Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Mtaji wako mkubwa sana sijui kwanini umefikilia hiyo biashara, Tafuta kwanza wazo lingine
 
Hongera sana nimependa hapo ulipoweka profit margin 30%.
Kiranga njoo uone
 
Mtaji wako mkubwa sana sijui kwanini umefikilia hiyo biashara, Tafuta kwanza wazo lingine
Ni biashara ambayo imesaidia kutatua tatizo la kukosekana kwa bidhaa hapa mtaani kwetu na nadhani mtaji wake sio mkubwa kama unavyofikiri. Na ni kitu ambacho nilikuwa natamani kukifanya sana baada ya kufanya biashara za mitaji mikubwa na nikaona changamoto nyingi sana na risk kuwa kubwa. It all about passion anyway and personal life decisions.
 
Wadau naomba kama kuna mtu anafanya biashara ya duka la rejareja kwenye makazi ya watu anisaidie list ya bidhaa dukani nikahemee. Nataka kufungua duka la rejareja mtaani kwangu nimeshaandaa fremu na mambo mingine kilichobaki ni kuchukua mzigo. Unisaidie bidhaa zinazotoka sana dukani. Najua maeneo yanatofautiana ila kwa makazi yetu watu wa wastani na kawaida nadhani mahitaji yetu yanafanana. Duka nalifungua maeneo ya kibamba. Nimetenga milioni 5 ya mzigo na nitashukuru kama utanisaidie na bei za jumla za kuchukua mzigo ili nijue nichukue kiasi gani na mahali unapochukulia pia. Natambua taarifa ni mali, hivyo nimetenga elfu 40 kwa atakaenisaidia hili. Ni PM. I will pay you seriously. Nahitaji anaefanya biashara hii tafadhali.
NB supplier wa unga na mchele nishampata
Sikuiona hii, ningekula elf 40 hivi hivi
 
Mkomamazu, Safi sana mkuu. Tatizo watanzania wengi tunapenda kukatishana tamaa. Kama hapo juu watu wanasema duka la rejareja achana nalo faida ni 10% tu. Hii sio sahihi.

Mimi nilianza na bidhaa za milion 1 laki 3 katikati ya mwaka huu. Nanunua hapo manzese tip top. Day one niliuza elf 26. Mpaka sasa nauza mpaka 160 elf, siku ikiwa mbaya siuzi chini ya 80. Na bidhaa zinazidi kujaa.

Ukitaka kufanikiwa kwenye biashara tafuta site isiyokuwa na sifa za ushirikina na husijihusishe kabisa na ushirikina, fanya mwenyewe usimwajiri mtu au uwe na usimamizi madhubuti, kama unategemea duka lenyewe kuishi punguza sana matumizi, jinyime usipende sana kula kula, fanya kwa malengo, jitahidi sana kuwa mfatiliaji wa mabadiliko ya bei za bidhaa.. Usijenge chuki na wafanyabiashara wenzio.

Mimi najiona mbali siku zijazo kutokana na kiduka changu. Japo nilifukuzwa kazi lakin sijuitii.
 
yello masai,

Ni kweli mkuu pole pole tu mambo yanaenda....siku za mwanzo ni issue ila nilipata imani sana kuuza bidhaa za 10,000 kwa siku na kuna siku mauzo yanafika 200,000 kwa siku. Hapo toa tigo pesa na mpesa ambazo commision ya kwanza nilipata jumla 160,000 kwa mwezi.

Mimi bwana naliangalia hili duka kwa mbali sana....nimekula amini sitoi chochote dukani kwa miaka miwili. Faida yote naidumbukiza dukani kununua vinavyohitajika na inayobaki naiweka bank.

Baada ya miaka miwili nitafanya tathmini kuona mwenendo wake ulikuwaje for those two years. Ila so far so good.
 
Kweli mkuu. Ila ukisikiliza maneno ya watu huezi fanya. Nilianza na bidhaa za 1.3 M ila sasa hata mtu akija na 4 M simwachii. Tupige kazi tu.
Mimi na wew tupo kwenye same boat....nilianza kama utani....sikuwa na sukari...mafuta...na bidhaa kibao....ila now nna kila kitu na still bado naona haitoshi....!!duka faida ipo...kama ukiwa serious na malengo...!!
 
Back
Top Bottom