Biashara ya kukopesha: Ni vitu gani tofauti ya kuandikishiana naweza kuchukua kwa ninaye mkopesha?

Biashara ya kukopesha: Ni vitu gani tofauti ya kuandikishiana naweza kuchukua kwa ninaye mkopesha?

jiwekuu770

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
2,246
Reaction score
1,645
Wakuu heshima yenu,

Nimeanza biashara ya kukopesha!! Nimeandaa daftari la kuandikishana ila kuna watu wengi tunashindana kwa sababu kila wakija nawaambia waniachie kitu ndo nimpe pesa wengine wanakataa kwani kwingine hawaletewi masharti ya hivo!!

Nilkua naomba ushauri, tofauti na kuandikishiana nifanye nini kingine ili nisidhulumike?

Ni Vitu gani unaweza ukachukua kama unataka kumkopesha MTU? (10,000-100,000)

Kwa ushauri
Wataalam na wenye uzoefu tafadhari
 
Nikopeshe kwanza 5k tuamini isije ikawa polojo tu hapa Alfa ulela
 
sajiri microfince yako na ufanye biashara halali.. chini ya hapo itakula kwako..

maana watu watakopa na hawatakulipa na hutakuwa na cha kuwafanyaaa...
Kusajili microfinance unatakiwa uwe na mtaji wa angalau milioni 200 kama sijakosea. Hiyo biashara ya kukopesha inaweza kuwa nzuri, ila tatizo kukusanya madeni ndio kimbembe hasa kama unakopesha ndugu na jamaa / marafiki wa karibu. Ili ufanikiwe inabidi uwe bandidu / mbabe mbabe saana.
 
Hii biashara imeliza watu hapa mtaani kwetu,.nakumbuka last month mtu wangu wa Karibu sana na mm aliniomba nimsindikize kumdai mtu ambaye amemzungusha toka July mpka dakika hii na hajaambulia kitu,..
 
sajiri microfince yako na ufanye biashara halali.. chini ya hapo itakula kwako..

maana watu watakopa na hawatakulipa na hutakuwa na cha kuwafanyaaa...
Kusajiri si inahitaji mtaji mkubwa sana
 
wakuletee hati za viwanja, vito vya thamani kama dhahabu nk, kadi ya gari, shares certificate etc
Sasa shida ni kwa hawa wanaokopa elf 20,10,50 ad 100000 huyu MTU ukimwambia akuletee hati ya kiwanja hamuelewani!! Ebu niambie labda vitu vya kuchukua kwa viwango hivo
 
ukikopesha usiandike umemkopesha andika umemwazima alaf usiandike kwa riba andika jumla ya fedha yote ni sh 120000 kama umemkopesha laki!
Hii n kisheria ukiandka umemkopesha kwa riba n kosa LA jinai
 
Somo hapa kuwa makini kidogo

Ushauri umegawanyika hivi,

Sajili business name ambayo itakuwa inashughulika na kuwashauri wafanya biashara wadogowadogo kwa masuala ya kifedha, alafu baada ya kuisajili, katika majukumu weka kuwa ni kuwakwamua kwa ushauri pengine na kifedha wanapokwama, sasa kupitia hapo, uwe unawakopesha kwa riba ila katika kuandikishana usitaje neno riba, maana huruhusiwi kufanya biashara, hii ,unachipaswa kufanya we kama umempa 200,000 arejeshe 240,000 andika umempa 240,000 kabisa kama umemuazima, ili umdai hiyo, na pia usikubali dhamana bila kujua umiliki na ubora wake

USISAJILI MICROFINANCE NI GHARAMA KWANZA HUTAIWEZA
 
Somo hapa kuwa makini kidogo

Ushauri umegawanyika hivi,

Sajiri business name ambayo itakuwa inashughulika na kuwashauri wafanya biashara wadogowadogo kwa masuala ya kifedha, alafu baada ya kuisajili, katika majukumu weka kuwa ni kuwakwamua kwa ushauri pengine na kifedha wanapokwama, sasa kupitia hapo, uwe unawakopesha kwa riba ila katika kuandikishana usitaje neno riba, maana huruhusiwi kufanya biashara, hii ,unachipaswa kufanya we kama umempa 200,000 arejeshe 240,000 andika umempa 240,000 kabisa kama umemuazima, ili umdai hiyo, na pia usikubali dhamana bila kujua umiliki na ubora wake

USISAJIRI MICROFINANCE NI GHARAMA KWANZA HUTAIWEZA
Sawa mkuu
 
Chukua vyeti vya ndoa... Waaambie wakishindwa kurejesha unaenda Mahakamani kuvunja ndoa, na kuwatenganisha wanandoa mpaka walipe deni... 😀😀😀
Weee, mbele ya kuwanyang'anya watu haki ya kupasha joto, mbona utalipwa fastaaa?
 
Ha ha ha [emoji3] [emoji3] [emoji2] we jamaa hauko serious
Chukua vyeti vya ndoa... Waaambie wakishindwa kurejesha unaenda Mahakamani kuvunja ndoa, na kuwatenganisha wanandoa mpaka walipe deni... 😀😀😀
Weee, mbele ya kuwanyang'anya watu haki ya kupasha joto, mbona utalipwa fastaaa?
 
mimi pia ninafanya iyo biashara.sijaisajili bado kwa sababu ninabiashara nyingine naifanya inanikeep bize sana.sijapata muda hasa.
-utaratibu wangu unaacha dhamana kiwanja,hati ya kiwanja au nyumba,kadi ya gari na gari lenyewe,laptop,smart phone kwa kampuni za apple samsung sony htc,au hisa kwenye kampuni flani.
-dhamana unayoiacha ni lazima ivuke 87% ya pesa unayotaka.na huwa ninatoa 60% hadi 80% ya thamani ya dhamana.kulingana na dhamana yenyewe.
-cha muhimu ww kama c.e.o uwe na mwanasheria unayemwamini,uwe na proffesional surveyor kwa ajili ya evaluations,viwanja na nyumba.kingine uwe na watu 5 professional&mixer ambao watakuwa washauri wako.
-malipo ya mkopo wangu ni 17% kila mwezi kwa muda wa miezi 8 au 4.+ amount uliyochukua. yaani 17% kivyake na amount uliyochukua kivyake.wafanyabiashara wengi wamjini wanakopesha kwa 35% interest+ amount ulioichukua/utakayoichukua.
-loan processing fee yangu ni 9% inalipwa kabla au up on loan delivery.
-Ila kwa sasa nakopesha wafanyabiashara wa mazao,wakulima,wafanyabiashara wenzangu wa madini na wanaohitaji kuingia kwenye madini au kilimo/mazao.biashara nyingine ninayokopesha ni jumla na rejareja.Nakopesha wanaotaka kuingia kwenye biashara,cha muhimu dhamana.
-Pia mkopaji anasign transfer documents kwa mwanasheria wa hiyo dhamana yake kuja kwa jina langu.akishindwa kulipa ndani ya siku 90 kisheria namfilisi bila kusuburi sekunde.
-Biashara hii inautajiri wa haraka sana,kuna mbinu na ubunifu.
+255627575354
 
Back
Top Bottom