Biashara ya Jezi inavyokua kwa kasi, Je zinatengenezwa wapi?

Ze_Papirii

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
558
Reaction score
1,117
Habari wanajamvi..

Nimejaribu kutembelea miji, manispaa, na majiji mbalimbali kwakweli kuna utitiri mkubwa sana kwa sasa wa maduka yanayouza jezi mbalimbali za timu za mpira wa miguu.

Kwa utafiti wangu mdogo nmeona jezi hizi zinapatikana kwa bei tofauti kutokana na eneo ila zina range kwenye 13k-25k kwenye maeneo mengi na jezi zinazouzwa sanaa ni za juu(t-shirt).

Ninachojiuliza ni kitu gani kimefanya biashara hii kukua kwa kasi kwenye miaka ya karibuni na ni wapi ambapo jezi hizi zinapotengenezwa na Je wahusika(timu za mpira wa miguu) wananufaika vipi na biashara hii.?
 
Timu ambazo Jezi zake zinauzika sana kwa sasa:-
1.Simba
2.Yanga
3.Wolves(Astropay ya Njano sanasana)
4.Al-Nassr
5.Mamelodi sundown
6.Real Madrid
7 Inter miami
8.Azam(Nyeupe na ile ya Njano)
9.Zanzibar Heroes
10.Manchester United(Team Viewer) etc

Unaeza ukaongeza hapo chini timu zngne zilizosahaulika..
 
No 3 ndo imekua vazi LA Taifa, kila mtu ako nayoo.
Hata mie nilinunuliwa, ila nlimpa mtu mwngne.
 
Kama ni kwa mtiririko ingeanza hiyo ya wolves.
Aisee haiwezi pita siku usikutane na mtu alievaa hiyo jezi
 
😅😅😅Mulemule,,ya wolves imekuwa sare kitaa
 
1. Man City light blue
2. Madrid white
3. Bayern white cream
3. Madrid black
4. Al Nasr green
5. Inter Miami black pink
6. Ajax
7. Tottenham
8. Man U
9. Arsenal
10. Liverpool white green
Yes Liverpool light green nayo imetembea sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…