Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Naishi Mbagala mkuu ila umbali si tatizo naweza hamia karibu na eneo endapo,biashara ni nzuri.
Mbagala ni pazuri pia kutokana idadi kubwa ya watu wanaoishi huko, ukipata huko ni vema sana
 
Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
 
Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
Kalamu za Nataraj unauzaje kwa bei ya jumla?
 
Jaribu huko huko mbagala hasa upande wa kulia kama unaenda kongowe yaan kuanzia pale terminal hadi kule kwenye jengo jipya. Kila la kheri karibu tujiajiri, ukitaka pipi, biscuits na jojo njoo ntakuuzia kwa bei ya jumla.
Shukran mkuu
 
Naishi Mbagala mkuu ila umbali si tatizo naweza hamia karibu na eneo endapo,biashara ni nzuri.
Fungua huko huko mbagala mana idadi ya watu maeneo ya mbagala n kubwa sana.. Kitu cha kwanza kujuwa ni kuwa biashara unayo taka kuifanya wapo wenzio wana ifanya sasa wewe utafanya kipi cha ziada zaidi yao ili uwe tofauti nao.

Kitu cha kwanza n kuweka bei tofauti nao hata kama utapata faida ndogo ila itachukua mda mfupi kumaliza mzigo. Kingine lugha njema kwa wateja co mteja ana kuja una nunaa mpaka basi onyesha tabasamu hata kama mambo yako ndani n mabaya. Mazingira yako ya kazi yawe masafi mda wote. Mteja akija na mtoto mpe mtoto pipi ya bure ila utachagua bidhaa moja wapo itakayo kuwa ina rudisha hela ya pipi bila mteja kujua.. Biashara n akili tu hakuna ndumba wala nn la mwisho mtangulize Mungu mbele siku zote
 
Nimekupenda bila viatu
 

Kuna watu wanakatisha tamaa hii Dunia.
 
Ujasiriamali unahitaji kujipa ujasiri sana ili unapokutana na vikwazo njiani na kukatishwa tamaa uweze kusimama na kusonga mbele zaidi.
 
Mimi ni mjasiriamali nimehitimu chuo nimepata mtaji wa millioni mbili nilikua na mpango wa muazisha biashara
 
Tafuta brand inayouza kama soda maji ama vilevi theni kuwa wakala/agent kwa milion 2 inatosha kuanzia na kulipa kodi ya chumba angalau miez 3. utauza kwa bei ya jumla. ungetaja na eneo ulipo ushauriwe vizuri na wadau wengine. pia fani uliosomea pengine mtaji huo waweza kujiajiri zaidi kupitia fani yako.
 
Kwa daresalaam?
 
Achana na retail, Panga mlango mku kuu nje kidogo ya jiji (hauna gharama kubwa) nenda kwa wahindi nunua compressor mpya kubwa ya kujazia upepo tairi za magari (mara ya mwisho kuuliza bei ilikuwa ni laki 850) nunua machine ya kuchajisha betry (laki nne na nusu nadhani) nunua chupa za maji ya petri na oil chupa ndogo ndogo ongeza na oil chafu kidogo.

Nunua tairi kuu kuu saizi ya madaladala yanayofanya roots sehemu ilipo fremua yako (hizi zitakusaidia daladala inakuja na pancha unamuazima tire zako aendelee na biashara wakati unaziba ya kwake kujenga mahusiano mazuri), Nunua tire rippers, ajiri kijana mmoja anza kazi iwe 24hrs. Baada ya miezi sita leta mrejesho hapa.
 
Wadau naomba kama kuna mtu anafanya biashara ya duka la rejareja kwenye makazi ya watu anisaidie list ya bidhaa dukani nikahemee. Nataka kufungua duka la rejareja mtaani kwangu nimeshaandaa fremu na mambo mingine kilichobaki ni kuchukua mzigo.

Unisaidie bidhaa zinazotoka sana dukani. Najua maeneo yanatofautiana ila kwa makazi yetu watu wa wastani na kawaida nadhani mahitaji yetu yanafanana. Duka nalifungua maeneo ya kibamba. Nimetenga milioni 5 ya mzigo na nitashukuru kama utanisaidie na bei za jumla za kuchukua mzigo ili nijue nichukue kiasi gani na mahali unapochukulia pia.

Natambua taarifa ni mali, hivyo nimetenga elfu 40 kwa atakaenisaidia hili. Ni PM. I will pay you seriously. Nahitaji anaefanya biashara hii tafadhali.

NB supplier wa unga na mchele nishampata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…