Mashine zipo kwa size,nashauri kwa kusaga sembe kinu cha kusaga utumie size 100,na chakukoboa tumia roller 3 au roller 4,Vinu imara kwa hapa bongo ni vya kuchonga kwenye viwanda vidogovidogo vya bongo ndio vizuri, coz madukani vingi ni vya kihindi mabati yake ni laini mno hua havidumu, lakini pia sijawahi ona kinu cha roller 3 cha India.Mashine zote hizi zinahitaji motor ya hzp 40 ambazo moja ina range 1.3-1.5 Tsh inategemea jinsi utavyoipata,Mimi niko huko kitambo na wiki iliopita nilitengeneza chakusaga size 100 kwa 1.4 na chakukoboa kwa 1.2,vinu hivi vinauwezo wakusaga 1tone/hrs.