Ili wazo nilitoa mwezi wa 9/10 kwenye group langu la whatsapp namna ya kupiga pesa kwa kutumia modem ya voda ya 5G. Modem ya voda inafika 200m kutokana na maelezo yao, unaweza ukatafuta sehem yenye mkusanyko wa watu ukafungua hii biashara ambayo mtu anaweza ku access internet ndani ya 200m.
Dada mmoja kwenye group aliipenda sana hii idea na kuchukua hatua na sasa anafanya kwenye mkoa alipo. Modem ya voda inatoa vifurushi tofauti kwa yule dada kaanza na speed ya 30mbs ambacho kwa mwezi ni 150k.
Voda wanatoa modem bure ila unaingia mkataba wa miezi miwil , modem inauwezo wa host device 64.
Kuzuia watu wasishare password, unaweza kufanya configuration kwenye router kwa kuwapa access wale tu ambao umewaunga na kuwapa access na ku assign mac address ya simu au device ili kuzuia new device isiweze ku access internet bila kulipia au kupewa access.