Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

Wakati mtaani kumejaa maneno kama yako wengine mauzo yanaongeka mwezi kwa mwezi. Game ime-change only the fittest will survive. Be the best,unique....biashara ya mazoea haina nafasi sasa hivi.
Ni kweli usemavyo ila uwe mpambanaji kweli. mwanzo kulikua na mzunguko mkubwa kutokana na wageni asaivi hakuna hivyo inahitaji mbinu kali kukamata soko
 
Ha haa jamaa huenda anapiga sana hela.
Hata ingekua laki 3 ikiwa garatii nipesa nzuri tu
Kwa mwezi? Yaani niweke 80m nisubiri 500,000/- kwa mwezi? Hapana aisee bakini na uwekezaji wenu wa nyumba. Hata Uber inaishinda hio nyumba!
 
Mkuu mi ninakushauri huo mtaji utenge katika mafungu kadhaa.

Tenga milioni 100, tafuta kiwanja/viwanja katika mji wa kiserikali au kibiashara (sio lazima uwe mji mkubwa sana) jenga apartment hata 2 kwa ajili ya kupangisha

Mil. 30, weka hardware maeneo ya miji inayojengeka kwa sasa

Mil. 30 wekeza kwenye biashara ya kununua na kuuza viwanja

Mil. 20 weka benki ya saving, kusubiri mchongo wowote (kumbuka kuna kipindi unaweza letewa mchongo wa maana kwa bei ya chini kwa kuwa muuzaji ana shida sana ya hela)

Mil. 20 iliyobaki iwepo kwa ajili ya back up endapo kuna shida itajitokeza kwenye business nyingine

Sikushauri uwekeze kwenye

1. Kilimo kama huna mzuka na kilimo na kama hujawahi kulima

2. Kwenye madini (kimbia kabisa)

3. Fixed account
 
Kwa mwezi? Yaani niweke 80m nisubiri 500,000/- kwa mwezi? Hapana aisee bakini na uwekezaji wenu wa nyumba. Hata Uber inaishinda hio nyumba!
Ni kweli ila kupata kiduchu chenye uhakika tena cha kudumu si sawa na kubahatisha
 
Mimi nilimuuliza anahitaji bilioni ngapi?
Yani kwa kipindi hiki kuingia kwenye biashara usio ijua uwe na bahati sana kukutana na watu sahihi ndo utoke.

Myaka tisa ni palefu sana tena ukiwa mchimbaji kwa maana alikua akipata mawe ya kusukumia siku yani kuanzia laki hadi miloni kadhaa.

Akiwa mchuuzi wa bidhaa hizi pia anawezankulinda fedha yake na akapata ufumbuzi mzuri.
 
Yani kwa kipindi hiki kuingia kwenye biashara usio ijua uwe na bahati sana kukutana na watu sahihi ndo utoke.

Myaka tisa ni palefu sana tena ukiwa mchimbaji kwa maana alikua akipata mawe ya kusukumia siku yani kuanzia laki hadi miloni kadhaa.

Akiwa mchuuzi wa bidhaa hizi pia anawezankulinda fedha yake na akapata ufumbuzi mzuri.
Mkuu umewahi Fanya biashara ya madini?
 
Million 200 dhahabu hizo ni kilo si chini 300..

Acha masihara mkuu..

Unamaanishaa nn hapa,,,,dhahabu hizo ni kilo si chini 300??
Inawezekana kabisa kupata 200m kwa mda aliopambanaa na ni dhahabu kg mbili na gram kadhaa waweza pata m 200 kutegemeana na bei ya soko
 
Wazo jengine fungua kampuni ya kubeti, inalipa sana awamu hii ya vyuma. Kwa huo mtaji nadhani unatosha kupewa kibali na serikali. Kama watazingua omba patnership na jamaa waliotangulia kufanya hio biashara uanze kula share yako ya kutosha kila mwezi kama moja ya wakurugenzi.
hili wazo lina Afya mnooo" awamu hii uki invest kwenye kamali ".. unatusua
 
Prondo,mimi siyo mtaalamu wa mambo ya biashara lakini kwa mtaji wa milioni themanini na kuingiza laki tano kwa mwezi siyo mbaya. Ni biashara halali chache sana ambazo unaweza kupata faida ya zaidi nusu milioni kwa mwezi kwa mtaji wa milioni themanini.
yaani ml.80 niiwekeze halafu nitarajie kupata faida ya ml.1 kwa mwezi... huo ujinga siwezi kufanya Aisee
 
Back
Top Bottom