Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

Nzuri hii
 
Ukijenga nyumba ya m80 unaipangisha kwa bei gani kwa mwezi? 500,000? Fikiria mtu anawekeza kibanda cha TigoPesa mtaji haufiki 5m kwa mwezi anapata over 1m kulingana na eneo, wewe ukajenge nyumba m80 upate kodi kwa mwezi 500,000/-!
 
Ukijenga nyumba ya m80 unaipangisha kwa bei gani kwa mwezi? 500,000? Fikiria mtu anawekeza kibanda cha TigoPesa mtaji haufiki 5m kwa mwezi anapata over 1m kulingana na eneo, wewe ukajenge nyumba m80 upate kodi kwa mwezi 500,000/-!
Biashara ya nyumba ni nzuri ila maeneo ya kupata wapangaji wa kukulipa kodi ya uhakika ndio hubaki tatizo

Maana kama ukipata kujenga vyumba vyako kumi na tano na kila chumba ukawa unapata elf arobaini kwa mwezi inaweza kukutengezea kama laki sita kwa mwezi

Ukija kwa mtu mwenye kibanda cha mpesa Tigopesa akiweka mtaji wa m 5 atapata zaidi ya hiyo laki sita kulingana na maeneo ilipo biashara yake
 
Biashara pekee isio na risk ni ya kununua viwanja sehemu potential kisha unavikata na kuviuza baada ya muda flani. Hakikisha tu unanuna viwanja sehemu halali na viwe na document zote muhimu.
Hii kitu kuna jamaa yangu inampa pesa sana sema inatakiwa uwe na mtaji mkubwa ambao wewe naona unakutosha sana hata ukianza na million 30 ukaikata hukosi faida ya 10 million ndani ya miezi michache. Zunguka hata mikoani si lazima Dar tu. Miji inatanuka kwa kasi we enenda kwenye miji yote potential.
Kwanini nakwambia biashara hii haina hasara, kiwanja hakishuki thamani. Huwa kinaongezeka thamani with time hivyo sehemu uliouziwa laki 6 leo, mwakani yaweza kuwa million 2 mpaka 3 kwa mji unaokuwa haraka sana.
 
Wazo jengine fungua kampuni ya kubeti, inalipa sana awamu hii ya vyuma. Kwa huo mtaji nadhani unatosha kupewa kibali na serikali. Kama watazingua omba patnership na jamaa waliotangulia kufanya hio biashara uanze kula share yako ya kutosha kila mwezi kama moja ya wakurugenzi.
 
asante ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…