Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Biashara ya daladala ni usimamizi ukiwa na usimamizi mbovu huwez hiyo biashara, mimi imenishinda nimepaki DCM karibu miezi 6 na hiv sasa liko sokon
Leta helaniuzie
Leta hela
Mkuu tuanzie kwenye uhai wa chombo chenyewe je nimashine nzima!? Siyo spana mkononi!Reffering to the bolded part above, inatia uchungu sana hasa nikikumbuka wakati nilioupitia kuzichanga kwa ajili ya hiyo project! These madereva are indeed "heart-less"! Hii ni wiki ya tatu nimeiweka Yard. Najua napata hasara kwa kuiweka yard, but I still consider it as the best thing to do at the moment... At least I have peace of mind. Kila ilipopigwa simu hata kabla sijajua ni nani moyo ulikuwa kama unataka kupasuka...
Wazo la kujenga nyumba kwa ajili ya biashara naliona kama bado ni over-size kwa sasa, hasa ukichukulia ukweli kuwa hata kibanda changu cha kuishi bado kinanipa mtihani wa finishing. Nashukuru kwa ushauri na kwa ku-share experience yako kuhusu biashara ya daladala.
Au ukanunue shares Kwenye kampuni inayoeleweka.Aisee ukimwambia mtu yeyote anayefanya kazi maofisini akanunue guta atakushangaa sana! Lakini ukiangalia it really make sense.
Hizi biashara za magari ni nuksi sana aisee. hasa kama na wewe tajiri hujui spea za magari. yaani utafilisika.
nakumbuka yalinikumba haya haya ya mkuu hapo juu. nilinunua Hiace 14m baada ya miezi miwili niliuza 8m huku nikiwa nimeshaingia gharama zaidi ya 1.5m. its better ukajenga nyumba kama una mtaji
mkuu, usiogope hakuna , hakuna biashara rahisi, wala kazi rahisi.Mimi binafsi napenda biashara ya Daladala lakini changamoto ninazozipata ni kama ifuatavyo - (1)Kulipa rushwa- mimi magari yangu hayatoi rushwa kwa namna yoyote hile - Msimamo huu umeleta uhasama mkubwa sana kati yangu na Polisi.(2) kutokuwa na business stability - kwamba kuna mambo kama polisi wanapoteza muda sana- kwenye biashara yangu napoteza at least siku mbili kwa wiki za hesabu - polisi kaamua tu kukupiga faini kutokana na sababu namba moja (3) Kuna baadhi ya ruote, wamiliki wezangu wa mabasi hawataki gari zangu ziende zifanye biashara kwenye hiyo route (Mbaya zaidi aliyekuwa anaendesha kampeni hiyo ) ni Polisi traffic (ambaye nae ni mmiliki wa daladala).(4) Spare part-hii imekuwa changamoto kubwa sana (5) Mafundi-hawa sasa kila mmoja anajua jinsi ilivyokuwa shida.
weka bei mkuuLeta hela
7,000,000/=weka bei mkuu
uko pande za wapi mkuu7,000,000/=
Duh, hii ngumu kumeza asee..Nashukuru kwa mchango wa mawazo!
Original Pastor, hilo la kumweka ndugu kama konda nimelifanya japo sikumtoa kijijini. Kilichotokea ni kuwa mheshimiwa alitafuta dereva kweli lakini hakuishia hapo aliweka na konda pia! Kila wakati yeye yupo chini ya mti akisubiri aletewe hesabu ya kila trip wanayofanya. Hesabu ndo ilikuwa mbovu zaidi kwa sababu kwanza watu wa kugawana waliongezeka maana ni makonda wawili (Mmoja akiwa bosi-mtoto) Pili nilikuwa na wakati mgumu kumbana kwa kuwa ni ndugu...
Hebu sikilizeni nyie, achenaneni na hyo mambo yanapoteza mda wenu bureee! Karibuni kwenye ulimwengu wa FOREX, unalamba hadi 2millions in 30 seconds, hahahaa! Najua mtashangaa ila ukweli ndo huo..
Lakin hilo nalo ndilo tatiz kubwaNilipopata vicent nilishauriwa kuchukua daladala (Hiace) ili ifanye kazi kigamboni. kupitia JF nilifaninikiwa kuipata. Lakini kilichofuata hapo ni sawa na ndoto ya kutisha!... ukiamka hutamani usinzie tena.
Leo dereva anakwambia center-ruber imeisha, kwa hiyo badala ya Tsh 40,000 unapata 15.Kesho asbh ndo kwanza unaingia ofisini anakwambia timing belt imekatika...inatumika pesa ya jana na haitoshi inabidi utoe yako mfukoni.
Siku ya tatu na ya nne akikuhurumia ukakusanya 80 basi siku inayofuata unaambiwa nimepigwa bao na majembe. Ilikuwa nilipe 250,000 so nimewapoza 35,000. so hesabu yako mkuu hii hapa elfu tano! Gosh!!!
Picha hizo zimeendelea mpaka nikatia shaka, akipiga dereva wkt mwingine nachomoka kuthibitisha tatizo. Ajabu! Mara kadhaa ni uongo kunakuwa hakuna cha majembe wala mashoka! Bse of that nimewatimua kila nikigundua usanii huo, ndani ya mwezi 1 madereva wanne! Sasa naanza kuhisi kuwa they are probably all the same!! Na inanipunguzia concetration yangu kazini.
Baadhi ya watu wanasema ningeweza kuitumia vizuri kama nikitafuta tenda ya kubeba watoto (Nursery) na kuwa hiyo haina longolongo nyingi. Naomba ushauri wenu wakuu! Pse, pse!!