Biashara ya korosho

Biashara ya korosho

Habari wale wadau wa korosho,ambao wapo mkoani mtwara kwa kipindi hiki tukutane hapa kwa ajiri ya kupeana update na kusaidiana kutatua changamoto tunazo kutananazo
Karibuni.
images.jpg
 
nikitaka kununua ni shs ngapi kwa kilo msimu huu?
 
Naomba kujua bei ya jumla kwa korosho zilizobanguliwa.
 
Tandahimba na Newala kwa mnada wa mwisho bei ilikuwa 4007 kwa kilo....
 
Jaribu kutoka kidogo,nauli haizidi 28,000.Ukitaka kutengeneza pesa njoo mkoani,huku ndo kwa watafuta mitaji,ila dar maisha yakikunyookea s mchezo.Kama huna pa kulala nitakupa lifti
 
Honestly i can say kwa miaka miwili tangu mh rais Magufuli kwa upande wa kilimo zao la korosho limeongezeka bei kwa 200%. Sijajuwa kwa nini miaka ya nyuma hili zao lilikuwa chini sana hadi wakulima wa Lindi na Mtwara kuañza kuliacha kwani halikuwanufaisha hata kidogo.

Mwaka 2016 ndipo wakulima walifuta machozi yaliyotoka kwa miongo kadhaa,bei ya 1kg ya korosho iliuzwa kwa bei ya sh3500+ kutoka bei ya awali ambayo ilikuwa sh1400.Wakulima wa zao hili la korosho walifurahi na kufarijika kwa kuuza kwa bei nzuri kabisa.Mwaka huu bei ya 1kg ya korosho ni sh 3900+ hadi 4000.

Nilinunuwa shamba mwaka 2015 but mwaka 2016 nilianza rasmi kuhudumia shamba kwa ajili ya msimu wa mwaka huo.Japo sikuweka nguvu sana kutokana na uwoga for the first tim lakini nilipata tani 2 àmbazo ni sawa na sh mil7±.

Baada ya kuona kumbe korosho ni ya forex trade ndipo mwaka huu nikatanuwa wigo wa huduma shambani na kununuwa shamba lingine.Nikayapatia huduma kwa wakati sahihi nayo yamenilipa mavuno sahihi.Hadi nimeshavuna zaidi ya tani 5 na shambani bado zipo zipo japo zimepunguwa kiasi.

Am sure nitakunja more than 12million Tsh. Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kulisimamia zao hili kwa sasa wakulima wamesahau machungu ya mbaazi. Maombi yangu naomba musichoke katika hili kwani wakulima wa korosho wapata walichokosa kwa miaka mingi.

My take;
Vijana wenzangu tuache kulalamikà na kutafuta public sympathetic na Ku dream kuwa tajiri through gambling. Twendeni kwenye ardhi kuna pesa nyingi sana.

NB; Nimenunuwa pori hekta 3 nimeangusha msitu mwezi huu December napanda miche ya mikorosho ya muda mfupi.
 
Safi mkuu. Una Jumla ya ekari ngapi ?

Na mikorosho unayo mingapi?

Mi nimenunua ekari 32 nimepanda miche ya kisasa ya mikorosho!?
 
Elezea kidogo kuhusu hiyo miche ya muda mfupi inaanza uzalishaji baada ya miaka mingapi ukiishaipanda.
Pia ninaomba unieleze kifupi korosho asilia, tangu kupanda hadi kuanza kuzalisha ni miaka mingapi?
 
Elezea kidogo kuhusu hiyo miche ya muda mfupi inaanza uzalishaji baada ya miaka mingapi ukiishaipanda.
Pia ninaomba unieleze kifupi korosho asilia, tangu kupanda hadi kuanza kuzalisha ni miaka mingapi?
Muda mfupi Ni ile ya kuzaa kuazia miaka mitatu na kuendelea.

Korosho asilia inachukua muda mrefu kuzaa takribani miaka 8
 
Back
Top Bottom