yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,662
- 3,715
Sawa mkuuJali sana wateja wako
Uwe na maono sahihi juu ya bussiness yako, na fanya tathimini baada ya mwezi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mkuuJali sana wateja wako
Uwe na maono sahihi juu ya bussiness yako, na fanya tathimini baada ya mwezi
Fursa hiyo. Fungua duka madamNimesubscribe....
Naona mtaa nnaoishi hakuna duka, yapo mbaali fursa.
Hivi ulikuaga na duka eeh? Kuna mambo nahitaji kufahamishwaFursa hiyo. Fungua duka madam
Upasua kichwa wake upo wapi, umeanza kwa vitishohakuna biashara pasua kichwa kama duka la rejareja.... usipozingatia mwenyewe ndani ya muda mfupi biashara inakufa kabisa, duka liko hivi unajikuta unatumia mda wako mwingi sana kuumiza kichwa nifanyeje duka langu lijae au nifanyeje biashara yangu isonge.....
naweza kukushauri yauatayo, huwa kwa kawaida maduka ya rejareja yanafahamika kuwa yana faida kiduchu sana, kwa hio kama unaweka hela au unafanya matumizi binafsi hakikisha juwa hela unayoitoa hapo haizidi 10% ya mauzo yako . mfano umeuza laki moja, hapo kama unafanya serving unatakiwa uweke elfu kumi tu.
changamoto kubwa maduka ya rejareja ni mikopo, mtu anakuzoea kuwa mteja wako siku mbili tatu leo anaishiwa anakuja anakwambia hali mbaya niazime mchele kg 5 na mafuta lita moja, utashindwa kumpa ? utaona aibu, wateja wengine ni waaminifu wanarejesha kweli, mwingine ukimpa ndio imekula kwako anakuhama kabisa.
pia tengeneza mahusiano mazuri(ya kibiashara) na wanawake kwa ujumla (wake za watu, wamama na mabeki tatu) hawa ndio wateja wakubwa kwa sababu ndio wanahusika kununua vitu vya nyumbani
kauli nzuri kwa wateja, sio unanuna kama unauza sumu... all the best
sio vitisho mkuu ni real..... ina faida ndogo sana ukizingatia pango sijui uweke hela ya umeme, then ukute umemweka mfanyakazi au pengine unakaa mwenyewe.... pia kinachofanya hii biashara iwe ngumu ni mchuano, yani unakuta mwenzio ana duka jiran na wewe atashusha bei ili apate wateja wengi, wewe ukisema unamuiga inakula kwako, kwa staili hii nishaona biashara nyingi sana zimekufa. ebu chukulia umenunua juice catoni moja (juice za mo), bei yake ni 5000 mpaka 5200, na zinakaa 12, hapo kwa haraka haraka unatakiwa uuze moja 600, lakini jirani yako anauza 500 akilenga kupata faida ya 1000 au 800 kwa catoni moja. je unadhani hii faida inakidhi ? hapo hatujaweka gharama za umeme wako, pia pengine mzigo unachukulia mbali kidogo umemlipa bodaoda au mwendesha mkokoteni , je hapo kuna kitu tena ? nadhani umeelewa kitu hapo, alafu watz tulio wengi mtu akipata hela kdg anawaza kufungua duka tu hawazi kingine, kuna biashara kama genge zinalipa sana mtu ukipata senta nzuriUpasua kichwa wake upo wapi, umeanza kwa vitisho
Ndo nimefungua tu sina hata mweziHivi ulikuaga na duka eeh? Kuna mambo nahitaji kufahamishwa
JF INA watu wenye akili mingi sanaMkuu Ibravo,
Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:
Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.
Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.
Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.
Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana;
Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.
Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.
Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.
Endelea tu kwenye kufungua duka lako utafanikiwa Dar es Salaam is the Land of opportunity for any hardworker
Isee mimi Mtu mume picha hiyo ni ya mke wangu.Thank you mamie
Isee mimi Mtu mume picha hiyo ni ya mke wangu.
You are welcome!Thank you and sorry for confusing.
Wewe ni Harmonize au Shemeji amefanana na Sara Mmasai?Isee mimi Mtu mume picha hiyo ni ya mke wangu.
Samahani ndio nani huyo Harmonize?Wewe ni Harmonize au Shemeji amefanana na Sara Mmasai?