Habari wadau,
Leo nizungumzie kidogo kuhusu boashara ya reja reja ya maduka ya bidhaa za matumizi ya nyumbani kama mchele,unga sabuni,nakadhalika.
Unapotaka kufungua aina hii ya duka ni lazima kwanza utambue eneo unalotaka kufungua je ni eneo la watu wenye kipato au watu wa hali ya chini,je ni eneo lenye mzunguko wa watu ni eneo ambalo halina mzunguko wa watu.
Kwa sababu za kiuchumi huku kwetu Super market culture bado haijakuwa vizuri kwa hiyo basi maduka haya yanauza sana.Unapotaka kufungua biashara hii haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia.
- Kodi ya fremu ya duka la reja reja yapaswa kuanzia shilingi 30,000 kwa mwezi hadi shilingi 150,000 kwa mwezi iwapo imazidi hapo ni lazima uwe na hakika kuwa eneo lina mzunguko wa uhakika.
- Leseni ya duka la rejareja ni kati ya shilingi 50,000 hadi 200,000
- Kodi kwa duka la rejareja inayolipwa TRA inaanzia shilingi 300,000 kwa mwaka kutegemea na makadirio ya mapato yako
- Kuna vitu vya aina mbili katika duka la rejareja,kwanza ni vitu vya kupima ambavyo ni muhimu zaidi kama vile unga,mchele,mafuta taa,maharagwe n.k.hivi unaweza kuviwekea mtaji wakuanzi shilingi 450,000 hadi shilingi 900,000 kutegemea kiasi na uwezo na pili ni vitu ambavyo si vya kupima mwenye kama vile sabuni,mafuta ya kupikia,sabuni za unga,sabuni za kuoga,lotions na mafuta ya kupaka,dawa za mswaki,viberiti,stili waya,mishumaa,soda,maji na vifaa vidogo vidogo.Hivi unaweza kuviwekea mtaji wa kati ya shilingi 600,000 na 1,500,000
- Kama una uwezo ongeza huduma za Mpesa,na uuzaji wa LUKU
- Unaweza kuhitaji kuwa na FRIJI,MIZANI,MASHINE YA KUUZA LUKU ambavyo unaweza kuvitengea mtaji wa angalau TZS 1,500,000
Jambo la muhimu katika duka la rejareja ni kuhakikisha kuwa unaweka kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya kila siku na kama unaweza kufunga stock basi funga stock kila baada ya miezi mitatu au unaweza kufunga stock kwa kuchagua upande wa duka yaani,vitu vya kupima peke yake na vitu vya mashelfu peke yake. Vile vile hakikisha unaweka mtu muaminifu unamfuatailia hasa kwenye mauzo na iwapo unasimamia mwenyewe usipende kutoa pesa za dukani kwa matumizi ya nje bila kujua katika mauzo hayo faida yako ni kiasi gani.
Kwa kawaida vitu vingi vya dukani profit margin yake ni ndogo sana hivyo kwa ajili ya makadiria weka margin ya 0.5 % mpaka 5% na hapo utajua iwapo mauzo yako yanakupa faida kiasi gani.
Tuendelee na mjadala