Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Kutokana na ripoti ya umoja wa mataifa kupitia shirika la WFP, nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara zinakabiriwa na ukame, hilo huenda likasababisha ukosefu wa chakula miongoni mwa jamii maskini.

Kutokana na ripoti hizo, ndipo nikaja na wazo la ujasiliamali baada ya kuona mambo ya ajira hayasomeki, ikichukuliwa sasa hivi ndo niko mwaka wa mwisho chuoni.

Kama habari inavyojieleza kuna mikoa yenye njaa hapa nchini kama vile Simiyu, Dodoma, Singida na kwingineko.

Kwa sasa niko Kigoma likizo-nyumbani, so wakati wa mavuno mahindi huwa bei chee huku, mfano gunia la debe 6 huwa ni Tsh 35,000/= tu. Sasa ndipo nimefikilia kwa mtaji wangu wa Tsh 1,000,000/= ambayo ni kujipinda na kuweka hela ya bumu ninaimani nitaipata.

So, kwa wakazi wa mikoa hiyo na mingine, pia wazoefu wa hii biashara ya kuchukua mahindi huku na kuyasaga unga wa dona na kuyauza mikoa hiyo siwezi kupata faida?

Nawasilisha.
 
Namimi nasubiria ushauri wa wadau ninahunia zangu 200 hapa Korogwe Tanga
 
Wakati unasubiria Ushauri hebu endelea kufanya. Timiza ndoto zako kutokana na kile ambacho hisia zako zimekituma, ukitegemea hisia za MTU mwingine katika kutekeleza wazo lako utapotea. Hakuna jipya chini ya Jua kila wazo LA biashara limeshafanyiwa kazi, sasa kilichobaki ni INNOVATION+COMPETITION, ndy njia pekee ya kukufanya uweze kuishi katika biashara. Timiza Lengo lako biashara iko more theoretically haitabiriki wala haina specific definition ndy maana watu wa kitaa Layman's wanatusua wakati wasomi wanabaki na SWOT Analysis kwenye makaratasi
 
Ungawa ulio packed unaliwa sana Mijini ambapo vjjijin sana hudaga mahindi kwenye mashine.

Mjinj ni kutokana na ubize wa watu kwenda kusaga mahindi.

Kuhusu kusaga Dona inakuwa haina faida sana kwa sababu watu wanao pack ubga hupata pesa kupitia pumba ambazo kama mwaka huu mwanzoni Gunia la kilo 50 lilifika 40,000.

Sembe ndo nzuri. Pia lazima ujue consumer behaviour ya watu wa huko unako taka kuwauzia unga,
 
Nashukuru sana kijana, kumbe pumba zinafaida kubwa hivyo?
 
Mkuu naomba ushauri kuhusu machine bora
 
Hangaika na vingine. Swala la mahindi niachie mimi, naomba tender.
 
Mdau tunaomba mrejesho wa project yako hiyo ya kusaga nafaka.. mafanikio n.a. changamoto mkuu
 
Habari wakuu.

Natafuta mtu wakufanya nae biashara ya unga wa sembe na dona.njoo na milioni 25 tufanye Kazi hiyo pamoja .

Eneo nimeshanunua kibaha jengo nimeshajenga bado kuweka mashine na umeme wa 3 face Kiwanda ni kukubwa na kina store pia.

Nilipanga nimalize December mwaka huu kiwanda kianze kazi lakini mipango haijakaa sawa au kwa anayejua taasisi inayowezesha viwanda kama hivyo Kwa mkopo.

Kwa muhitaji tuwasiliane PM
 
Mkuu kiwanda kikianza kazi mm nipo kwa ajili ya malighafi ya bidhaa unayo zalisha. Nikimaanisha ya kwamba kwenye suala la Mahindi nitakuwa nakuletea mzigo utakao, Karibu sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…