Raphael Thedomiri
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 442
- 729
Yap! KabisaKupanga ni kuchagua funga duka katafute story mtaani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yap! KabisaKupanga ni kuchagua funga duka katafute story mtaani
Kuna watu hawataelewa ulichoandika hapa..!Anaesema haamini uchawi katika biashara, huenda hajawahi kufanya biashara, na kama anafanya biashara na kufanikiwa ni "maujanja" yake. Ndio maana waliofanikiwa wanaamini "mafanikio ni Siri na Siri ndio mafanikio". Na kama hujawahi kufanya biashara fanya kichwakichwa uyaone.
Good experienceNilipo maliza Form four matokeo hayakuwa mazuri sana nikamwambia mzee nifungulie biashara ya duka ili nijenijiendeleze mwenyewe kimasomo kwa hela yangu kweli mzee alikubali akanipa mtaji nakumbuka wa 350,000 akanijengea kaduka hapo home ambacho kiligharimu kama 1.5m ujenzi wake miaaka ya 1990, Nilikomaa na biashara kwa hasira nakumbuka sikutaka kabisa kupoteza muda ilinibana kisawa sawa lazima ujikane na uache mambo mengi hadi starehe unaweza kujikuta hata kuoga ni issue kwani huna muda huo mpaka usiku.
Nilikuwa na location nzuri wateja kibao hasa wakina mama, na kawa mjanja nikaweka bidhaa kulingana na mahitaji mfano mimi nilianza na kaduka kabidhaa na vyakula baadaye nikaona watu wanahitaji Pombe ilo eneo limezungukwa na wachaga wengi nikaweka pombe ilinipa wateja wengi sana watu walisema nilikuwa na kamzizi kumbe hapana nilikuwa na kauli nzuri na wateja by that time ulikuwa ukiuza cret moja ya bia unapata faida ya 9,400 nilijikuta kwa siku nauza cret 2 na wik end nauza 4-5.
Nikaweka binti mkali sana toka Kondoa kama muhudumu anakuja jioni nilipiga hela kwa kweli, Nikapata mtaji wa kutosha nikawongeza huduma ya nyama choma na supu jioni.
Wadau wakaongezeka sana nikatenganisha Duka nikaweka kipub nyuma na jiko la nyama choma na supu nikaongeza wahudumu wakawa wawili warembo sana nakumbuka mmoja aliitwa Celina alikuwa na nyota ya wateja sana hayo magari yanaopark hapo mauzo yakapanda nikawa nauza cret 10 kwa uchache hapo hata ndoto za shule ziliyeyuka kabisa, nikajenga room moja kama vip hivi baada ya kupata ushauri wa wateja ambao walikuwa VIP kazuri full AC kifupi nilipata hela sana nikajenga room tano za kulala maana wateja walidemand sana.
Baadaye ulizuka mgogoro mkubwa wa kifamilia nikaamua kufunga nikaenda zangu chuo kupiga certificate na baadaye diploma nikahamisha biashara Jijini Dar sasa napiga kazi nyingine.
Hii ya poutry ni ngumu mara 2 zaidi ya duka.kwenye poultry kuna mziki mwengine huko, wa matunzo mana makuku haya ya kisasa, mmh! maybe kama utafanya na wa kienyej
Kwaiyo kuku wa kisasa awa lali muda wote ni kula tu?Hii ya poutry ni ngumu mara 2 zaidi ya duka.
Maana kuku wanahitaji care ya hali ya juu yaani uangalizi wake ni wa masaa 24.
Inabidi muda mwingine inakubidi uamke usiku wa manane ukaangalie kama kuna chakula cha kutosha,maji ya kutosha pamoja na usalama wao kwa ujumla.
Wakati duka uangalizi wake ni wa masaa 12 tu kisha unaenda kulala.
hawana muda maalumu wa kula na kulala kama wewe unavyojipangia.Kwaiyo kuku wa kisasa awa lali muda wote ni kula tu?
Biashara ya DUKA ni nzuri, ila baishara ya KIOSK ni stress.