Habarini wana JF,
Kama ada ya Watanzania wengi, nina wazo la kuuza internet kwa watu.
Muda mrefu nimekuwa nikifanya utafiti kupitia mitandao ya kijamii nimegundua biashara hii inaweza ikafanywa na vijana walio wengi wa Tz badala ya kukomaa na library, vibanda umiza, pharmacy na biashara zingine ndogo ndogo ambazo zimekuwa kimbilio la vijana wengi.
Hii biashara ni maarufu sana kwa vijana wa nchi kama Ufilipino, Indonesia, India, Pakistan na nchi kadha wa kadha. Hata kwenye utafiti wangu kupitia YouTube vijana wengi kutoka nchi hizo ndio ma-dealer sana wa biashara hizi.
Pia nikaja kugundua hata hapa Tz wapo watu wanafanya biashara hii ila ujuzi ndio changamoto hasa utumiaji wa teknolojia sahihi kwenye hii biashara.
Nikakutana na internet ya kijamii kutoka UDOM kupitia masafa ya UHF(WHITE SPACE TV). Hivyo nikaonelea inaweza kuwa msaada mzuri kwenye kufanya biashara ya internet. Ila changamoto kupitia program hii utaalam ni changamoto hivyo watahitajika wataalam na mtaji mkubwa kiasi kufanikisha biashara hii. Ila bado pana ombwe kwani bado sijajua gharama halisi kuweza kunufaika na internet hii.
Nikarahisisha wazo kwamba si lazima sana kutumia masafa ya white space tv, bali vijana wanaweza kukodi internet kutoka makampuni pendwa kama Supakasi ya Vodacom, au fiber za TTCL, ZUKU, GO FIBER, SIMBANET na kampuni za VSAT kupitia vifurushi vyao vya unlimited/uncapped data.
Kama kampuni husika itaruhusu kugawa internet, basi kijana unaweza kutumia fursa hiyo kwa kukodi unlimited internet na kununua baadhi ya vifaa ila kuweza kusambaza kwa waya ama wireless access point.
Vifaa muhimu ni kama komputa, router, cloud key software na vifaa vya kurushia wifi kama camfast au tplink
Mpango wa wateja ni kuuza vocha ambazo utaziprint kupitia software za mtandaoni ama kuuza kwa wifi ya password.
Lengo ni kuuza kwa wateja wengi iwezekanavyo na kufwata mlolongo mzuri wa kibiashara ikiwemo kufanya saving, cash flow au liquidity analysis na mambo kadha wa kadha ya kibiashara ikiwepo utafiti wa soko, mchanganuo wa biashara nk
Vipi mdau wa Jamii forum? Una uzoefu wa hii biashara? Nini mtazamo wako? Una teknolojia gani kuboresha? Una project kama hii ambayo ina exisist? Tuambiwe kwenye komenti hapa kiungani.
View attachment 2437983