Biashara ya hardware kwa mtaji wa mil.7

Pamoja sana. Usiogope. Hakunaga pesa inayotosha kuanzisha kitu. Hata huo mtaji wako ungekuwa ni 700M badala ya 7M, bado tu usingeweza kuweka kila kitu.
Nimekupata vyema mkuu.. ngoja nitafute location nzuri
 
Spea za nini gari, pikipiki?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Umemshauri vyema sana namimi nalichukua wazo lako kama lilivyo nifanyie kazi kama nitaweza nitakujulisha
 
Umeshaanza??
 

Mkuu hakuna mtaji mdogo wala mkubwa kwenye biashara yote ile.
Hiyo pesa inatosha kwa kuanzia.
Muhimu tafuta eneo zuri lenye idadi ya watu wengi ambao wanaweza kuwa wanunuzi.
Zingatia sana kuwe na watu wengi lkn watakaohitaji bidhaa utakazokuwa unauza.
Kwa pesa hiyo usianze na vitu vikubwa kama vile nondo, saruji, mbao nk.
Anza na vitu vidogo kama vile Nyundo, misumeno, misumari, tape measure, bidhaa za umeme kama vile nyaya za umeme, balbu nk.
Usihamishe goli kwa kufikiria kufanya kitu tofauti na unachopenda kufanya.
Nakutakia mwanzo mwema na mwaka ujao tarehe kama hizi lete mrejesho.
 

Asante mkuu kwa ushauri wako.. bado naendelea kutafuta location mzuri
 
Mkuu hapa mwisho nimecheka sana 😀
 
Umesema kweli
 
Usikate tamaa mimi nilianza na mataji ulio Chini ya hapo nilianza na kuuza cement tu vitu vingine niliendelea na naendelea kuongeza hadi saiv
 
Kwa kunzia inatosha kabisa kwa hadware ya kawaida ukimix na vifaa vya umeme, vitasa vya milango misumari size zote, makomeo disk za kukatia chima na vungne vingi vodogo vidogo hadi mtaji ukue
 
Huo mtaji mkubwa inatakiwa atafue uchocholo wanakojenga sana mbona atauza tu hasa wajengaji wadogo wadogo
 
Tatizo baadhi ya wabongo wanadhani lazima uwe na mtaji mkubwa wanashindwa kuelewa kuwa mbuyu ulianza kama mchicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…