Biashara ya kufanya mtaji 30 milioni

Biashara ya kufanya mtaji 30 milioni

Huu ujinga umewahi kunikuta mimi aisee mleta mada awe makini Sana aiseee
Kweli, wanaume tunalalamika ndoa zina matatizo ila hakuna mwanaume utakua na akili alaf mwanamke ambaye wewe ndio umemtafuta mwenyewe aje kukusumbua akili,
Mama zetu sio kwamba walikua na adabu sana kudumu kwenye ndoa, ni akili za mwanaume kwenye kuchagua mwenza atakayeendana nae, ndio maana zamani mtu alikua anachaguliwa mwenza na wanadumu, wazee wanakujua mtoto wao na wameona mengi hivyo akikuchagulia mtu lazima mtadumu milele
 
Anataafutwa mke hapo, hujaelewa nini? Hiyo habari ya biashara ni ulimbo tu wa kunasia. Akili mtu wangu.
Shida yenu vijana wa Tanganyika ndo hio mkiona mtu kaongea kitu akaeka na habari ya ndoa mnafananisha akili zenu na mihemko yenu ilio wafanya mkimbilie ndoa kwa kubugi jambo ambalo linawafanya mnajuta mbaka leo .Nikufahamishe tu kijana mwenzangu kwamba Tanzania hii hii kunavijana wenye focus kubwa sana kwenye haya maisha na wanapambania ndoto zao usiku na mchana naswala la ndoa au familia ni ishu ya extra sana na hakili hio haijaja baada na kubugi na kukimbilia majukumu bali ni ndoto za mtu nakuji control kwenye mambo ya mihemko.Najua kabisa wewe hapo ulipo ushajichanganya na Ushabugi ndo mana unawaza negativity nakuamini vitu haviwezekani.
 
Kwa upande wangu, kabla hujaaza kufafa chochote lazima kwanza ujue changamoto zake, hasara na faida, iwe biashara, kilomo au ufungaji na uvuvi. ukisha jua changamoto hasara na faida, chagua unachoona utakimudu. Miti ya mbao ni mizuri ila na yenyewe inahitaji matuzo, kumbuka adui wa miti ya mbao ni moto hivyo inahitaji sana uangalizi.
🙏
 
Juzi nimeomba ushauri kuhusu biashara ya kufungua pharmacy kwa mtaji wa 30m nitafute mwanamke mwenye diploma ya pharmacy nimuoe aje akae kwenye hio biashara.

Ila comment na ushauri mwingi kutoka kwa waja walishauri nisije karibu kufungua biashara na kumuweka mke.

Kwakweli Mimi kwaupande wangu naamini biashara ni usimamizi na mm saivi niko kwenye ajira ya serikali nanilipo kuwa nataka kufungulia hiyo pharmacy nimbali kidogo na eneo langu la kazi .lengo langu ni hapo badae nije kuachana na ajira nifanye biashara wakati zikiwa zimesha simama ,

Option ya pili baada ya pharmacy ilikuwa ufugaji wa nguruwe ila nimefanya utafiti nimekuja kugundua huu ufugaji unaugumu sasa kutokana naulishaji pia kama uzalishaji nimkubwa soko lake ni finyu kidogo.kuna mtu kanishauri nitafute shamba nipande miti ya mbao baada ya miaka 10-15 nitazalisha hela nyingi.

Mwingine kanishauri nitafute eneo ninunue mbuzi 100 nifuge bada ya miaka mitano makadirio yakati ntakuwa nimesha zalisha mbuzi kama 1500 na soko la mbuzi liko juu sana.

Ushauri wenu wadau wangu!!.
Anzisha danguro, inalipa kichizi.
 
Kwa mtaji wako kiongozi kama sio mkopo basi una uwanja mpana wakutumia pesa zako ,Mimi Niko na mawazo 2 ,ambayo ni Financial services pamoja na ardhi (kilimo).

Financial services,hii inaitaji tu mfanyakaz mwaminifu pamoja na location ya mzunguko ndipo kutakua na faida kubwa hii asara zake labda tu mfanyakazi akosee kufanya muamala tofauti na hapo ni maokoto tu .

Ardhi (kilimo)
Ardhi unaeza kununua na kua na hati miliki ukawa umetunza ela zako bila kuhitaji msimamizi na ardhi Kila siku thamani inapanda juu mfano kwa huku kwetu mbeya kwa baadhi ya maeneo aridhi yake inagharama sana na inapanda Kila siku

Either ununue ardhi Kisha ufanye kilimo Cha muda au Cha muda mrefu kama kupanda miti .nb shambani Kuna ela sana kwa huku kwetu kwa kilimo Cha kiazi na mahindi.
Thanks 🙏
 
Juzi nimeomba ushauri kuhusu biashara ya kufungua pharmacy kwa mtaji wa 30m nitafute mwanamke mwenye diploma ya pharmacy nimuoe aje akae kwenye hio biashara.

Ila comment na ushauri mwingi kutoka kwa waja walishauri nisije karibu kufungua biashara na kumuweka mke.

Kwakweli Mimi kwaupande wangu naamini biashara ni usimamizi na mm saivi niko kwenye ajira ya serikali nanilipo kuwa nataka kufungulia hiyo pharmacy nimbali kidogo na eneo langu la kazi .lengo langu ni hapo badae nije kuachana na ajira nifanye biashara wakati zikiwa zimesha simama ,

Option ya pili baada ya pharmacy ilikuwa ufugaji wa nguruwe ila nimefanya utafiti nimekuja kugundua huu ufugaji unaugumu sasa kutokana naulishaji pia kama uzalishaji nimkubwa soko lake ni finyu kidogo.kuna mtu kanishauri nitafute shamba nipande miti ya mbao baada ya miaka 10-15 nitazalisha hela nyingi.

Mwingine kanishauri nitafute eneo ninunue mbuzi 100 nifuge bada ya miaka mitano makadirio yakati ntakuwa nimesha zalisha mbuzi kama 1500 na soko la mbuzi liko juu sana.

Ushauri wenu wadau wangu!!.

ushauri wangu jipe mda kwanza.. sababu ulizoweka hapo juu kwa nini unataka kufanya biashara na jinsi ulivyoplan kuiendesha hiyo biashara tayar tunasema hiyo biashara ni "dead on arrival"

unatakiwa kujua mchawi wa kufanikiwakwenye biashara ni vitu viwili aina ya biashara unayoitaka kwa maana ya kuifanyai reserach na pili ni time managment.. watu wengi wanafeli sababu hawalipi uzito swala time management.. kumbuka wazo na mipango ya biahsraa unayo wewe kichwani... haijalishi msimamizi ni nani kama hamshei common goals hiyo baishara its doomed to fail. na mbaya zaid msimamizi akiwa mna vinasaba vya mahusiano awe mke au ndugu

ushauri wangu sababu una ajira .. tulia.. iweke hiyo pesa sehem (sio saving account) iwe fixed au wekeze sehemu walau hata izalishe faida kdogo kwa maana ya kuilinda thaman yake .. ili uweze kujipa mda wa kutafakari kwa kina hasa kwenye swala la time managment.. kwangu mie sasa hivi hauko tayari 30m ni nyingi ikiwa bank au mfukoni ukishaiweka kwenye biashara ndio utajua ni pesa ndogo sana. take your time hauko tayar kwa biashara inaeleka unauhitaji wa kutengeneza mrija wa pili wa income ila bado hujajipanga.

fanya research. dunia kijiji sasa hivi.. tafuta elimu ya fedha na uwekezaji na jinsi ya kumanage mda .. utaona kwa position yako uwekeze vipi pesa yako. usitake kufungua biashara ambayo mafanikio yake itahitaji 100% of your time huku ukiwa na ajira.. lazima kimoja kifeli aidha biashara au kazi yako..
 
Back
Top Bottom