Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Kuchanganya vyoye ndo bora zaidi.
Naona bora hata duka la vyakula lina maslah kuliko duka la kawaida maana kuna bidhaa inakupa faida ya 8000 sasa kwny duka la kaawaida kuna baadh ya takeaway unanunua sh 417 unakuja kuuza 500 kweli utatoka?
 
Chumvi kubwa kwa huku 12000
Chumvi ndogo 5000
Ponpon 40000
Freestyle hizi ni ped ndogo nabkubwa 22000
Betri aina zote ndogo na kubwa wakati kubwa huku nilipo ni 110000
Sukari kg 50 ni 105000
Sukar kg 25 ni 54000
Ngano azam bora 25500
Kleesoft sabuni ya unga kg 15 ni 31000
Uzi una mwaka tayari, ingekuwa vyema mtoa mada hapa atupe mrejesho wa maendeleo ya biashara yake. Mkomamazu, njoo hapa tafadhali utueleze maendeleo yako.

Asante
 
Uzi una mwaka tayari, ingekuwa vyema mtoa mada hapa atupe mrejesho wa maendeleo ya biashara yake. Mkomamazu, njoo hapa tafadhali utueleze maendeleo yako. Asant
Nimesema mara nyingi so far so goo and I see the future holding well. Kikubwa naendelea vizuri tu na mimi lengo la kuleta uzi ni kutaka kupata taarifa kuhusu biashara ya rejareja. Maendeleo ya duka langu hayo ni ya kwangu wala halikuwa lengo langu kuu. Ila taarifa tu zihusuzo hii biashara.
 
Nimesema mara nyingi so far so goo and I see the future holding well. Kikubwa naendelea vizuri tu na mimi lengo la kuleta uzi ni kutaka kupata taarifa kuhusu biashara ya rejareja. Maendeleo ya duka langu hayo ni ya kwangu wala halikuwa lengo langu kuu. Ila taarifa tu zihusuzo hii biashara.
Mkuu kama hutajali tengeneza group la whatsapp iwe rahisi kupeane updates mbalimbali kama bidhaa, bei zake na machimbo ya kupata bidhaa kwa bei nzuri
 
Asante ndugu
Apart frm this, dukan kwang nauza zaid sana pombe kal na lain {mbalimbali} Huwa naongeza bidhaa kutokana na uhitaji wa mteja. Anapohitaj kinywaji flan chaap nakifuatilia kama sina kwa ufup nafanya biashara kimkakati sanaa. Ss bas nahita idea ya bidhaa au hiduma nayoweza uza yenye faida kubwa. Sio chin ya 1000 ikiwa chin sana bas isipungue Faida 500.

Naomba idea nzur tafadhali wenye uzoefu na wasio na uzoefu.
 
Napendaga sana nikiona mangi tunapeana updates kama hizi. Nakumbuka wakat naanza nilimuambia girlfrnd nataka kuanza kuuza duka akanicheka. Nilikuwa mchumi mpaka tukaachana, lakini ilinibidi nimove on kwani nilibania pesa kwakuwa ndo biashara ilikuwa inaanza.

Nashukuru Mungu Maisha yanaenda. Future naiona. Nakula nnachotaka

Hii biashara inalipa sana, lakini hasa ukiwa serious
 
Yaani wewe jamaa balaa. Kwa hiyo faida ya TZS 83 sio pesa mkuu? Ukiuza 100 si 8,300 hiyo? Kwani ulishajiuliza vocha wanapata faida kiasi gani? Vitu vingine vipo dukani vya faida kidogo ila sisi tunaviita baiting item. Yaani bidhaa chambo. Hizi bidhaa zinaleta wateja dukani na akifika dukani anaweza kununua kitu kingine chenye faida kubwa. Mtu akija kununua vocha anaweza kupenda kitu ambacho amekiona dukani na akawa anakihitaji na pengine hakuwaza kuwa angekikuta hapo. Ivi ulishajiuliza kuwa daladala ina seat 25 ambazo kwa trip moja kama jamaa hajasimamsisha abiria anakula 10,000 tu?

Hata kama akisimamisha na kushusha na kupandisha kwa trip moja kama anatoka simu 2000 anaenda Mbezi mwisho mara chache sana atagonga 20,000 mkuu. Sasa piga hesabu za mafuta, pesa ya kuwaachia wapiga debe, pesa ya hesabu. Lakini jamaa wanadunduliza na wako njiani kila siku na wanatengeneza pesa. Usipende biashara ya faida kubwa sana ila risk kubwa na investment yake ni kubwa sana.

Sie ngoja tukomae huku kwanza na hiki kidogo tupate uzoefu wa kuheshimu pesa kabla ya kuanza hizo zenye faida kubwa. Kikubwa ni kwamba duka la rejareja linalipa sana maana hizo ndo supermarket za mtaani na kila siku watu wanatumia bidhaa zetu maana nyingi ni necessities na lazima wanunue.
Naona bora hata duka la vyakula lina maslah kuliko duka la kawaida maana kuna bidhaa inakupa faida ya 8000 sasa kwenye duka la kaawaida kuna baadh ya takeaway unanunua sh 417 unakuja kuuza 500 kweli utatoka?
 
Kama mnaniruhusu semeni su! WhatsApp group hilo
 
Well presented!

Nimekuelewa sana!

Hiyo ndio tunasema UTOFAUTI wa Kibiashara!

Kuna bidhaa zinakaa dukani kiMKAKATI mf Vouchers za simu, soda etc!

Mteja wa vocha ya tigo ya 500 leo, kesho atakuja kununua voucher na sukari ama ngano!

Baada ya wiki anakuwa mteja wako mazima!

Mkomamazu,
 
Sina uzoefu sana wa biashara ila nimepambana, nimefungua duka la rejareja eneo ambalo ni karibu na chuo, kwa hiyo wateja wetu wengi asilimia 90% ni wanachuo.

Natambua mawazo yanatofautiana, ujuzi unatofautiana lakini pia kila siku tunajifunza maana maarifa hayana mwisho. ombi langu kwenu nahitaji ushauri wa bidha ambazo naweza nikaziongezea kwa duka langu au kiti kingine ambacho naweza nikakiongeza dukani kutokana na mazingira (location) ya duka niliyoyataja kikanipa faida.naamini kwa mawazo yenu pengine nitapata mwanga (wazo jipya) ambao sikulifikiria.

Bado naendelea na utafiti binafsi kutokana na mazingira lakini naamini mawazo yenu yanaweza fungua upeo wangu zaidi juu ya biashara.

Nb.duka ni la rejareja, lina vitu muhimu vya majumbani kama vile mchele, vinywaji kasoro bia na sigara (siweki vilevi),sabuni, unga n.k.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom