Biashara hazijawahi kuisha chini ya jua ni vile tu unavyoamua kuchukulia mambo na kujichukulia wewe upo vipi,leo nataka nimsaidie mtu mmoja mahali flani kuichambua hii biashara ili kama alikua akiwaza nini chakufanya na hapati apate pakuanzia,na kwa wanaoifanya basi waboreshe ili mwisho wa siku urudi nyumbani ukiona mafanikio ya kazi ya mikono yako.
Kwanza nataka utambue hakuna biashara yyte chini ya jua kwasasa utakayoianzisha ukawa peke yako, kwahyo ondoa yale mawazo aah biashara hii kila mtu anaifanya, kila hatua mbili mtu anaifanya,nk ukiona biashara yyte kila mtu anaifanya sio kwamba eti ni rahisi ila ni kwasababu Kuna pesa ktk hiyo biashara, sasa kama na wewe utaamua kupishana na pesa kisa kila mtu anapesa ni sawa, vizuri.
Mahitaji ya hii biashara makubwa ni
1. Meza
2. Mwamvuli
3. Computer
4. Moderm
5. Benchi
6. Radio
Yawezekana upo unatafuta kazi na una mtaji flani au huna mtaji kbisa lakini una weza kutumia computer vizuri na pia una computer,hapa yaweza kuwa laptop au desktop ilimradi ni computer yoyote ya uwezo wowote inatosha na inafaa kukurudisha nyumbani na pesa,kuliko kukaa bure.
Unaifanyaje hii biashara sasa kwa wewe unaetaka kuanza kuifanya?
Amka hapo ulipo tembea nenda huko barabarani tafuta duka la mtu ambalo lina kibaraza kwa mbele au sehemu yyte unayoweza kuweka meza yako na ukapata pakui hifadhi usiku wakati wa kuondoka,au inaweza kuwa hata kisehemu cha pub,NK mtafute muhusika muombe kukaa eneo lake na mueleze nia yako na unachotaka kukifanya na kwmba unahtaji 1.eneo lake 2. Umeme wake 3.Kuhifadhi vitu vyako wakati unafunga usiku.
Utakapopata nadhani sasa kazi itakua kwako kufata vitendea kazi vyako na kuja navyo site kuanza kazi rasmi,Hakikisha meza yako mbele umechora huduma unazotoa kisha njoo kazini tulia pale.
Watu wengi wakiskia huduma ya kuingiza movie au miziki wanadhani n lazima computer iwe na nafasi kubwa sana ya kuhifadhi miziki ya tangu enzi zileee,hapana si lazima Japo ni vizuri kama ungekua na vihifadhi data (hdd) ili kufanikisha kazi yako kwa urahisi kidogo lakini kama huna nayo sio kesi unaweza kuanza hivyo hivyo ndio mana ktk mahitaji pale juu nilisema Moderm inahitajika.