Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Naomba nielekezwe namna ya kujua kufanya hesabu kila mwisho wa mwezi kwny faida na hasara kwny duka hilo la rejareja
 
Aisee Jf siondoki n'goo!! Kuna watu very critical kwa ushauri
 
hakuna biashara pasua kichwa kama duka la rejareja.... usipozingatia mwenyewe ndani ya muda mfupi biashara inakufa kabisa, duka liko hivi unajikuta unatumia mda wako mwingi sana kuumiza kichwa nifanyeje duka langu lijae au nifanyeje biashara yangu isonge.....

naweza kukushauri yauatayo, huwa kwa kawaida maduka ya rejareja yanafahamika kuwa yana faida kiduchu sana, kwa hio kama unaweka hela au unafanya matumizi binafsi hakikisha juwa hela unayoitoa hapo haizidi 10% ya mauzo yako . mfano umeuza laki moja, hapo kama unafanya serving unatakiwa uweke elfu kumi tu.

changamoto kubwa maduka ya rejareja ni mikopo, mtu anakuzoea kuwa mteja wako siku mbili tatu leo anaishiwa anakuja anakwambia hali mbaya niazime mchele kg 5 na mafuta lita moja, utashindwa kumpa ? utaona aibu, wateja wengine ni waaminifu wanarejesha kweli, mwingine ukimpa ndio imekula kwako anakuhama kabisa.

pia tengeneza mahusiano mazuri(ya kibiashara) na wanawake kwa ujumla (wake za watu, wamama na mabeki tatu) hawa ndio wateja wakubwa kwa sababu ndio wanahusika kununua vitu vya nyumbani

kauli nzuri kwa wateja, sio unanuna kama unauza sumu... all the best
 
Upasua kichwa wake upo wapi, umeanza kwa vitisho
 
Upasua kichwa wake upo wapi, umeanza kwa vitisho
sio vitisho mkuu ni real..... ina faida ndogo sana ukizingatia pango sijui uweke hela ya umeme, then ukute umemweka mfanyakazi au pengine unakaa mwenyewe.... pia kinachofanya hii biashara iwe ngumu ni mchuano, yani unakuta mwenzio ana duka jiran na wewe atashusha bei ili apate wateja wengi, wewe ukisema unamuiga inakula kwako, kwa staili hii nishaona biashara nyingi sana zimekufa. ebu chukulia umenunua juice catoni moja (juice za mo), bei yake ni 5000 mpaka 5200, na zinakaa 12, hapo kwa haraka haraka unatakiwa uuze moja 600, lakini jirani yako anauza 500 akilenga kupata faida ya 1000 au 800 kwa catoni moja. je unadhani hii faida inakidhi ? hapo hatujaweka gharama za umeme wako, pia pengine mzigo unachukulia mbali kidogo umemlipa bodaoda au mwendesha mkokoteni , je hapo kuna kitu tena ? nadhani umeelewa kitu hapo, alafu watz tulio wengi mtu akipata hela kdg anawaza kufungua duka tu hawazi kingine, kuna biashara kama genge zinalipa sana mtu ukipata senta nzuri
 
I
JF INA watu wenye akili mingi sana
 
Habari wana jamvi, nahitaji kufungua biashara ya duka la rejareja mahitaji ya nyumbani. Naomba mwongozo maduka ya jumla yako wapi jijinibdar es salaam mimi ni mgeni.

Maduka ya vitu kama sabuni, baby diapes,betri. Achana na vitu vya kupima kama nafaka, hivyo nimekuja navyo toka Tanga nimehamisha duka.

karibuni kuchangia wajameni.
 
Ni Mmakonde mmoja hivi anaishi na Mwanamke wa Kizungu, kama hutojali unaweza kugoogle utapata maelezo yatakayo kidhi haja yako kwa kiwango cha kuridhisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…