Mkuu hakuna mtaji mdogo wala mkubwa kwenye biashara yote ile.
Hiyo pesa inatosha kwa kuanzia.
Muhimu tafuta eneo zuri lenye idadi ya watu wengi ambao wanaweza kuwa wanunuzi.
Zingatia sana kuwe na watu wengi lkn watakaoitaji bidhaa utakazokuwa unauza.
Kwa pesa hiyo usianze na vitu vikubwa kama vile nondo, saruji, mbao nk.
Anza na vitu vidogo kama vile Nyundo, misumeno, misumari, tape measure, bidhaa za umeme kama vile nyaya za umeme, balbu nk.
Usihamishe goli kwa kufikiria kufanya kitu tofauti na unachopenda kufanya.
Nakutakia mwanzo mwema na mwaka ujao tarehe kama hizi lete mrejesho.