Asanteni Varbo na Chungurumbira.
Chungu: sijakupata vizuri mkuu.
Inakupasa upate peeling machine nzuli possibly SN machine is the best ktkt kukoboa, pia combined mashine ya kuchekecha kutoa vumbi na magunzi. Pia mchanga, capacity yake ni kubwa sana na inafanya kazi nzuli sana ktk kukoboa haivunji mahindi hii, ktk kutegeneza donna grade 1 ndo yeneyewe
Kwangu mimi nilitaka tu kukupa ushahuri kuwa utakapokuwa umekamilisha ujenzi wa majengo ya mitambo na store basi nitafute nikupe ushahuri wa mashine, katika dunia ya leo hatutumii tena roller machine kwa kukoboa kwani inakuwa na wastage kubwa ya mahindi, wastani wa gunia la kilo 108 kgs kwa roller machine utajikuta unapata kg 75 au 78 za mahindi, lakini kuna mashine za kisasa output baada ya kukoboa inakuwa kg 92 hadi 95 ktk gunia la kg 108 hii inakupa faida kubwa na tija zaidi, ukiamua kutegeneza unga wa dona machine hii ndo yenyewe, capacity yake ipo ya ton 20 kwa siku, 30tons kwa siku hadi 50tons inategemea utaaamua kutumia hammer mill au vip, hata hivyo ktka kusaga kama utaamua kutumia hammer mill ni wakati mzuli kupata vinu vizuli vya kisasa kabisa vinavyotumia motor ya HP50 vinu 3 stainless steel unga unakuwa bora sana na sio carbon steel mill,
haya bwana kazi ni kwako, thanks
Bei ya kutengeneza kinu cha kusagia mahindi cha panga 8 ni 1.5ml bila mortar (sina uhakika na spelling za mota kwa kizungu) kinu cha kukoboa ni 1.3 mpaka 1.4 bila mortar. Mortar ya 40HP ni 1.3mil that means utahitaji mbili kwa mashine zote i mean kusaga na kukoboa. Bag sealer (mashine ya kuishonea viroba) hizi ni cheap we andaa kama 250000 mpaka 300000 kwa mashine moja ila za india ni nzuri zaidi. If you need more info we ni pm mkuu nipo huko kwa muda sasa.
We jamaa una mawazo km yangu,safi sana mkuu.Mawazo mazuri sana!
Je, hakuna uwezekano wa kuziendesha hizo mashine zote tatu (ya kusaga, kukoboa na kushona mifuko) kwa kutumia umeme wa Solar?
Nikiwa na 20M siwezi kuanzisha mradi huu.
Njaa yangu ni kutumia pumba kwa ajili ya kutunza kuku wa kienyeji, ng'ombe na nguruwe (a.k.a Noah).
Kuhusu mifuko inapatikana kkoo ila kutengeneza label kwenye mifuko mm nafanya hiyo kazi tuonane mkuu.Asante Concordile 101.
Naona.mwenzangu walau una ABC...
Kwangu navuta three phase maana naanza na vitu vikubwa size 100 ya kusaga na roller tatu ya kukoboa na nimejenga nyumba pia ya wafanyakazi of which wataishi pale pale na huo mlango mkubwa wa kiwanda uko sambamba na dirisha la masterbed room hahaha lakin nafikiria kuweka security camera maana always labour ndo changamoto kubwa. Nina store inaweza kuchukua hata gunia 500 za mahindi ila nafikiri inabidi kuyatreat. Ntaomba mwongozo wako mkuu hasa kuepuka mahindi kuoza na unga kupata fungus maana nataka nianze na stock ya walau ton tatu. Pia sijui napata wapi mifuko na lebeling zake na je nilazima usajiri TBS na TFDA?
Itabidi nikutafute mkuu nami nataka kufanya biashara hii maelezo yako yamenihamasisha sana asante kwa ushauri huu.Mkuu mimi niko dar. Ni kweli kuwa kwa sasa kuwa watu wengi wanakula dona. Lakini kumbuka kuwa kama unatengeneza dona lazima uwe na oda kabisa na uwe makini na mahindi unayo nunua, mengine wanaweka dawa ku-prerve. Kwa hiyo wakati wa kutengeneza dona ni lazima uyaoshe Ni vigumu Kwa uzoefu wangu kutunza unga wa dona kwa muda mrefu. unavunda haraka kwa sababu mahindi wanakauka kwa kutumia joto la jua hivyo ku-control moisture content ni vigumu unless una unakausha hayo mahindi kwa njia ya kisasa zaidi. Pia swala la mizani uwe makini. Wakala wa vipimo huwa wana mizana ambayo weme-certify/recommend unaweza ukawaon wakakushauri. kupunguza usumbufu na imani kwa wateja mimi nilinunua mzani mkubwa wa digital wenye capacity ya 100kg for about 1M. Pia kumbuka kutengeneza nembo yako.