Biashara ya dhahabu kwa mtaji wa 25M

Biashara ya dhahabu kwa mtaji wa 25M

Ukiingia kwenye hii sector , uwe na moyo mgumu na maamuzi magumu
 
What if!
Nikiwa na shimo langu, mchimbaji akaingia kuchimba tukagawana mifuko.

Na mchimbaji aliechimba akajakusaga kwenye mashine yangu pia!!

Nikatunza lundo langu kwa 5-6months

Nikaingiza plant?

Hapo sipati kitu?
Hiyo ya kuchimba ndo unafilisika huku unaona, wale wachimbaji huwa wanajali uwalishe tu we wanakupa moyo kuwa wameuona mkanda wa dhahabu hauko mbali kumbe wanakudanganya utawalisha na kuingia hasara saa hiyo kila baada ya mita kadhaa inabidi ufunge zile box za timba mti mmoja unauzwa hadi 20k kufunga box 1 tu unatumia hadi 300k+

Alafu inatakiwa usimamie masaa 24 kama una familia inabidi wakusahau hakuna kurudi nyumbani ukiwapa nafasi tu wachimbaji wanakuibia
 
Hiyo ya kuchimba ndo unafilisika huku unaona, wale wachimbaji huwa wanajali uwalishe tu we wanakupa moyo kuwa wameuona mkanda wa dhahabu hauko mbali kumbe wanakudanganya utawalisha na kuingia hasara saa hiyo kila baada ya mita kadhaa inabidi ufunge zile box za timba mti mmoja unauzwa hadi 20k kufunga box 1 tu unatumia hadi 300k+

Alafu inatakiwa usimamie masaa 24 kama una familia inabidi wakusahau ukiwapa nafasi tu wanakuibia

Kwahivyo njia ipi nzuri kupata mawe mazuri kwenye karasha lako?
 
Kabla ya kuanza kununua mawe ijue kwanza miamba mana unawezanunua kiroba ata m.1.ukaenda kusaga ukapata grm 5
 
Kwahivyo njia ipi nzuri kupata mawe mazuri kwenye karasha lako?
Biashara ya madini ni ngum sana wale wa karasha maeneo mengine hawalipwi wanasaga bure wanachonufaika ni kubaki na ile vumbi ya marudio ambayo nayo kuiozesha na kupata dhahabu inabidi uipeleke plant, kukodisha plant kwa mwezi siyo chini ya million 2 sehem nyingine 3m alafu walinzi inabidi uwaweke we mwenyewe na uwalipe nje na gharama ya kukodisha plant

Kuna hatari ya kuibiwa carbon pia wafanya biashara wa dhahabu wengi wana magenge ya waizi wakijua huna uzoefu wanakuja kuiba wale walinzi wako uliowaweka pia sometimes siyo waaminifu wanaweza kukuibia mzigo ukiiva.

Inahitaji uzoefu hiyo biashara na kwa mtaji wa 25m ni ngumu sana kukamilisha gharama za huo mzunguko labda uwe unauza udongo wa marudio kwa matajiri we kazi yako iwe ni kusaga tu, sasa muda wa kusubiri hadi rundo ikamilike inabidi uwe na biashara nyingine ya kukuingizia kipato maana huingizi hela
 
Biashara ya dhahabu naifananisha na forex. Kutajirika na kupotea ni kugusa tu.... Kama ni kuhusu kukusanya marudio m25 haitoshi na utaingia kwenye madeni yasiyo ya lazima.....

Kuna mdau katoa ushauri WA kutoa huduma nadhani tengeneza kibanda movable tembelea kwenye milipuko ya MADINI (rush) kuwa updated Sanaa kutajua maeneo maji tu yanaweza kukupa faida kubwa sanaa
 
Kwa kuwekeza kwenye biashara husika (dhahabu) kwa kununua marudio shingapi inatosha kuanzia?
 
Maangalizo yote anayopewa mwamba akiyazingatia atatoboa, akipuuza moja tu, atarudi hapa akilia kilio cha mbwa koko, mkuu japo una abc za dhahabu ila nakushauri usiingie mazima, hakunaga undugu kwenye dhahabu, nenda kwa hao ndugu zako ila usiwaambie una hyo 25m, kaa nao at leas 6mnth, utakuwa umejifunza mengi sana kuhusu biashara ya dhahabu, hz mambo nazijua sana, huwezi nidanganya ktu kwenye dhahabu ila siwezi mshauri mtu aingie kichwakichwa, hyo 25m inaweza kukubadilisha jina ukaitwa milionea ila inawezwa fyekwa kwa miezi kadhaa tu ukarudi home unaongea peke yako.
 
Kwa kuwekeza kwenye biashara husika (dhahabu) kwa kununua marudio shingapi inatosha kuanzia?
Sawa hata hiyo inatosha ila risk ni kubwa mno... Dhahabu ni mchakato WA muda mrefu (hasa WA marudio)...... Kwa mtaji wako itakulazimu kuchukua PPM ndogo na kumbuka wajanja ni wengi mno Kwa hii business kuegeshewa mzigo ni kugusa so kusema shngapi hasa ni itategemea ila to me at least 150 inakupa uhakika WA kurekebisha makosa kiasi ila 25 kosa dogo umeenda na maji.

Na usilogwe ukaanzisha duara au kuingiza ubia (share) kichwa kichwa.

Au laa chukua ushauri WA udalali japo unapingwa na serikali.

Katika udalali unaweza ukatenga nusu ya hiyo fedha ukatafuta dealers WA kufanya nao KAZI katika masoko then nenda kashawish wateja katika elations au mialo.... Hapa mteja utampa bei ndogo kiasi then boss wako (dealer) akupe bei nzuri.
Mfano. Umepata mteja mwenye gram 150 wewe ukampa bei ya 147,550/g then dealer ukakubaliana nae 148,300/g kinachopatikana ndo chako.

Note madalali wengi hawana mitaji wao ni mtu kati tu.

Udalali ni risk pia unaweza tengenezewa zengwe la utoroshaji kuchomoka humo utaomba poo ila vijana ndo wanaishi humo, na kuendesha familia zao.

Wajuvi watasahihisha nilipokosea.
 
Kabla ya kujingiza kwenye hiyo biashar.kwanza Uijue.zunguka kwenye machimbo ya dhahab uifaham na ujenge uzoefu pia.yan hiyo m 25.kuichoma ni ,madakika.so mkuu fanya utafit wa kinadharia kwanza pasipo kitumia kias kikubwa cha hela..angalizo faida ni kidgo sana sio kama inavyoaminishwa.na ili upate faida kubwa itakulazm uwe mafia
Hii biashara mkuu acha kabisa. Tuliingia huko hukp chinya na jamaa yangu. Mwanzo ilitulipa tukaona tulikuwa wapi mbona tulichelewa. Ila kibao kilipogeuka, yan tulichoma mtaji tukabaki na mils 8 tu kaamua tuigawane kila mtu aende akajipange upya.
Mwenzangu akahamia chimbo jingine na akaongeza mtaji. Mwanzo mambo yakaenda poa sana.
Ila baadaye akaanza akipima anaona PPM ni kubwa ananunua anakusanya mzigo akija kupima anashangaa imeshuka hapo alikuwa anakusanya mzgo karibu wa mls 70 na ana asaga mawe pia alikuwa na jarasha 2.
Aisee alichoma ela akahisi anarogwa akaanza zunguka kwa waganga ela inaliwa na mtaji ukakata baada ya mwaka na miezi kadhaa. Akauza makarasha akarudi town ila aliowakuta akina jembe ni jembe wanaendelea tu.
 
Sawa hata hiyo inatosha ila risk ni kubwa mno... Dhahabu ni mchakato WA muda mrefu (hasa WA marudio)...... Kwa mtaji wako itakulazimu kuchukua PPM ndogo na kumbuka wajanja ni wengi mno Kwa hii business kuegeshewa mzigo ni kugusa so kusema shngapi hasa ni itategemea ila to me at least 150 inakupa uhakika WA kurekebisha makosa kiasi ila 25 kosa dogo umeenda na maji.

Na usilogwe ukaanzisha duara au kuingiza ubia (share) kichwa kichwa.

Au laa chukua ushauri WA udalali japo unapingwa na serikali.

Katika udalali unaweza ukatenga nusu ya hiyo fedha ukatafuta dealers WA kufanya nao KAZI katika masoko then nenda kashawish wateja katika elations au mialo.... Hapa mteja utampa bei ndogo kiasi then boss wako (dealer) akupe bei nzuri.
Mfano. Umepata mteja mwenye gram 150 wewe ukampa bei ya 147,550/g then dealer ukakubaliana nae 148,300/g kinachopatikana ndo chako.

Note madalali wengi hawana mitaji wao ni mtu kati tu.

Udalali ni risk pia unaweza tengenezewa zengwe la utoroshaji kuchomoka humo utaomba poo ila vijana ndo wanaishi humo, na kuendesha familia zao.

Wajuvi watasahihisha nilipokosea.
Umeshaur vzur sana.
 
Kama una mda wa kutosha tafuta sehemu ya kuchimba weka crusher saga mawe ukuuze rudio, kuuza rudio hata kwa mwaka mzima usiwe na haraka ya kuchenjua
 
Hii itamuua kwenye kununua mawe (mgao) ukizingatia bado ni mgeni ila pia ununuzi WA mawe sio rafiki sanaaa Kwa sasa
Kama una mda wa kutosha tafuta sehemu ya kuchimba weka crusher saga mawe ukuuze rudio, kuuza rudio hata kwa mwaka mzima usiwe na haraka ya kuchenjua
 
Mwanangu me nipo chunya… ila hii kazi inaonesha hauna uzoefu nayo kabisa.. sikushauri kabisa
 
Mwenye uzoefu na dhahabu Tafadhali anielewshe hapo Kuna rafiki yangu kanitumia hyo report Kuna eneo walifanya vipimo na ananishawishi tuungane tukafanye kazi, mm sina uzoefu na mining industry, nimescreenshot part ya hyo report.
Screenshot_20231010-161935.png

Screenshot_20231010-161935.png
 
Back
Top Bottom