Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
 
Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
Kalamu za Nataraj unauzaje kwa bei ya jumla?
 
Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
Shukran mkuu
 
Naishi Mbagala mkuu ila umbali si tatizo naweza hamia karibu na eneo endapo,biashara ni nzuri.
Fungua huko huko mbagala mana idadi ya watu maeneo ya mbagala n kubwa sana.. Kitu cha kwanza kujuwa ni kuwa biashara unayo taka kuifanya wapo wenzio wana ifanya sasa wewe utafanya kipi cha ziada zaidi yao ili uwe tofauti nao.

Kitu cha kwanza n kuweka bei tofauti nao hata kama utapata faida ndogo ila itachukua mda mfupi kumaliza mzigo. Kingine lugha njema kwa wateja co mteja ana kuja una nunaa mpaka basi onyesha tabasamu hata kama mambo yako ndani n mabaya. Mazingira yako ya kazi yawe masafi mda wote. Mteja akija na mtoto mpe mtoto pipi ya bure ila utachagua bidhaa moja wapo itakayo kuwa ina rudisha hela ya pipi bila mteja kujua.. Biashara n akili tu hakuna ndumba wala nn la mwisho mtangulize Mungu mbele siku zote
 
nakuunga Mkono kaka shankal, ila ushauri wangu mie angaweza kufanya biashara mbadala ya uzalishaji kwa mtaji wake huo huo. kama ifuatavyo
1. biashara ya kuuza barafu
  • eneo/ Soko: wauza maji wote walipo kando kando ya barabara, mama lishe na majirani wengine ambao hawana mafrihi ya kupozea maji ya kunywa( haswa uswahiliniI) Unachotakiwa kufanya ni kila unapotoka/ kwenda chuoni jitahidi kufanya utafiti hata kuuliza size za barafu na kutangaza biashara yako japo kwa kdgo uone kwa kila kituo unapata order ngapi/ mda mwingine kuna jamaa wanakuja kununua( mia kwa barafu) kwa jumla hapo kwako wenyewe wanasambaza kwa wengine( 200 wakienda kuuza road).
  • Mtaji: upo wa aina mbili. Mtaji wa kutokuwa na aibu( kuondoa aibu kubeba barafu asubuhi wakati wenzako wamepiga kadeti na tai wewe beba barafu zako peleka kwa customer zako..
  • Mtaji wa Pesa/vitendea kazi( Friza nakushauri ununue mpya na ya kusimama( friza maalumu kwa barafu) kabisaa kama ukipata used uwe umefanya uchunguzi wa kutosha na usijilaumu baadaye. Ukinunua jipya wapata warranty ndefu na mtumba wapewa waranty muda mfupi.. kingine cha ziada bei za friza zinategemeana zinacheza kuanzia laki 7 mpaka 2 million kulingana na brand name na size ya friza. pesa inayobakia ni kuandika bango(kitambaa cha matangazo kuwa unauza barafu kwenye njia kuu ambapo unawalenga wale wateja wako uliowapitia na wengine ambao watasoma (wale wa Jumla jumla) Mtaji mwingine ni ndoo ya maji(20 lita) na kikombe na vikaratasi vya barafu ( nenda kariakoo kanunue kwa jumla then unaanza kazi)
  • Mapato: ukiwa unaanza itakupa shida ila jitahidi uwe mbunifu wa biashara yako na jiwekee malengo ya kuuuza angalau barafu 50 kwa siku ziwe kubwa na zigande ziwe chuma(jiwe) ukiuuza kwa reja reja (150*50= 7500) na ukiuza kwa jumla ni (100*50=5000) mahali pengine unaweza ukauza kwa reja reja hata 200 kulingana na bei ya soko/eneo. wingi wa barafu inategemeana na ukubwa wa friza yako
  • Gharama;Friza mpya inaweza ikala unit 4 za umeme kwa masaa 24( makisio tu), ukiweka nauli na gharama nyingine za ziada weka 15000 kwa mwezi.. bei ya unit moja ya umeme ni 400-420 ukizidisha kwa mwezi unapata( 4*30*420=50400)+ 15000= 65400 fanya na mawasiliano unajunga kwa mwezi iwe elfu 70000.
  • FAIDA: NI mapato toa gharama( kama ifuatavyo
  • kwa mauzo ya rejareja ya mia kwa mwanzoni (50 barafu)*150 ((150*50*30= 225000)-gharama(70000)=155000) mengine kwa bei ya 200 na bei ya jumla ya mia utapga mwenyewe.
naomba kuwakilisha... USAKAPESA OYEEEEEEEEEE :yield::yield::israel::israel::israel::israel:
Nimekupenda bila viatu
 
Mkuu Ibravo,
Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.
Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.
Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.
Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana;
Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.
Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.
Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.

Kuna watu wanakatisha tamaa hii Dunia.
 
Ujasiriamali unahitaji kujipa ujasiri sana ili unapokutana na vikwazo njiani na kukatishwa tamaa uweze kusimama na kusonga mbele zaidi.
 
Mimi ni mjasiriamali nimehitimu chuo nimepata mtaji wa millioni mbili nilikua na mpango wa muazisha biashara
 
Tafuta brand inayouza kama soda maji ama vilevi theni kuwa wakala/agent kwa milion 2 inatosha kuanzia na kulipa kodi ya chumba angalau miez 3. utauza kwa bei ya jumla. ungetaja na eneo ulipo ushauriwe vizuri na wadau wengine. pia fani uliosomea pengine mtaji huo waweza kujiajiri zaidi kupitia fani yako.
 
tafuta brand inayouza kama soda maji ama vilevi theni kuwa wakala/agent kwa milion 2 inatosha kuanzia na kulipa kodi ya chumba angalau miez 3. utauza kwa bei ya jumla. ungetaja na eneo ulipo ushauriwe vizuri na wadau wengine. pia fani uliosomea pengine mtaji huo waweza kujiajiri zaidi kupitia fani yako
Kwa daresalaam?
 
Achana na retail, Panga mlango mku kuu nje kidogo ya jiji (hauna gharama kubwa) nenda kwa wahindi nunua compressor mpya kubwa ya kujazia upepo tairi za magari (mara ya mwisho kuuliza bei ilikuwa ni laki 850) nunua machine ya kuchajisha betry (laki nne na nusu nadhani) nunua chupa za maji ya petri na oil chupa ndogo ndogo ongeza na oil chafu kidogo.

Nunua tairi kuu kuu saizi ya madaladala yanayofanya roots sehemu ilipo fremua yako (hizi zitakusaidia daladala inakuja na pancha unamuazima tire zako aendelee na biashara wakati unaziba ya kwake kujenga mahusiano mazuri), Nunua tire rippers, ajiri kijana mmoja anza kazi iwe 24hrs. Baada ya miezi sita leta mrejesho hapa.
 
Wadau naomba kama kuna mtu anafanya biashara ya duka la rejareja kwenye makazi ya watu anisaidie list ya bidhaa dukani nikahemee. Nataka kufungua duka la rejareja mtaani kwangu nimeshaandaa fremu na mambo mingine kilichobaki ni kuchukua mzigo.

Unisaidie bidhaa zinazotoka sana dukani. Najua maeneo yanatofautiana ila kwa makazi yetu watu wa wastani na kawaida nadhani mahitaji yetu yanafanana. Duka nalifungua maeneo ya kibamba. Nimetenga milioni 5 ya mzigo na nitashukuru kama utanisaidie na bei za jumla za kuchukua mzigo ili nijue nichukue kiasi gani na mahali unapochukulia pia.

Natambua taarifa ni mali, hivyo nimetenga elfu 40 kwa atakaenisaidia hili. Ni PM. I will pay you seriously. Nahitaji anaefanya biashara hii tafadhali.

NB supplier wa unga na mchele nishampata
 
Back
Top Bottom