomba kujua Zanzibar unanua sh ngapi, gharama zote hadi inaingia barabarani kuanza kazi ina range kwenye sh ngapi na pia kwa siku dereva analeta sh ngapia. Pole kwa maswali mengimkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…