Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Chumvi kubwa kwa huku 12000
Chumvi ndogo 5000
Ponpon 40000
Freestyle hizi ni ped ndogo nabkubwa 22000
Betri aina zote ndogo na kubwa wakati kubwa huku nilipo ni 110000
Sukari kg 50 ni 105000
Sukar kg 25 ni 54000
Ngano azam bora 25500
Kleesoft sabuni ya unga kg 15 ni 31000
 
List mbona haiko exhaustive mkuu. Unaweza kuandaa kwenye excel file list nzima na mahali unapochukulia hapa Dar. Nafikiria kariakoo ila sijui unachukulia wapi?
 
Madaftri makubwa 21000 mpaka 26000
Madaftari madogo ya mwandiko na hesabu 21000
Peni obama 4500 mpaka 5000
Pencil 7000
Rula 3000 kwa dazani
Dawa ya meno
Miswaki
Viwembe
Sabuni kuogea
Salama
Stiliwaya
Mafuta ya kula
Mafuta ya kupaka
Blue band
 
Chumvi kubwa kwa huku 12000
Chumvi ndogo 5000
Ponpon 40000
Freestyle hizi ni ped ndogo nabkubwa 22000
Betri aina zote ndogo na kubwa wakati kubwa huku nilipo ni 110000
Sukari kg 50 ni 105000
Sukar kg 25 ni 54000
Ngano azam bora 25500
Kleesoft sabuni ya unga kg 15 ni 31000
Shukrani sana mkuu. Unapochukulia wapi mzigo?
 
Hizi ni bei za mizigo ya kanda ya kati. Mikoa ya Manyara, Singida, Dodoma, Tabora na shinyanga

Sijajua huko kwenu wanauzaje. Maana huko viwanda vipo karibu,wauzaji wa jumla wanaweza kuuza kwa bei nzur sababu garama za usafir ni ndogo
 
Ahsante mkuu ngoja nisubiri wa Dar waje
 
Kwa mtaji ulionao tafuta bidhaa moja tu uuze kwa jumla, biashara ya duka la reja reja hailipi faida zake kwenye bidhaa ni ndogo sana kama 10% maake ni kwamba ukiuza laki moja kwa siku unapata faida 10,000 bado kodi TRA, manispaa, usafi, mlinzi. Kwa pesa hiyo unaweza fanya biashara ya nafaka na ikakulipa vizuri tu mfano unatoa mchele Morogoro au mbeya unakuja kuuza Dar.

Ni ushauri tu.
 
Kwa mtaji ulionao tafuta bidhaa moja tu uuze kwa jumla, biashara ya duka la reja reja hailipi faida zake kwenye bidhaa ni ndogo sana kama 10% maake ni kwamba ukiuza laki moja kwa siku unapata faida 10,000 bado kodi Tra, manispaa, usafi, mlinzi. Kwa pesa hiyo unaweza fanya biashara ya nafaka na ikakulipa vizuri tu mfano unatoa mchele Morogoro au mbeya unakuja kuuza Dar,
Ni ushauri tu.
Ahsante kwa ushauri mkuu. Mtaji wa nafaka upo mkuu nimeshaleta mzigo kutoka mbeya wa mchele na nina unga wa sembe na dona pia. Nataka kuweka na vitu vingine vya rejareja. Faida ya asilimia 10 inanitosha mkuu nyingi sana hiyo madam turnover ikiwa kubwa.
 
Duka la rejareja faida yake ni ndogo mnooo,kwa mfano waweza uza laki tatu kwa mwezi ukapata faida 15000 tuu.Kwa mm ninavyoona fanya biashara ya kitu kimoja kingi uuze kwa jumla mfano viazi toka Mbeya to Dar, au maharage na nafaka nyingine.
 
Duka la rejareja faida yake ni ndogo mnooo,kwa mfano waweza uza laki tatu kwa siku ukapata faida 15000 tuu.Kwa mm ninavyoona fanya biashara ya kitu kimoja kingi uuze kwa jumla mfano viazi toka Mbeya to dar,au maharage na nafaka nyingine.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu. Mtaji wa nafaka upo mkuu nimeshaleta mzigo kutoka mbeya wa mchele na nina unga wa sembe na dona pia. Nataka kuweka na vitu vingine vya rejareja. Faida ya asilimia 10 inanitosha mkuu nyingi sana hiyo madam turnover ikiwa kubwa.
Nakuongezea mbinu nyingine, baadala ya kufungua duka la rejareja, nunua bajaji ile ya kubebea mizigo nunua bidhaa nyingi halafu unasambaza kwenye maduka hakikisha bidhaa yako unaichukua kwa bei ya chini kabisa, ikiwezekana uende mwenyewe kiwanda, bajaji hiyo unaweza kuitumia kusambaza hizo nafaka kwenye maduka baadala ya kuweka mzigo kusubiri wateja.
 
Mimi nauza vifuatavyo ambavyo vinatoka haraka;

mafuta ya kula,
sukari,
unga ngano(mara nyingi naisambaza kwa mama ntilie ili iuzike haraka),
sabuni ya kufulia(ya mche na unga),
pipi na jojo,
maharage,
majani chai,
mifuko ya kubebea,
viberiti,

angalau hivyo vina cash flow nzuri kwa upande wangu.
 
Shukrani sana mkuu kwa msaada wako. Ubarikiwe sana
 
Nakuongezea mbinu nyingine, baadala ya kufungua duka la reja reja, nunua bajaji ile ya kubebea mizigo nunua bidhaa nyingi halafu unasambaza kwenye maduka hakikisha bidhaa yako unaichukua kwa bei ya chini kabisa, ikiwezekana uende mwenyewe kiwanda, bajaji hiyo unaweza kuitumia kusambaza hizo nafaka kwenye maduka baadala ya kuweka mzigo kusubiri wateja.

Nashukuru sana. Ila mimi hii biashara ya rejareja nimefanya utafiki kidogo hapa mtaani itanifaa sana maana hakuna duka la rejareja karibu lilopo liko mbali kidogo na service yake sio nzuri na linafungwa mara kwa mara na kuwalazima jamaa kutembea umbali mrefu kufuata huduma. Ni biashara ambayo nina passion nayo mda mrefu na sitauza vitu hivi tu ila nitaweka na gesi, huduma za kutuma na kupeka pesa na vocha za kurusha. Kwa sasa zinapatikana mbali kidogo kama gesi lazima upande boda boda kuifuata. Nadhani ni vizuri nikashauri kuwa nielekezwe na kushauriwa na wanaoifanya hii biashara na ushauri ujikite kwenye hii biashara maana nimeomba kusaidiwa list ya vitu kwenye hii biashara na sijaomba wazo la biashara. Hatua ya wazo la biashara nimeshatoka huko.
 
Duka la rejareja faida yake ni ndogo mnooo,kwa mfano waweza uza laki tatu kwa mwezi ukapata faida 15000 tuu.Kwa mm ninavyoona fanya biashara ya kitu kimoja kingi uuze kwa jumla mfano viazi toka Mbeya to dar,au maharage na nafaka nyingine.

Shukrani kwa wazo ndugu. Maharage na nafaka pia vitakuwepo kwenye hili duka maana nina jamaa yangu anayeleta maharage na mchele kutoja sumbawanga na mbeya atakuwa ananiletea pia. Kuhusu viazi Mbeya to Dar ninafanya hii biashara pale mabibo ila kwa sasa khali si nzuri na nimeweka mpira kwapani.

Kiazi aina ya Tigo kinauza kwa shilingi 65,000 mpaka 70,000 Mbeya (vigunia viwili hivi) na obama inauzwa kuanzia 70,000 na kuendelea shambani. Sokoni kigunia kimoja kinauzwa kwa bei ya juu 52,000 mpaka 53,000 ila bei hupungua mpaka 38,000. Usafiri wa gari ya kuchukua mzigo wa zaidi ya gunia 100 huwezi kuipata chini ya millioni moja na laki nne. Ukipiga hesabu hapo ni kama kwa gunia unapata elfu 2500 kama utauza kwa bei ya juu.

Hapa ni baada ya kutoa ushuru wa mazao, ushuru wa sokoni, pesa ya dalali na gharama zako. Ila bei ikishuka chini ya 49,000(ambayo ni kawaida maana mzigo ukikaa sana unaoza) unapata hasara. So hii naijua na huwa naifanya kwa msimu ambao soko liko vizuri.
 
Nashukuru sana. Ila mimi hii biashara ya rejareja nimefanya utafiki kidogo hapa mtaani itanifaa sana maana hakuna duka la rejareja karibu lilopo liko mbali kidogo na service yake sio nzuri na linafungwa mara kwa mara na kuwalazima jamaa kutembea umbali mrefu kufuata huduma. Ni biashara ambayo nina passion nayo mda mrefu na sitauza vitu hivi tu ila nitaweka na gesi, huduma za kutuma na kupeka pesa na vocha za kurusha. Kwa sasa zinapatikana mbali kidogo kama gesi lazima upande boda boda kuifuata. Nadhani ni vizuri nikashauri kuwa nielekezwe na kushauriwa na wanaoifanya hii biashara na ushauri ujikite kwenye hii biashara maana nimeomba kusaidiwa list ya vitu kwenye hii biashara na sijaomba wazo la biashara. Hatua ya wazo la biashara nimeshatoka huko.
Wawekee wateja maziwa ya unga ya kupima na prestige ya kupima wakikuzoea utanikumbuka
 
Back
Top Bottom