Biashara pekee isio na risk ni ya kununua viwanja sehemu potential kisha unavikata na kuviuza baada ya muda flani. Hakikisha tu unanuna viwanja sehemu halali na viwe na document zote muhimu.
Hii kitu kuna jamaa yangu inampa pesa sana sema inatakiwa uwe na mtaji mkubwa ambao wewe naona unakutosha sana hata ukianza na million 30 ukaikata hukosi faida ya 10 million ndani ya miezi michache. Zunguka hata mikoani si lazima Dar tu. Miji inatanuka kwa kasi we enenda kwenye miji yote potential.
Kwanini nakwambia biashara hii haina hasara, kiwanja hakishuki thamani. Huwa kinaongezeka thamani with time hivyo sehemu uliouziwa laki 6 leo, mwakani yaweza kuwa million 2 mpaka 3 kwa mji unaokuwa haraka sana.