Biashara ya kuingiza movie na miziki kwenye flash na simu

Hivi ukiwa laki 5 unaweza ianzisha mkuu
 
Kweli huu. Hii biashara nilikuwa naichukulia poa kumbe vijana wanapata.

Juzi nimeona kijana kaweka meza mbele ya duka la mtu. Ananiambia kuna siku anafikisha 80,000. Wimbo mmoja 300.
 
Zipo desktop complete set mtumba kwa laki 3 au pungufu kidogo. Nzuri, imara na HDD 500. Hii inatosha kwa kuanzia. Hapo utabakiza chenji laki 2 ya kununua ya mziki.

Meza, extension cable na elfu 30 ya kifaa cha internet.
Shukrani mkuu Ngariba1 kwa kunipa mwangaza.
 
Bado najifunza hii kazi mimi niliifanya kitambo miaka ya 2008-2013 hivi kulikua na hela balaa wimbo mmoja kwenye simu naweka buku, CD ya Picha/video vcd 7000 DVD 10,000/copy mpaka Nilinunua Pikipiki kwa hela hizo
 
Ubarikiwe mkuu. Si watu wengi wenye moyo wa kushare mianya ya kuzalisha fedha. Hopefully watu watafanyia kazi na kubadili mentality za lazima kuajiriwa ili kuendesha maisha
 
Idea yako ni nzuri ..na siku hiz watu wanafungua office ya maana ya kueka movies mfano na movie moja inaekwa kwa 1000.nje jamaa wanaeka tv umoja ambayo ina trela za movies mpya ukiingia ndani kuna kochi na tv iko ukutan so movie jamaa aki play kwenye computer unaiona kwenye tv yaan office ziko smart kweli
 
Mkuu kongole najimeki kamshahara mwezi huu nivute COMPUTER MACHINE tu. Maana vifaa vifuatavyo ninavyo:
1. Monitor ipo inchi 17
2. Subwoofer ipo watt 65
3. Ujuzi wa computer upo wa kutosha
4. Moderm zipo 2 (moja inafanya kazi pia kama kadi reader)
5. External hdd 320GB ipo moja

NACHOPAMBANIA KWASASA:
1. Computer machine nzuri machine tupu
2. Na iwe na internal tera 1 hivi
3. Niijaze mazaga yote nianze kazi mkuu.

Nakibarua kinanipatia vijichenchi kiasi ila mambo magumu mkuu embu nifanye hii kazi kwanza. God bless me.
 
Huu ni ukweli mkuu....mada zako huwa ni za uhalisia,kama ile ya kutumia kipaza sauti kwenye biashara....niliwahi kufanya hii kazi pale machinga complex miaka ya 2013-14 aisee kila unachokiongea ni kweli,hiyo ya mtu kukupa buku 5 imewahi kunitokea tena ilikuwa kumuwekea whatsapp kwenye simu yake,jamaa alikuwa mfanya biashara ya mitumba wale wanaofungua belo za suruali asubuhi,unakuta vitu vidogo sana unaingiza hela bila kukaza misuli na kutoka jasho...

Tulianzishaga internet cafe ya kutumia modem ya kawaida tukawa tunajiunga kifurushi cha buku moja akija mteja analipa jero au buku kwa nusu saa,unashangaa wanakuja watu wenye heshma zao kukata tiketi za ndege online wafanyabiashara wanaoenda china na kwingineko.....na anakuta computer moja haulizi anajali huduma tu kumbe unaweza anza kiutani utani baadae unakuja itwa freemason.

Unaweza usiamini mpaka leo kuna watu hawajui kutumia smart phone zao,mambo ya kudownload whatsapp,instagram,sijui youtube hawayajui kabisa na unaweza piga hela hapo hapo mtaani iwe dar au mkoani.
 
Hatari sana
 
Mkuu hii biashara ongea tu kwa kua huijui kwa zamani ata ungeanza na terabyte 1 unatoboa ila sasa mkuu bila kua na kuanzia terabyte 20 unafukuza upepo mtaji wake sio chini ya million 1 kma unataka uone pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…