Biashara ya dhahabu kwa mtaji wa 25M

Biashara ya dhahabu kwa mtaji wa 25M

Mwenye uzoefu na dhahabu Tafadhali anielewshe hapo Kuna rafiki yangu kanitumia hyo report Kuna eneo walifanya vipimo na ananishawishi tuungane tukafanye kazi, mm sina uzoefu na mining industry, nimescreenshot part ya hyo report.
View attachment 2777804
View attachment 2777804
Huyu anakualika mkachimbe duara Kwa alichoandika hapo hajui anachoenda kukifanya faida mnaenda kuipta Kwa kuuza mawe kupitia migao.....

Hiyo KAZI ni zaidi ya kubet MKUU gharama alizokupa hapo sio halisi hata kidogo na uchimbaji ungekuja rahisi hivyo Kila mtu angefanya...

So far sikukatishi tamaa nenda kapambane ila andaa kiasi kingine Cha pesa kisichopungua 30M.

1. KULIpa wafanyakazi kipindi chote.
2. Kuwalisha Kwa muda wote.
3. Kwa mifuko 1000 means kuimarisha shaft (duara) italazimu kufungua matimba.
4. Tunaelekea msimu mvua maduara hujaa maji na hapo utahiji kukodi au kununua pamp (hapa ndo Kuna mziki)
5. Kama kweli mzigo na Kuna mwamba means utahitaji kublast baada ya muda. Uless hakuna mwamba mgumu.
5

Nb. Kumbuka huanzi kuchimba na kuanza kuuza mawe lazima uende chini unless ardhi hiyo Ina dhahabu sana utauza mpaka sesa (ardhi ya juu) na Kwa mtazamo wangu hapo hakuna dhahabu hiyo Hilo eneo msingekua nalopaka sasa basing on your document.


Dhahabu Kwa Tanzania Ina tycoons wake na utawakuta Kila mkoa na Kila eneo lenye mzigo wa uhakima.
 
Mkuu,KamaPesa hukuipata kwenye dhahabu basi usifanye biashara ya dhahabu kwa sasa.Ni ushauri tu.
 
Habari ndugu zangu, samahani kuna yeyote mwenye connection ya kupata kile chuma kilicho kwenye hali ya kimimilika yaani Mercury.
 
Kama Pesa kweli ipo mkononi na si ndoto kuwa ukiipata hiyo Hela ndio ..uta...
Na iwapo ni kweli unataka kuingia kwenye Biashara ya Dhahabu;

Sheikh Usikurupuke, - ELIMU kwanza;
Nyofoa Milioni mbili ziwekeze kwenye Elimu yako wewe mwenyewe kwanza kuijua Dhahabu.
Bila kujali unataka ukae upande gani hasa wa hiyo Biashara.

Si ajabu unataka kuifanya hiyo Biashara lakini huenda hujawahi hata kuiona kwa macho ya wazi inafananaje hiyo Dhahabu yenyewe.

Pale AMGC Kunduchi wanayo Kozi ya kama nadhani muda wa wiki mbili kama sikosei.
Ukitoka hapo utakuwa umefunguka pa-kubwa kiufahamu na ziada.
Kwani zaidi ya kufundishwa nadharia pia utaiona kwa macho yako na kujua mengi kuhusu Dhahabu.

Faida nyingine, wakati unasoma hapohapo upo uwezekano mkubwa wa wewe ku-connect na watu mbalimbali wanajishughulisha na shughuli mbalimbali zinazoendana na Dhahabu kama vile wataalam, Wafanya Biashara Wachimbaji, Wanunuzi Watafiti nk kutoka makundi kadha wakadha.

Mwisho, Tshs. 25Million ni Hela ndogo sana kwa wengine lakini ni Hela kubwa mno ukitulia na kujipanga vyema.

Nawasilisha.
 
Kama Pesa kweli ipo mkononi na si Ndoto kuwa ukiipata hiyo Hela....ndio ..uta...
Na iwapo ni kweli unataka kuingia kwenye Biashara ya DShahabu;

Usikurupuke, - ELIMU kwanza;
Nyofoa Milioni mbili ziwekeze kwenye Elimu yako wewe mwenyewe kwanza kuijua Dhahabu.
Bila kujali unataka ukae upande gani hasa wa wa hiyo Biashara.

Si ajabu unataka na unayo nia ya kuifanya hiyo Biashara lakini huenda hujawahi hata kuiona kwa macho inafananaje hiyo Dhahabu yenyewe.

Pale AMGC Kunduchi wanayo Kozi ya kama wiki mbili kama sikosei ( Kozi ni ya nguvu lakini)
Ukitoka hapo utakuwa umefunguka pakubwa.
Zaidi ya kufundishwa pia utaiona kwa macho yako.

Faida nyingine zaidi wakati unasoma hapohapo upo uwezekano mkubwa wa wewe ku-connect na watu mbalimbali wanaifanya kwa vitendo shughuli zinazoendana Dhahabu kama wataalam mbalimbali, Wafanya Biashara pamoja na Wachimbaji vilevile upo uwezekano wa kuwaona wawili watatu kama si kujikuta kwasababu hii au ile mkajikuta mnasoma wote.

Utaondoka na vingi kiukweli kabisa.

Lakini ikiwa huna ABC za Bidhaa yenyewe unayotaka kuhangaika nayo inaweza ikakugharimu,

Mwisho, Tshs. 25Million ni Hela ndogo sana lakini ni Hela kubwa mno ukitulia na kujipanga vyema.

Nawasilisha.

Asante sana ndugu, nitafanyia kazi
 
Samahani kaka, naomba unipe ufananuzi wa kazi ya plant na Elution au zote ni kitu kimoja?
Plant ni sehemu unapopeleka ile rudio au mchanga ulotengeneza ( saineti ), elution ndo kiwanda cha kuzalisha hyo dhahabu.

Hapo elution utapeleka carbon ambayo imeshika mali.
 
Sio kwamba sina ujuzi 100%, najua ila sio level ya kujisifu najua kuhusu hii biashara,.

Na Swali langu ni njia ipi nzuri kuweka 25M

Ni kwenye karasha kusaga mawe ya watu na kutunza Rudio

Kuingia polini kununua dhahabu kwa wachimbaji wadogo

Au kununua rudio na kupeleka plant

Naomba kujua njia ipi nzuri hapo na kwanini?
Njia nzur kuwa na karasha nunua mawe saga mwenyewe.
 
What if!
Nikiwa na shimo langu, mchimbaji akaingia kuchimba tukagawana mifuko.

Na mchimbaji aliechimba akajakusaga kwenye mashine yangu pia!!

Nikatunza lundo langu kwa 5-6months

Nikaingiza plant?

Hapo sipati kitu?
We unaijua biashara sema unaiogopa, mpk hapa unaelezea kitu poa.

Sijui unataka kutishwa na asoijua ili iweje, ingia uwanjan after 5 months nakuhakikishia 50m hii hapa.
 
Back
Top Bottom