Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Hongera
Retail business ndio ina faida
 
Safi sana mkuu umeleta amasa kwa wengine
 
Duka la rejareja faida yake ni ndogo mnooo,kwa mfano waweza uza laki tatu kwa mwezi ukapata faida 15000 tuu.Kwa mm ninavyoona fanya biashara ya kitu kimoja kingi uuze kwa jumla mfano viazi toka Mbeya to dar,au maharage na nafaka nyingine.
Mkuu faida ya duka la rejareja ni kati ya 10% hadi 18%. Na hilo ni duka gani uuze 300,000 kwa mwezi? Mi nina duka la mtaji 2 mil nauza kati ya elfu 40 hadi 60 kwa siku pia nina genge nauza elfu 25 hadi 40 kwa siku. Na trend ya msuzo inakuwa positively

Kuuza laki 3 kwa mwezi maana yake unauza elfu 10 kwa siku. Hapo unakuwa ulifungua duka bila kupata ushauri au kupiga hesabu zako vizuri
 
Kutoa elfu 40 ni kujitakia tu, hata usingetangaza hilo dau still watu wangekusaidia.
Nilitaka kufanya maamuzi ya haraka na sikuwa na mda wa kusubiri japo kuna waliojitokeza kunisaidia na nawashukuru sana. Sio kwamba sikujua kuwa nitapoteza elfu 40 ila kama kuna mtu angejitokeza na kunipa vitu nilivyotaka sikuwa na hiana kumpa hiyo pesa maana nilishapanga kufanya hivyo na najua angepoteza muda wake na rasilimali kuifanya hivyo.
 
Kwa kuongeze hapa uliposema sio rahisi kuuza bidhaa za duka la reja reja kama umesite vizuri kwa mwezi uuze 300,000. Huyu jamaa alipost hii post kabla sijaanza na kama ningemsikiliza ningekata tamaa. Tujaribu kuchangia mada tunazojua undani wake kwa faida ya wengi na sio kuchangia kitu ambacho hujakifanya. To be honest tangu nimeanza leo hii mwezi wa tatu sijawahi kuuza kwa mwezi chini ya laki 9 ni kati ya 1.2 mpaka 1.5 a month. Hata kama mtu ukiuza 300,000 kwa mwezi kwa profi margin ya 10 to 18% huwezi kupata tu 15,000 labda kama uwe hujafanya pricing nzuri na kupunguza matumizi dukani. Tunaofanya hii biashara tunaona na kujua yaliyomo na binafsi niko tayari kumshauri mtu yeyote anayetaka kuingia huku kwa uzoefu wangu wa angalau these 3 months.
 
Mkuu mim nimevutiwa sana na ujasiri wako nami nipo njiani najipanga na msingi ukikaa pouwa nitakucheki kwa ushauri wako zaidi.na je msingi wa kiasi gani kwa wastani duka la reja reja unafaa kwa hali ya chini,?
 
Hivi mtu anaweza kukopeshwa na benki kwa kutumia bussness plan?
 
Hongera sana mkuu.

Kuna maduka mawili makubwa yapo tandale, moja wanaita kwa nasoro, Lingine wanaliita kwa lazaro wanauza hizi bidhaa kwa bei ya jumla. Bei zake zipo chini kdg ukilinganisha na maduka mengi ya manzese.

Location: baada ya kumaliza daraja la manzese uelekeo wa magomeni, barabara ya kwanza kushoto nenda nayo moja kwa moja jengo la kwanza la ghorofa kushoto kwako ndipo hapo kwa nasoro. Kufika kwa lazaro kutokea kwa nasoro, endelea na barabara hiyo hiyo uelekeo wa kwenda sweet coner, thn kunja barabara ya kwanza kulia, uelekeo wa tandale sokoni, kabla hukafika tandale sokoni, uliza dukani kwa lazaro utaelekezwa.

*Duka linalipa ukiwa makini na kazi
 
Nashukuru sana kwa mleta huu uzi kwani hata mimi mwakani ni
mejipanga kufungua duka la rejareja kupitia hapa nimeweza kujifunza mengi
 
Barikiwa sana mkuu kwa kuweza kushare na wenzanko kile unachokifahamu hakika umeonyesha wewe sio mbinafsi
 
Thank you for sharing.
 
Ahsante sana mkuu. Hapo kwa Nassoro ndo nilinunua bidhaa za kwanza kabisa kuna jamaa alinielekeza. Kwa lazaro sijafika, nitafika pia. Shukrani sana
 
Hivi mtu anaweza kukopeshwa na benki kwa kutumia bussness plan?
Nadhani zamani kwa siku hizi mkuu sijui japo nadhani ni bora ukapambana upate chochote chako uanze biashara hiyo baadae kama unataka kuendelea ndo ukakope. Ila wazo tu bila uzoefu wa biashara kwa waswahili wa mabenki yetu hapa sijui kama inawezekana. Maana siku hizi watu wanachukua business plan online wanazi - customize kwenye idea zao na wengi wanakuwa na wasiwasi na feasibility ya kitu mpaka waone. Kukopa ili uanze biashara mimi sishauri sana bora upambane hata kama ikubuma unakuwa huna deni na mtu. Nimefanya hivyo maraja nyingi na zimenibumia na wala sidaiwi na mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…